Thursday, March 1, 2012

Groove Awards yaanza kupokea majina for Nomination


Logo ya Groove Awards kwa mwaka 2011
Zile tuzo maarufu za muziki wa injili nchini kenya maarufu kama GROOVE AWARDS Zimeanza mchakato wa kuwapata washindani(Nominees) wa kategori zipatazo thelathini na moja. Kwa mujibu wa waandaaji wa tuzo hizo wanamuziki watakaoingia kwenye ushindani huo ni lazima wawe wametoa kazi zao kuanzia January 1st 2011 mpaka  January 1st 2012.

Groove awards  ni tuzo za muziki wa Injili zinazosifika kwa maandalizi yenye ubora  kuliko tuzo nyingine zozote za injili Afrika mashariki na kati. Waandaaji wa tuzo hizo wiki moja kabla ya Tuzo kufanyika,huwakutanisha wanamuziki wanaowania tuzo hizo(nominees)na kufanya ziara mikoa mbalimbali nchini humo pamoja na kufanya matamasha ya wazi ya  muziki wa injili. Mwaka jana katika ziara hiyo Tanzania iliwakilishwa na Christina shusho pamoja na Rose Muhando.

Ili kupendekeza jina la mwanamuziki wa injili unapaswa kuingia kwenye tovuti ya www.grooveawards.co.ke na kufuata maelekezo ambapo kwa TANZANIA unapaswa kupendekeza jina la mwanamuziki bora nchini hapa.Kupendekeza ni rahisi kwa kuwa unapaswa kusubmit jina la mwanamuziki online.

Christina Shusho akiwa Nakuru nchini Kenya kwenye ziara ya Groove Awards mwaka jana

Tuzo zinazowaniwa ni pamoja na

1. Male artist of the Year 2.     Female Artist of the Year 3.     Group of the Year 4.     New Artist/ Group of the Year 5.     Song of the Year 6.     Worship of the Year 7.     Album of the Year 8.     Hip-hop Song of the Year 9.     Audio Producer of the Year 10. Video Producer of the Year 11. Song Writer of the Year 12. Video of the Year 13. Collabo of the Year 14. Dance Group of the Year 15. Ragga/Reggae Song of the Year 16

  Gospel Radio Show Of the Year 17. Gospel TV of the Year 18. Radio Presenter of the Year 19. DJ of the Year 20. Pwani song of the Year 21. Rift Valley song of the Year 22. Western song of the Year 23. Eastern song of the Year 24. Nyanza song of the Year 25. Central song of the Year 26. Artist of the Year (Uganda) 27. Artist of the Year (Rwanda) 28. Artist of the Year (Tanzania) 29. Artist of the Year (Burundi) 30. Artist of the year (Southern Sudan) 31. Artist of the year (Ethiopia).

Marion Shanko on Stage during GA Tour 2011

Kwa mwaka jana katika kategori ya Artist of the year from Tanzania ushindani ulikuwa kama ufuatavyo ambapo Christina shusho aliibuka mshindi.

ARTIST OF THE YEAR (TANZANIA)
26a. Bahati Bukuku
26b. Bonnie Mwaitege
26c. Christina Shusho
26d. Neema Mwaipopo
26e. Rose Muhando
26f. Upendo Nkone

Mch Piter Odanga akihubiri na kufanya Maombezi katika moja ya Ziara za Groove Awards mwaka jana

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...