Friday, March 2, 2012

Send Off Party ya Martha Mwaipaja


Mwanamuziki wa injili Martha Mwaipaja akiwa na Mumewe mtarajiwa Mch John Said jana wakati send off party

Siku ya J/pili ya Tare 26/2/2012 ilikuwa Kitchen Party ya Muimbaji wa Muziki wa Injili Martha Mwaipaja iliyo fanyika Ukumbi wa Bwende ulioko Kiwalani jijini Dar es salaam.

Tare 1/3/2012 yaani jana ilikuwa Send off yake iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,na siku ya J/pili ya Tare 4/3/2012 itakuwa ni siku ya Ndoa katika kanisa la Ukonga Mombasa.

Marha Mwaipaja Mungu amempatia Mume ambae ni Mchungaji wa Kanisa la {Udhiirisho wa Injili} Pastor John Said.Kwa mujibu wa Pastor John amesema kuwa, Ndoa itafungwa katika kanisa la Ukonga Mombasa shughuli itafanyika Ukumbi wa Sinza Delux kuanzia Saa moja usiku na kuendelea.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...