Wednesday, March 16, 2011

ASKOFU KAKOBE AIPINGA TIBA YA LOLIONDO

Askofu Zakaria Kakobe
Askofu Kakobe alisema Watanzania wengi wanapenda uwongo kuliko ukweli na kutahadharisha kuwa kutokana na kuwepo mtu huyo watu hawatasubiri tena maombezi bali watapukutika kwenda Loliondo.“Hofu yangu iko katika vituo vya maombezi vilivyofurika mjini, wakati huu vitabaki tupu, watu wataenda Loliondo na hawatasubiri tena maombezi,”alisema Kakobe na kuongeza :

“Tukisema tusubiri serikali ama TFDA ituthibitishie itakuwa ngumu maana kila mmoja anatia bidii kama polisi na wengine”.Alisema kanisa lake litaendelea kuwepo na kamwe haliwezi kutikiswa na Loliondo na kujigamba kuwa wanaweza kumsambaratisha mchungaji huyo.

Kakobe alieleza kuwa kwake yuko muhubiri wa Injili iliyo hai na ambayo iko ndani ya Biblia huku akikumbusha mtu aliyemwita 'Babu wa Tegeta' ambaye alijitokeza miaka ya nyuma na kudai kuwa anatibu Ukimwi ambaye alisema walimsambaratisha.Kakobe ambaye alitumia muda mwingi kunukuu vifungu mbalimbali vya Biblia, alisema mfumo wa uponyaji wa Mungu umeshafunuliwa na kwamba kwa sasa hawahitaji Mungu yeyote atoe ndoto.

“Hizi ni nyakati za mwisho, unatakiwa kuchagua kanisa ambalo utaongozwa katika haki na si kupeperushwa kama karatasi,”alisema Kakobe huku akishangiliwa na waumini wake.Aliwatahadharisha waumini wake akiwataka kuwa makini na mchungaji huyo

“Kama umesikia mtu fulani anafanya maombezi la kwanza la kujiuliza je ameokoka kwa sababu Mungu hatendi kazi na watu ambao hawajaokoka, lazima awe anahubiri Injili,”alisema.Askofu huyo alitumia ibada hiyo kuwahamasisha waumini wake kumpinga mchungaji huyo kwa maombi huku akitamka:

 “Tusibabaishwe na Ukimwi, hapa tumeombea watu wamepona Ukimwi na vithibitisho vya vyeti vipo,”alisema Kakobe na kushangiliwa na waumini wake ambao baadhi yao walisikika wakisema, "tupo."

Kakobe alisema hata kama mtu huyo angekuwa anatibu kwa Sh1 kwenye Neno la Mungu haikubaliki na kueleza kuwa maandiko yanasema, 'mmepewa bure toeni bure.'Katika hatua nyingine, askofu Kakobe alisema matatizo ya umeme nchini hayataisha hadi waziri wa Nishati na Madini aende akatubu kanisani kwake. Alisema mambo yanayojitokeza sasa ni matokeo ya yale waliyoyafanya Tanesco kanisani kwake na kutaka Ngeleja akatubu ili matatizo yaishe.


Source : 1.Mwanachi
            2.Sayuni

1 comment:

  1. Haijawai tokea hata siku moja shetani akawa na nguvu kuliko Mungu.
    Kakobe angetupa hesabu matumizi ya fedha za sadaka walizotoa wahumini kwa imani kuwa wanamtolea Mungu.
    Kama sio kubwa kuliko shilingi 500 anayochaji Mch.Mwaisapile.
    Je neno hili
    Ufunuo 22:2, twalifananisha na tukio gani Duniani.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...