Thursday, March 8, 2012

Flora Mbasha Kuhudumu nchini MarekaniFlora Mbasha Mumewe pamoja na Madancers wa kundi hilo
Mtumishi wa Mungu na mmiliki wa studio ya Flem Records iliyoko Tabata jijini Dar es salaam Flora Mbasha na Mumewe Emmanuel Mbasha, wanatarajia kwenda nchini Marekani kwa ajili ya Huduma.Katika taarifa hiyo aliyoitoa ikiwa haijaeleza ataondoka Lini,atahudumu wapi ila akasema kuwa mengi ataendelea kuyatoa.

Flora mbasha kupitia  Wall yake ya Facebook amesema
“Bwana Yesu asifiwe rafiki zangu, ninapenda kuwaaga, tunasafiri kwenda Nchini Marekani tutakuwa na ziara huko. tunahitaji maombi yenu sana, tutakuwa tukiwajulisha kila kinachoendelea huko. tunawapenda sana. mbarikiwe. Enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe, aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa”
Wakati Flora Mbasha na mumewe wakijipanga kwenda Marekani, tarehe 29 Feb 2012 Mtumishi wa Mungu Josephat Mwingira pamoja na Praise team yake walienda nchini Nigeria na kuhudumu katika kanisa la Mtumishi wa Mungu Pastor Simion Oka ambaye ni mmoja kati ya watumishi wa mungu wakubwa nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...