Thursday, March 10, 2011

THAMINI HUDUMA YA UCHUNGAJI - DUNSTAN MABOYA

Mtume Dunstan Maboya
MAFANIKIO :- Ni kufikia  pale Mungu anapotaka ufikie, na fedha ni moja kati ya alama za mafanikio.

  • Hata kama mtu akikutabiria  kuwautapata pesa  toka mbinguni,tambua fika kua hautapata fedha ambazo hazimo kwenye mzunguko wa fedha (Money circulation) wa nchi  husika.
  • Nyumba yeyote  haipendezi  kwa maombi  ni pesa , sura za watumishi  na afya  zao  hazipendezi kwa maombi ni pesa  ndio maana leno  utakuta  Pastor  kama kachoka kifedha, kimaombi,kimafunuo hata washirika nao  mkondo ni ule ule .
  • Usibabaike na miujiza ya mtu  kwani miujiza  mbele ya Mungu  ni HAKI  YA KILA MWAMINI. Thamini kazi za mchungaji wako.
  • Pamoja  na kuwapo  kwa huduma  zote tano lakini  huduma ya uchungaji ndio pekee  inayoweka mwamini karibu  zaidi na MUNGU.
 Wakati wa shida mwinjilisti, mwalimu , mtume  na nabii  wanaweza kutoa udhuru  au wakakimbia kabisa lakini mchungaji  atakuwa na wewe mpaka dakika ya mwisho.

  • Elisha  “Nabii “ alimkimba mwanamke Yezebeli  mpaka Mungu  alipomuinua YEHU kwa ajili yake
  •  Paulo “mtume” alipokuwa anatafutwa sana  alishushiwa dirishani  kwa “kamba “na akakimbia .
Mtume au nabii anaweza akakudai pesa  au kukuamrisha utoe pesa kana kwanba ni zake, lakini  mchungaji  atakuacha utoe  kwa hiyari  yako  akiamini Mungu  atakuongoza  kufanya hivyo .

Mara zote mchungaji hufurahi sana pindi  anapoona kondoo zake wamenawiri wako salama. Mitume manabii hujiangalia kwanza wao huku wakijitambia ile nguvu ya Mungu iliyo juu yao. Eliya hakuangalia zaidi hitaji la yule mama mjane aliyesema amebakiza chakula kidogo kwa ajili yake na mwanae, badala yake Eliya akasema Nipe mimi kwanza, ndivyo mitume walivyo.

Kwa kulijua hilo ndio maana Yesu alipokuja duniani pamoja na kuwa na huduma zote tano ndani yake lakini bado hakujitambulisha kama  Nabii, Mtume, Muinjilisti, Mwalimu bali alijitambulisha kwa kusema “Mimi ndimi Mchungaji mwema.

D. Maboya
  

3 comments:

  1. Askofu wangu amenena. Nafurahia sana hayo mafundisho. Ni kweli mara nyingi sisi wachungaji tunategemea mungu anene na watu wake. Natamani sana arudi tena peterborough UK kwenya Faith To Faith Conference 2012. Nawezaje kuwasisliana naye.
    pastor@faithinchrist.org.uk
    Mchungaji Reuben

    ReplyDelete
  2. Mungu akkubariki sana mtumishi Maboya.

    ReplyDelete
  3. aisee ni maneno mazuri sana ya ukweli mnoooo hakuna la kubisha kabisa..ahsante MABOYA

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...