Wednesday, February 1, 2012

Sir Andy Chande Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons 2

Sir Andy Chande
*Nimepata kutambua umuhimu wa mafunzo ya Freemason katika kujenga hisia za utuwema na ukweli kwake mtu wenyewe na kw abinadamu wenzake. Moyo wangu mawazo yangu na roho yangu, vyote vimeimarika kutokana na kushiriki kwangu katika Freemason

*Mwaka 1972 nikachukua hatua yangu ya kwanza kuelekea kwenye madaraka makubwa zaidi katika Freemason nilipochaguliwa Afrisa Mkuu wa Wilaya wa kufanya kazi na Makao makuu ya Freemason ya Mkoa kule Nairobi ambao wakati ule ulikuwa unasimamia makambi kiasi cha ishirini na manane katika Afrika nzima

*Freemason Tanzania wamesaidia kituo cha watu wenye ukoma cha kindiwi wilayani Utete; Kituo cha watoto cha Mama Theresa; shule  ya Vipofu ya Pongwe, mkoani Tanga; Kituo cha yatima cha Arusha, Hospitali ya Mnazi mmoja kula Zanzibar; na Shule ya Viziwi ya Buguruni.


Tangu miaka hiyo ya 1920 idadi ya  vikundi vya Mason nchini Tanzania na  Afrika Mashariki kwa ujumla imeendelea kuongezeka. Ogezeko  kama hilo hilo limejidhihirisha katika Asia, Marekani ya  kusini, na baadaye Ulaya ya Mashariki, baada ya kipindi kile cha kuingia kwa ukomanisti lakini kwingine kote hasa Ulaya ya Magharibi, Amerika ya  Kusini na Australia, idadi ya Wanachama wa Mason wamekuwa wakipungua polepole na kuacha pengo kubwa duniani kutoka milioni saba waliokuweko wakati wa vita kuu ya kwanza hadi kufikia milioni tano tu.

Hata hivyo mchango wanaodai kuutoa ndugu hao millioni tano, kwa Chama chao na kwa Jamii, ni mkubwa sana. Wanatoa misaada kila mwaka, kulingana na kazi zinazotekelezwa na vikundi vyao, kiasi cha dola milioni 400 za Marekani. Huku Tanganyika, baadaye Tanzania, walisaidia kituo cha watu wenye ukoma cha kindiwi wilayani Utete; Kituo cha watoto cha Mama Theresa; shule  ya Vipofu ya Pongwe, mkoani Tanga; Kituo cha yatima cha Arusha, Hospitali ya Mnazi mmoja kula Zanzibar; na Shule ya Viziwi ya Buguruni, ni machache tu kati ya miradi mingi iliyogharimiwa na vikundi vya Mason.

Kati ya miradi hiyo yote, ule wa Shule ya Buguruni ndio ninaouthamini sana moyoni mwangu; maana mimi ndiye mwandishi na mchangishaji mkuu wa fedha; mhamasishaji na mtetezi mbele ya Viongozi Wakuu kwa niaba ya shule hiyo kwa muda wa miaka thelathini iliyopita lakini bado pamoja na shughuli zote hizo za maana, kwa muda wote huo niliokuwa Mwanachama wa Freemason mara nyingi wale Wanachama wa Zamani wamenyanyaswa sana na magazeti ya  nchi za Magharibi.

Kutoka kuonekana kuwa Chama ambacho huruma na dhamiri zake katika kumwinua binadamu zinathaminiwa, kama ilivyokuwa katika kipindi kirefu cha karne za kumi na nane na kumi na tisa na mwanzo wa karne ya ishirini, sasa kimeporomoshwa hadhi kw amashambulizi makali ya magazeti yasiyokuw ana msaada, kiasi cha kuigeuza Freemason kuwa kama kivuli tu, kikundi cha wafitini cha ajabuajabu waliojaa hila!

Sir Andy Chande kulia akiwa na Rais Benjamin Mkapa
Ili kuanza kukielewa vizuri zaidi Chama hiki, na hivyo pengine kuanza kuoanisha dhana na hali halisi, lazima mtu arudi kwenye misingi Freemason itikadi yenyewe ya Wema na maadili ndiyo ilivyonitumbukiza katika mazungumzo yangu ya kwanza mwanzoni mwa miaka ya 1950 na akina Campbell Ritchie na Maclean, juu ya huruma kwa binadamu. Wakati ule ndipo nilipoanza kutambua kuwa, kumbe, maana kamili ya Uanachama wa Freemason ni Sayansi ya Maisha ambayo lengo lake ni kumtia moyo mwanadamu kwa  kumwelekeza vile anavyotarajiwa kuwa mtu mwenye ukamilifu katika vyote.

Sehemu kubwa ya hoja hiyo ya Ukamilifu wa mtu inafichwa katika dhana, na       pengine ndiyo maelezo ya uvumi unaoelekezwa kwenye shughuli za Freemason. Lakini taratibu hizo zimejengwa kwa malengo ya makusudi, ambayo mimi nayaona kuwa mazuri tu, ya kuamua na kuboresha fikra, moyo na hadhi ya binadamu kwa hiyo katika hatua ya kwanza ya kuingizwa kwenye Freemason, mising mkuu ya maadili ya kusema kweli inayojenga Freemason inasisitizwa kiasi cha kutosha katika mawazo ya mtu anayetaka kujiunga na Chama au mtahiniwa.

Hatua ya pili ya Freemason inasisitiza kuendelezwa kwa vipaji na ufundi katika sanaa na sayansi ili mtu aweze kuwa na manufaa makubwa kadiri inavyowezekana katika maisha. Hatua ya tatu inatoa nafasi kwa mtu kufikiria saa chache za mwisho wa maisha yake, lau kama hili litaonekana kuwa kama ndoto kwa njia hivyo, huyo anayetaka kujiunga na Freemason anaelekezwa namna ya kuishi kwa kutumia nafasi zote kabisa zilizopo katika namna inavyooana na misingi mitatu ya Freemason, ambayo ni: Upendo wa kindugu, misaada na ukweli, na kwamba kifo ni lazima.

Misingi ni mitatu ikisha kufafanuliwa katika malekezo ya wakufunzi yanayositiri mengi kati ya matunda ya Freemason, ndiyo ilivyovutia zaidi nilipopata kujua kwa ndani, kwa mara ya kwanza, baadhi ya mambo katika kikosi cha Antient. Katika taratibu za Freemason, mzingi wa upendo wa kindugu unawaelekeza ndugu zetu wote kuwatambua  binadamu wote kuwa familia moja iliyoumbwa na huyo Mwenyezi, lakini wakati huo “msaada” unatoa ujumbe kuelekeza imani niliyofunzwa na baba yangu, yaani kuwasaidia  wenye shida iwe katika kuwapunguzia umasikini, au kuwaliwaza wanaosumbuliwa na matatizo. Huo ni wajibu wetu sisi sote.

“Ukweli”, msingi wa tatu nap engine, ndio muhimu kuliko yote ni dhana takatifu ambayo, kwa mwanachama wa Freemason, ndio msingi wa kila jema la binadamu “kuwa mtu mwema na kweli” ni somo linalotolewa mapema kwa kila mtu anayetaka kuingia katika Freemason; hivyo ni kauli inayotumiwa kila mahali kama zana ya kurekebisha na, kama ikibidi kuelekeza njia ya maisha na vitendo vya mtu kulingana na masharti yale manne muhimu ya Freemason: kiasi, uvumilivu, busara na haki.

Na misingi yote hii, na maadili na umuhimu unaojumuisha siyo tu mafunzo ya falsafa za watu wa kale, kuanzia wagiriki, paka Budha, mpaka Zaroster. Lakini hata za dini zinazojulikana. Kinyume na propaganda zinazoenezwa za Mafashisti wa kiitaliano na wengine wengi zaidi ya  hao, Freemason si chombo cha dini wala vile vile, kinyume chake, hakipingi dini; kwa kweli Freemason wanawakaribisha watu wote bila kujali imani zao za dini, wala hawafanyi mbinu za kubadili imani zao wala kuelekeza ibada zao; wanachojaribu tu ni kuwafanya binadamu bora zaidi.

Sir Andy Chande akiwa na wenzake wakipanda Miti jijini Tanga kama moja ya shughuli zao za kijamii
Hivyo hiyo ndiyo dunia niliyoitumbukia mwaka 1954, na ikawa sehemu muhimu ya maisha yangu kuanzia hapo. Katika kipindi hicho nimepata bahati ya kushuhudia kujitolea kwa Wanachama wa Freemason katika kuwasaidia wenye shida ndani ya Afrika Mashariki na hata nje ya hapo. Nimepata kutambua umuhimu wa mafunzo ya Freemason katika kujenga hisia za utuwema na ukweli kwake mtu wenyewe na kw abinadamu wenzake. Moyo wangu mawazo yangu na roho yangu, vyote vimeimarika kutokana na kushiriki kwangu katika Freemason; na kuimarika huko kunatofautiana kabisa na hisia zinazotangazwa katika magazeti mashuhuri ya nchi za magaribi. Kuwasaidia wenzetu kuwasaidia wengine ndiyo misingi niliyojifunza katika miaka yangu mingi ndani ya Freemason.

Baada ya kushika nafasi za juu zaidi katika kambi hii ya Nyota ya Jaha mnamo miaka ya mwisho wa 1950 na 1960 nikateuliwa kuwa kiongozi mstahiki mwaka 1967, wakati huo ndio kwanza nimeteuliwa Rais wa Muungano wa vyama vya Round Table vya Afrika  Mashariki. Mwaka uliofuata, kwa vile nilivyokuwa Mwanachama wa kwanza wa Round Table asiyekuwa Mzungu, nikawa raisi wa kwanza wa Roundi Table na vyama vinavyoambatana nayo duniani mwenye asili isiyokuwa ya kizungu: ukweli ulioinua hadhi ya nafasi hii kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko ilivyokuwa  kawaida.

Kwa nafasi hiyo nikalazimika kusafiri sana, kuandamwa na Magazeti, na kuwa na shughuli nyingi za uwakilishaji kimataifa, mwaka 1970 nikakamilisha kipindi changu cha uongozi kama rais wa Kimataifa wa Baraza la Dunia la Klabu ya Huduma za Vijana; na mwaka uliofuata, baada ya kulazimika kustaafu kutoka katika chombo hicho kwa sababu ya umri, nikiwa makamu wa kudumu (wa heshima) wa Mwenyekiti wa Muungano wa Round Table katika Afrika Mashariki mwaka 1970 nikajiunga na Round Table ya Dar es salaam, hatua ya kwanza kuelekea kwenye nafasi ya Gavana aliyewajibika na klabu sabini na nane katika sehemu kubwa ya Afrika.

Mwaka 1972 nikachukua hatua yangu ya kwanza kuelekea kwenye madaraka makubwa zaidi katika Freemason nilipochaguliwa Afrisa Mkuu wa Wilaya wa kufanya kazi na Makao makuu ya Freemason ya Mkoa kule Nairobi ambao wakati ule ulikuwa unasimamia makambi kiasi cha ishirini na manane katika Afrika nzima.

Kila nilivyopata madaraka makubwa zaidi, ndivyo nilvyohakikisha kwamba nilifanya kila lililowezekana kutakasa Freemason mbele ya Umma. Kwa uzoefu wangu mimi, watu kwa kawaida hutilia mashaka, na hata kuogopa, mambo wasiyoyaelewa. Kwa hiyo wakati wote nilipoulizwa habari za Freemason nikajitahidi kumweleza huyo muulizaji misingi ya chombo hicyo, nikisisitiza kwamba hakikuwa chama cha siri, na wanachama wake wanajulikana wazi: na kwamba mikutano yake haifanyiki katika sehemu za kujificha ila katika kumbi za mikutano zinazojulikana, zenye hati ya serikali na zinazoweza kutambulika wazi wazi.

Kama nilivyokwisha kusema mapema chama hiki na maajabu yake, kiliingia wakati wa Vita Vikuu vya pili, tulipokuwa tunajaribu kuwalinda wanachama wetu waliokuwa Italia, ufaransa na Ujerumani dhidi ya vituko vya mataifa makubwa toka wakati huo tumejidhihirisha wazi wazi mbele ya umma, na kujitahidi wakati wote kuwaondolea mashaka na kudhihirisha kuwa chama chetu ni chombo kinachomwingiza mtu mwema na kujitahidi kumfanya mwema zaidi.Habari yote hii ni kwa Mujibu wa kitabu cha Sir Andy Chande

Source:Jibu la Maisha Jamii Forum

1 comment:

  1. Historia ya freemason kwa maoni yangunaona mnaitoa kwa ufupi sana. Hata hivyo naona ni vyema mkaielezea kwa mapana na mahusiano yake na nchi yetu Tanzania. Kila mtu atajwe kwa namna anavyohusika. www.findtruefaith.blogspot.com

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...