Thursday, May 19, 2011

MUNGU NA MALI -Mwl C. Mwakasege


Mwl C. Mwakasege
     Kuna uhusiano gaini kati ya Mungu na mali?
     Kuna uhusiano gaini kati ya mkristo na mali?
     Kuna uhusiano gaini kati ya wokovu na mali?
     Je, nidhambi kwa mkristo kuwa na mali nyingi?

Hebu na tuangalie maneno ya yesu kristo juu ya Mungu na mali.
      “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana hatamchukia huyu, Na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwenzi Kumtumikia Mungu na mali’’ (mathayo 6:24)

Neno la kingereza lililotafasiliwana kuandikwa ‘MALI’ ni ‘MAMMON’  na  hili ‘mammon’ ni jina la roho ya bilisi anayotawala mali. Kwa maneno mengine naweza kusema kuwa ‘mammon’ ni jina la pepo.

Kwahiyo, neon ‘mali’ neon mali lilivyotumika hapa linamaanisha ‘pepo linaloitwa pepo mali’ ndiyo maana yesu kristo alisema “hakuna mtu awezaye kutumikia MABWANA wawili…” Yesu kristo asingeliita mali kuwa nimojawapo ya MABWANA kama hakuwa juu ya roho inayo itwa mali. Roho hii ya shetani  iitwayo mali imefanya watu wengi, hata wakristo waache kumtumikia Mungu aliye hai, na badalayake waitumikie roho inayowasukuma na kuwatamanisha juu ya mali, ili waitumie kwa uchoyo na ubinafsi.

     Wakristo wngine wanadhani wanaweza  kumtumikia Mungu na vile vile kummtumiakia mali. Yesu kristo alisema; “HAKUNA mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana ATAMCHUKIA HUYU, NA KUMPENDA HUYU; AMA ATASHIKAMANA NA HUYU, NA KUMDHARAU HUYU. Hamwenzi kumtumikia Mungu na mali.”

Kwakusema hivi akuwa anamaanisha kuwa na vitu vinavyo itwa mali si vibaya. Kitu anachosema ni kibaya ni KUITUMIKIA MALI! Bibilia inasema katika Zaburi 24:1 kuwa, “Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana; Dunia na wote wakaao ndani yake .”

Mtu hakuumbwa ili aitumikie mali. Mtu aliumbwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu na amtumikie yeye peke yake. Mali ya dunia iliwekwa kwa ajili ya kumtukia mtu, na siyo mtu aitumikie mali! Mtu aliwekwa juu ya mali yote na aliingizwa kuitawala (Mwanzo 1:28 – 30).

Kuwa na mali siyo vibaya, wala siyo dhambi. Mali inakuwa kikwazo katika maisha ya mkristo inapoaza kumfanya mtu amsahau Mungu na mapenzi yake. Ndiyo maana Yesu kristo alisema “ kwa shida gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu” (Luka 18:24) siyo kwamba huwezi kuingia ufalme wa Mungu. Bali kwa shida wenye mali watauingia ufalme wa mungu. Kwa maneno mengine ni kwamba wakimtanguliza na kumtumikia Mungu, mali haita kuwa kwazo katika maisha yao ya ukristo.


 Sasa tuishije katika ushauri wa namna hii?

“Kwa namna hiyo nawaambieni, msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, yakwamba hawa pandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? NI YUPI KWENU AMBAYE AKIJISUMBUA AWEZA KUJIONGEZA KIMO CHAKE MKONO MMOJA? Namavazi ya nini kuyasumbukia? fikirini maua ya shambani jinsi yameavyo, hayafanyi kazi wala hayasokoti, nami nawaambieni hata sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo yahayo, basi ikiwa mungu huyauvika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa karibuni, JE!HATAZIDISANA KUWAVIKA NINYI, ENYI WA IMANI HABA?. Msisumbuke basi, mkisema, tule nini? au tunywe nini? au tuvae nini? Kwa maana haya yote mataifa huyatafuta,  kwa sababu baba yenu wa mbinguni anajua mnahitaji hayo yote.{matayo 6;25-32}

Kuna wakristo wengi wameyaelewa vibaya maneno ya Bwana YESU kristo hata kufikia kutokufanya kazi kwa kisingizio cha kwamba Yesu kristo alisema tusiyasumbukie maisha. Kwao kufanya kazi ina maana kusumbukia maisha. Lakini napenda kuwaambia yakua Yesu kristo hakua namaana yakutuambia tusifannye kazi aliposema tusiyasumbukie maisha.

Nadhani unaamini kuwa ni Roho wa kristo aliyemuongoza mtume PAULO kuwaandikia wathesolenike juu yamashauri mbalimbali ya kikristo katika1Wathesolenike3;10b anasema,”ikiwa mtu hataki kufanya kazi,basi,asile chakula’  Nimuhimu kufanya kazi. Kufanya kazi sio kusumbuka na maisha na Kusumbuka na maisha sio kufanya kazi.

Jambo ambalo Bwana Yesu alitaka tufahamu wakati alipokua akisema tusiyasumbukie maisha nikwamba katika kila jambo tumshirikishe Mungu na kumtanguliza yeye. Wakiristo wengi wanadhani wanaweza kula, kunywa na kuvaa bila msaada wa Mungu.Yesu kristo alisema katika Yohana15:5b kuwa; ‘…..maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote’’{HILI NIPAMOJA NA KULA NA KUVAA} ndio maana katika wakilipi4:13 imeandikwa kuwa”nayaweza mambo yote katika YEYE anitiaye nguvu” Yesu kristo ndiye atutiate nguvu.
Yesu kristo alitoa muongozo mzuri sana wa jinsi ya kuishi hapa ulimwenguni alisema;
Bali utafuteni KWANZA ufalme wake,na haki yake,na hayo yote mtazidishiwa”{mathayo 6;33}
Ukiyaangalia maisha ya watu wengi utadhani Yesu kristo alisema”bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake, na hayo yote MTAONDOLEWA” Inahuzunisha kuona watu wengi wakiokoka maisha yao yanageuka kuwa duni, wanashindwa kula vizuri wala kuvaa vizuri.

Ngoja nirudie kusema SI MAPENZI YA MUNGU UWE MASIKINI. SI MAPENZI YA MUNGU TUKOSE CHAKULA WALA MAVAZI. Ni Mungu yupi ambaye atawapenda ndege akiawavika na kuwalisha, nakuacha watoto wake aliowaumba kwa mfano wake wakose chakula na mavazi?. MUNGU wetu tunayemuabudu na kumtumikia katika kristo Yesu,anapenda tuishi maisha mazuri, tule na kuvaa vizuri.Tunachotakiwa kufanya nikuutafuta kwanza ufalume wake,na haki yake, na hayo yoye{chakula na mavazi}TUTAZIDISHIWA na sio TUTAONDOLEWA.

Ukiona mtu anasema ameokoka halafu anajikuta amekosa chakula na mavazi, huku anafanya kazi,basi ujue anafanya kazi na kukusanya vitu hivyo pasipo Bwana kwa kuwa asiye kusanya pamoja na Bwana hutapanya.

Source: Mwl C. Mwakasege


5 comments:

  1. Nimependa mafundisho haya,na nashukuru nimebarikiwa kwayo.asante

    ReplyDelete
  2. nimebarikiwa saaaaaaaaaaaaaana

    ReplyDelete
  3. Ubarkiwe mtumish wa Mungu

    ReplyDelete
  4. Asante sana Mtumishi wa Mungu aliye Juu

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...