Sunday, March 13, 2011

MTAZAMO WA MUNGU NA MAAMUZI YA MWANADAMU

Toka enzi za baba zetu kiroho kina Ibrahimu, Daudi, Eliya, na wengine wengi  ambao kupitia wao leo tumechukua kijiti cha kumtangaza kristo, suala la maamuzi ya mwanadamu na jinsi Mungu alivyopanga juu ya mwanadamu huyo hukinzana. Nilikutana na mtumishi mmoja wa Mungu ambaye niliamuamini kuwa ni mtumishi mkubwa wa Mungu .Wakati tulipokua tukiongea akaniambia alifanya maamuzi yasiyofaa mwaka 1981, na kuanzia hapo maisha yake na huduma pamoja na huduma yake viliporomoka . Baada yakuachana nae niliendelea kutafakari akilini yake Maamuzi yasiyofaa ya  mwaka 1981, lakini leo bado yameyashikiria maisha yake , hili ni jambo la kulichukulia uzito mkubwa na sio  kama tunavyofikiri.

Hatima ya mafanikio ya mwanadamu iko katika kufanya kusudi la Mungu juu ya mwanadamu huyo
Kila hatua unayochukua sasa, itakupeleka mbele au kuyadhohofisha maisha yako. Moja kati ya mambo yanayogharimu maisha ya wanadamu leo ni kutofahamu nini hasa anatakiwa afanye maishani,mwishoni anajikuta anafanya hili na kuacha kasha anafanya lingine.

Wengi wamekumbuka katika fursa zilizo wazi na zinazoonekana na watu wengi kua ndio bora lakini mwisho wake haziwazalishii kitu chochote.Kubwa tunachohitaji leo nini mpango wa Mungu juu ya maisha yetu. Kwa kua mara nyigi tumekua tukiamua mambo kulingana na mitazamo yetu na siyo mtazamo wa Mungu juu yetu kitu ambacho sio sahibhi. Mithali 16:25 “Iko njia ionekanayo kua ni sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni mauti”.

                                                                         

Kwa kua sisi tu wanadamu hata kama tukiamua kufanya jambo tukiwa tumetulia na kujipanga kwa akili zetu zote, hatuna uwezo wa kufanya maamuzi yakuaminika na yakudumu kwa asilimia mia. Hata kama tutafanya jambo kwa utaalamu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha ndugu na jamaa zetu wasomi(wananzuoni) na wakasema ni sahihi, lakini bado kufanikiwa kwa jambo hilo sio kwa kuaminika na kunaweza ishia katika uharibifu. Hakuna nguvu au ufahamu wa kibinadamu utakaoenda sambamba na njia za MUNGU. Isaiah 55:8 “Maana mawazo yangu sio mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu”.

Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake

Tunapokosea kufanya maamuzi yaliyo sambamba na hatima ya Mungu iliyo juu yetu hupelekea kuharibika kwa maisha kama tulivyoona habari ya yule ndugu. Tumeona watu wengi wakiondoka katika nchi walizozaliwa na kwenda kuishi katika nchi zilizoendelea kwa lengo la kupata maisha mazuri, lakini uamuzi huo kwa kua haukuwiana na Uelekeo wa Mungu juu yao umepelekea kujutia maamuzi hayo kila kukicha na wakati mwingine kurudi makwao wanashindwa,na hata wakiweza wanahofia kwenda kuanza maisha upya, hii ni kwa kua jibu la matatizo ya mwanadamu haliko katika taifa aliloko bali liko katika MUNGU.
 

V.Mboya

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...