Friday, March 2, 2012

Joshua Nasari Mtoto wa Mchungaji anayeiwakilisha Chadema Jimbo la Arumeru Mashariki

Joshua  Nasari
Tarehe 29/02/2012 Mkutano mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo(Chadema) katika wilaya ya Arumeru ulimteua Joshua  Nasari kuwania kiti cha Ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kilichochwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia chama cha Mapinduzi Marehemu Jeremiah Sumari. 

Joshua Nasari ni mtoto wa tano kati ya watoto nane wa Mchungaji Samuel Nasari,katika orodha ya watoto hao wa Mzee Samuel Nasari, watoto watano ni wa kiume na watatu ni wa kike huku Joshua akiwa ni mtoto wa pili wakiume katika Familia hiyo.Hii ni mara ya Pili kwa Joshua kuwania kiti hicho ambapo mwaka 2010 Nasari kupitia Chadema alikuwa mshindi wa pili katika uchaguzi huo.

Kiumri Joshua alizaliwa Mwaka 1985 na ni mhitimu wa Masomo ya Sayansi ya Jamii katika chuo kikuu cha Dar es salaam.Kuchaguliwa kwa Joshua Nasari ni changamoto kwa Familia za watumishi mbalimbali kuwa kuna mambo makubwa yanaweza kufanywa katika chi hii kupitia Familia za Makuhani.

1 comment:

  1. Nimefurahi kusikia hilo,mie nashuudiwa ushindi mkubwa sana juu ya mabadiliko ya kimaadili katika watu wa MUNGU wanaokesha kila siku BWANA kufanya jambo jipya Kwa TZ,maana Yoel 2.28 inatushudia kabisa katika zamani hizi watu kumrudia MUNGU Nuru imeingazia Taifa ili

    AHsante EL-shaddai

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...