Saturday, May 21, 2011

AFRICA GOSPEL MUSIC AWARDS 2011

Africa Gospel Music Awards (AGMA) ni tuzo kubwa kabisa zinaaowahusisha wanamuziki wa muziki wa injili kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika. Tuzo hizi ambazo zinafanyika mara ya pili zina lengo la kutambua na kuthamini kazi za wanamuziki wa injili barani Afrika.Kwa mwaka huu wa 2011 tuzo hizo zinahusisha jumla ya kategori ishirini (20), ambapo upendekezaji wa wagombea katika kategori tofauti ulifanyika kuanzia tarehe 15th April 2011 mpaka tarehe 13th May 2011.Upigaji kura ulianza rasmi jana tarehe 20 May na utafungwa tarehe 24 June 2011.Tuzo za AGMA mwaka huu zimepangwa kufanyika jijini London Uingereza Tarehe 9th July 2011.

Daddy Owen mwanamuziki kutoka kenya ambaye anaongoza kutokea kwenye kategori nyingi

Wanamuziki wa Kenya wan`gara

Baada ya mikiki mikiki ya kutafuta contestants kwenye kategori mbalimbali, kwa upande wa Afrika mashariki wanamuziki wa injili toka nchini Kenya wameibuka kidedea kwa kuchomoza kwenye kategori takribani nane. Wakati Christina shusho ndiye mtanzania pekee aliyeibuka kama Nominee, Shusho yumo kwenye kategori ya Mwanamuziki Bora wa Injili afrika mashariki. Nchi nyingine za Rwanda na Uganda nazo zimefanikiwa kupenyeza wanamuziki katika kuwania tuzo hizo.

 Hosanna Inc imekuwa ikizifuatilia Tuzo hizi za Afrika tangu kwenye mchakato wa kupendekeza washiriki watakaowania tuzo hizo. Wingi wa wakenya kwenye Tuzo hizo sio kwamba wanafanya Vizuri kuliko wa-tanzania, siri kubwa hapa ni INFORMATION, kwa kuwa masharti ya kushiriki ni ya kawaida.Wengi wa wanamuziki wa tanzania hawazijui Tuzo hizi na hata wadau mbalimbali pia hawana taarifa juu ya uwepo wa Tuzo hizi na namna ya kushiriki. Ila ni matumaini yetu kuwa mwakani mambo yatabadirika na kuwashirikisha watanzania wengi zaidi.

Zifuatazo ni baadhi ya Tuzo na washiriki wanaowania Tuzo Hizo
Best Gospel Album
AGMA Special Award
Event of the Year
Lifetime Achievment Award
Best Male Artiste
Regional Awards Category
Best Female Artiste
Best Artiste/( USA)
Best Gospel Group
Best Artiste (East Africa)
Best Gospel TV Programme
Best Artiste (North Africa)
Best Gospel Radio Programe
Best Artiste (West Africa)
Best Gospel DJ/Presenter
Best Artiste(S.Africa)
Discovery of the Year
Best Artiste/s (Europe)
Best Contribution to Africa Gospel Music

Best Music Video
  • KWASA - GBOOF
  • MERCY- KWESI OTENG
  • CHARLES GRANVILLE - BY MY SIDE
  • REBECCA - I NEED YOU MORE
  • AGIDIGBA VIDEO BY TIM GODFREY AND THE X’TREME
  • SALUTI - DADDY OWEN
  • THE PRESENCE –JOE PRAIZE
Best Gospel Album
  • BOHYE - NO TRIBE. GHANA
  • TIMELESS ONE - ALEXANDER VICTOR. UK
  • SYSTEM YA KAPUNGALA - DADDY OWEN. KENYA
  • REBECCA MALOPE – UKUTHULA. SOUTH AFRICA
  • HYMNZ UNLIMITED - NII OKAI. GHANA
  • AWESOME GOD-AARON T. AARON-UK
  • PULPIT KWA STREET-JULIANI-KENYA
  • RACING UP – PAUL MWAI-KENYA
  • WORSHIP IN HIS PRESENCE WITH BENJAMIN DUBE – SOUTH AFRICA
Event of the Year
  • EVOLUTION 6 BY IMPACT PROJECT MINISTRIES. ACCRA. GHANA
  • AFRICA WORSHIPS WITH SONNIE BADU. LONDON. UK
  • HARVEST PRAISE 2011 WITH REV BENJAMIN DUBE, ACCRA, GHANA
  • THE BIG CHURCH DAY OUT. UK
  • GROOVE AWARDS. KENYA
  • TRUE WORSHIPPERS "A NIGHT IN HIS PRESENCE" VIRGINIA,USA
  • LAGOS EXPERIENCE. LAGOS, NIGERIA.
Overall Best Male Artiste

Uche Agu mtunzi wa Double double yumo kwenye wanaowania wanamuziki bora wa kiume barani Afrika
Best Male Artiste
  • DADDY OWEN- KENYA
  • SONNIE BADU - UK
  • BENJAMIN DUBE-SOUTH AFRICA
  • JOE PRAIZE- NIGERIA
  • UCHE AGU –SOUTH AFRICA
  • CHARLES GRANVILLE-NIGERIA
  • EBEN-NIGERIA
  • FABRICE NZEYIMANA-BURUNDI
  • AARON T. AARON-UK
  • KABELO ERIC -BOTSWANA
Overall Best Female Artiste
  • DIANA HAMILTON-UK
  • OHEMAA MERCY-GHANA
  • LARA GEORGE-NIGERIA
  • SINACH- NIGERIA
  • EMMY KOSGEI-KENYA
  • REBECCA -UK
  • TOYIN MOTARA-NIGERIA
  • CECILIA MARFO-GHANA
  • WINNIE MASHABA- SOUTH AFRICA
  • KEFEE BRANAMA- NIGERIA
Best Gospel Group
  • OBERT MAZIVISA & TRUMPET ECHOES. UK
  • ROYAL PRIESTHOOD. GHANA
  • TRIBE OF JUDAH CHOIR. USA
  • NO TRIBE. GHANA
  • TIM GODFREY AND XTREME. NIGERIA
  • ALLEN AND DA NEW WAVE. UK
  • JOYOUS CELEBRATION. SOUTH AFRICA
  • DAVISON BAND. UK
  • K-STONEZ . NIGERIA
Best Artiste (East Africa)
Christina Shusho ndio mwanamuziki pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye Tuzo za Afrika
Best Artiste (East Africa)
  • FABRICE NZEYIMANA
  • ALICE KAMANDE
  • EXODUS-UGANDA
  • CHRISTINA SHUSHO TANZANIA
  • BLESSED SISTERS RWANDA
  • GEN. MANASSEH MATHIANG SOUTHERN SUDAN
  • JOY NKUNDIMANA BURUNDI
  • JULIANI
  • EMMY KOSGEI
  • MOSES "QQU" ODHIAMBO
  • DADDY OWEN

1 comment:

  1. AFRICA GOSPEL MUSIC AWARDS 2011 ni matapeli kwa jinsi walivyoshindwa kusubiri tarehe walizowatangazia watu kupiga kura zao; badala yake walifunga upigaji kura mapema na hivyo kuwazuia wapenzi wengi wa muziki wa injili kutumia fursa yao ya kuwapigia kura waimbaji wanaowapenda. Kama wakristo wanatakiwa wasiwe waongo bali wasimame kwenye tarehe walizotaja wenyewe awali. Pia majina yaliyopendekezwa hayawakilishi kihalali Africa badala yake ni chaguzi zisizoiwakilisha Africa kwa uhalisi wake. Ni matumaini yangu kuwa AFRICA GOSPEL MUSIC AWARDS 2011 watasikiliza maoni ya watu na kurudisha uhalisi wa Muziki wa injili hata katika tuzo na wanaotuzwa.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...