Tuesday, October 23, 2012

Papa Atangaza Watakatifu Wapya Saba


Baba Mtakatifu Papa Benedikto XV1

Baba Mtakatifu Benedikto XV1, Jumapili iliyopita ambayo ilikuwa ni Jumapili ya Misioni Duniani, aliongoza Ibada ya Misa , ambamo pia aliwatagaza watumishi wa Mungu saba kuwa Watakatifu. Nao ni Giacomo Berthieu, Pietro Calungsod, Giovanni Battista Piamarta, Maria del Monte Carmelo (Maria Carmela Sallés y Barangueras), Maria Anna Cope (Barbara Cope), Caterina Tekakwitha na Anna Schäffer.

Katika homilia yake, Baba Mtakatifu, alionyesha kufurahia kwamba, kweli ilikuwa ni siku ya furaha kutokana na matukio mawili kwenda sambaba , Mkutano wa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Uinjilishaji mpya na Jumapili ya Misioni Duniani. Alisema, hata Neno la Mungu lililosomwa pia liliangazia matukio yote mawili, likionyessha jinsi wainjilishaji walioitwa kushuhudia na kutangaza Ujumbe wa Kristu , wao wenyewe pia wanavyotakiwa kuichukua sura ya Kristu na kuifuata njia yake. Hili ni kweli katika vyote Utume kwa mataifa na Uinjilishaji mpya. Papa alieleza hayo akitazamisha katika maisha ya waliotangazwa Watakatifu.

Na Kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, Papa alielekeza mawazo yake katika Madhabahu ya Lourdes, ambako mahujaji walilazimika kukatisha hija kutokana na mafuriko ya maji kutoka mto Gave, baada ya mvua kubwa kunyesha.

Papa aliwataka waamini wote watolee sala zao kwa Mama Bikira Maria kumwomba awalinde wamisionari wote, mapadre, watawa na walei ili kila kona ya dunia ipande mbegu nzuri ya Injili. Na pia wasali kwa ajili ya Sinodi ya Maaskofu , hasa wakati huu wanapoendelea kuchambua changamoto zinazokabili Uinjilishaji mpya unao lenga kuenezaji kw kishindo zaidi imani ya Kikristu.

Na mwisho ,kama kawaida, Papa alisalimia katika lugha mbalimbali na kutoa baraka zake kwa wote.

Source:Radio Vaticana

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...