Friday, March 9, 2012

Tina wa Mary Mary Atarajia Kupata Mtoto


Tina Campbell  akiwa na Mumewe aitwaye Teddy
Tina Campbell ni mmoja kati ya duo sisters wanaounda kundi la Mary Mary ambalo ni Mashuhuri sana duniani kwa uimbaji wa nyimbo za injili,miezi kadhaa ijayo Tina pamoja na mumewe wanatarajia kupata mtoto wao wa tano. Kauli hiyo ya Tina aliitoa wakati akifanya Mahojiano na Jarida la Essence yaliyofanyika hivi karibuni nchini Marekani.

Wakati Tina akiyasema hayo, dada yake Erica wanayeunda wote kundi hilo la Mary Mary ametoka kujifungua wiki kadhaa zilizopita na Mungu amemjalia yeye na mumewe mtoto wa Kike.Tina alizidi kusema kuwa “Hawakutegemea kupata mtoto mwingine kwa kuwa mtoto wao wa nne waliamini kuwa ndiyo mtoto wa Mwisho lakini Mungu amezidi kuwabariki.Akaendelea kusema “We thought our home was exciting and busy now -- it's about to be even more exciting and busy. We are looking forward to it."

Ndugu wawili Tina Campbell kushoto na Erica Campbell kulia ambao kwa pamoja wanaunda kundi la Mary Mary

Pamoja na hayo yote Mary Mary kwa sasa wako busy wakiandaa Tv Show ya kwao ambayo itakuwa ikionekana kwenye  WEtv kuanzia Mwezi March 29 mwaka huu wa 2012. Kwa kile kinachoonekana kuzidi kupendwa kwa kundi hilo Mary Mary wameingia kwenye mchuano wa kuwania Tuzo Mashuhuri za Gospel duniani ziitwazo Dove Awards.

katika Tuzo hizo Mary Mary wako kwenye kipengele cha “The Best Urban Album of the year” kupitia Album yao ya Something Big walioitoa mwaka jana. Mwezi wa tano mwaka huu wa 2012 Mary Mary wanatarajia kuzindua album yao mpya itakayoitwa Go Get ItNo comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...