Monday, March 19, 2012

Baada ya Rose Muhando na Anastazia Mukabwa, sasa ni Geraldine Oduor na Christina Shusho


Geraldine Oduor kushoto na Christina Shusho

 Geraldine Oduor ni mwanamama kutoka nchini Kenya ambaye kwa sasa amekamilisha album yake aliyoipa jina la NENO LAKO ambayo amemshirikisha world reknown gospel artist Christina Shusho kutoka Tanzania. Album hiyo ina jumla ya Nyimbo kumi ambazo nyingi kati ya hizo wameshirikiana na Christina shusho.Kwa upande wa Geraldine hii itakuwa ni album ya tatu kufanya toka aanze kumtumikia Mungu kama muimbaji wa kujitegemea.

Geraldine aliyezaliwa katika familia yenye msimamo mkali wa kikatoriki, mwaka 2010 wimbo wake wa “YESU KENDO” uliokuwa kwenye album yake ya pili aliyoipa jina la MUNGU WA BIBLIA, ilifanikiwa kushinda tuzo ya Nyimbo bora ya injili kutoka ukanda wa Nyanza nchini humo katika Tuzo zinazoheshimika sana nchini kenya ziitwazo Groove Awards. kwa Mwezi huu Groove Awards zimeanza nomination kabla ya kufanyika rasmi miezi kadhaa ijayo.

Kwa mujibu wa Oduor, Shusho na Oduor walikutana katika trip ya  umishieni walipokuwa wakihubiri injili kwenye maeneo ya vijijini(rural areas)kitu ambacho kiliwaweka pamoja.

Geraldine Oduor na Christina Shusho wakiimba pamoja kwenye umishieni
 Combination ya Shusho na Oduor inakuwa ni ya pili kufuatia kombination album iliyo-hit sana Afrika mashariki na kati kwa mwaka jana kati ya Legendary Rose Muhando kutoka Tanzania na  Anastazia Mukabwa kutoka kenya, album hiyo waliita “KIATU KIVUE”.Biblical hakuna kushindana kati ya kina Shusho na kina Anastazia Mukabwa japokuwa ni wazi kuwa wadau watakuwa makini kuona kama album ya Oduor na Shusho itamake headline as it was happened to ile ya kina Mukabwa.

Christina Shusho na Geraldine Oduor

Pamoja na hayo yote ukweli unabaki pale pale wote tunafanya tunavyofanya tukiwa kama watumishi kwa utukufu wa Mungu na sio kwa ajili ya status zetu.

Wewe Watosha - Geraldine Oduor

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...