Dr Barnabas Mtokambali |
Kanisa la Tanzania Asemblies of GOD(TAG) liko mbioni kuanzisha chuo cha Muziki katika mpango wake wa kuimarisha huduma za Kanisa, hususani katika kusifu na kuabudu.Katika salamu alizotoa katika ibada maalumu iliyofanyika siku za hivi karibuni katika Kanisa la TAG Ubungo jijini Dar es salaam,Askofu mkuu wa TAG Tanzania Dr Barnabas Mtokambali alisema “muziki tulionao makanisani kwetu ni wa kubabia babia,hauko kwenye viwango vya kimataifa, ni muhimu kuwa na muziki wenye radha za Noteni katika kutumia ala za muziki na kuimba”.
Aliongeza kuwa “kabla ya kuanzisha chuo hicho tutapeleka watu ili wapate utaalamu wa kutosha ili waje kufundisha watu wengine watakaokuwa wakifundisha muziki makanisani” Dr Mtokambali alisema kuwa kwa sasa anamkakati wa kujenga chuo kingine cha Biblia jijini Mwanza baada ya kupatikana ekari zipatazo Tano na hivyo kutoa nafasi ya chuo cha sasa kuwa chuo cha Muziki jambo litakalochukua Miaka mitano hadi kumi.
Katika kufafanua hilo Dr Mtokambali alisema kutokana na mchakato huo itawalazimu waalimu wa Muziki makanisani kusoma Muziki kwa kina kabla ya kufikia hatua ya kufundisha ili hatimaye waweze kufikia hatua ya ngazi ya cheti,Stashahada na Shahada.Chuo hicho pia kitatumika kuwandaa waalimu wa watoto ili kuwa na huduma hiyo kila kanisa kikamilifu.
No comments:
Post a Comment