Tuesday, February 28, 2012

Brazili yawa nchi ya pili Duniani kwa kutoa idadi ya wamishinari wengi kwenda miisho ya dunia


Mnara mkubwa kabisa wa YESU duniani ulioko katika jiji la Rio De Jeneiro nchini Brazili
Nchi ya Brazili imekuwa ni nchi ya pili duniani kwa kutoa idadi kubwa ya wamishionari wanaokwenda sehemu mbalimbali duniani kwa lengo la kumtangaza Kristo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya kimarekani ijulikanayo kama Global Christianity study Organisation, Brazili ilitoa jumla ya wamishionari wapatao 34,000 kati ya jumla ya wamishionari 400,000 waliotumwana mataifa yote duniani kwa mwaka 2010.

Katika utafiti huo wakati Brazilli ikichukua nafasi ya pili, Marekani yenyewe ndio inaongoza kwa kutoa jumla ya wamishionari 127,000.Pamoja na Marekani kuongoza,Marekani pia imekuwa nchi ya kwanza katika kupokea idadi kubwa ya wamishionari kutoka mataifa mengine wanaoingia nchini humo kwa ajili ya kumtangaza Kristo Yesu.

Kwa mwaka 2010 Marekani ilipokea jumla ya wamishionari wapatao 32,400 na wengi wao wakitokea nchini Brazili.Kwa sasa Brazili ni nchi ya pilli duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya wakristo wa madhehebu ya Kiprotestant.

Kwa sasa idadi ya wamishionari wa kujitolea imeongezeka kwa kasi dunuani hususani baada ya kuongezeka kwa teknolojia ya Mawasiliano ya uma(Teknohama), ambapo mtu anaweza kukaa nyumbani kwake na kuhubiri au kuhubiriwa kwa njia ya Internet. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...