Wednesday, March 7, 2012

Winnie Wambui(FOI) Wa Maximum Melodies Afariki


Winnie Wambui
Winnie Wambui maarufu kama FOI ambaye ni mmoja wa wanakundi la Injili la jijini Nairobi lijulikanalo kama Maximu Melodies amefariki Dunia Ijumaa iliyopita ya tarehe 02/03/2012.FOI alifariki kwa ajali alipokwa akienda kuhudhuria moja ya vikao vya kundi hilo na ndipo alipogongwa na lori katika moja ya mitaa ya nairobi.akiwa kundini humo foi alikuwa lead vocalist wa Maximum melodies na mhasibu wa kundi hilo.

Winnie Wambui alifikwa na mauti hayo siku chache baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kufikisha umri wa miaka 27,Winnie alizaliwa tarehe 20 Feb 1985.Mazishi yatafanyika ijumaa hii tarehe 9/03/2012 na tayari tovuti inayokwenda kwa jina la  www.winniewambui.com imezinduliwa kwa ajili ya kumuenzi marehemu Winnie Wambui.

Kundi zima la Maximum Melodies kutokaNairobi Kenya,Winnie Wambui ni wa katikati katika mstari wa chini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...