Kanisa la Pentecoste [MMPT] lililopo Buronge katika
Manispaa ya Kigoma/Ujiji liisa
hilo,mabechi 14, ubao wa kufundishia, mikeka 3 na mlango 1 viliteketea kwa
moto.Jumla ya mali zilizoteketea kwa moto ni Sh.Milioni 1,337,000.Kamanda huyo alisema “kiini cha tukio hili bado
kufahamika, hakuna madhara kwa binadamu, upelelezi wa tukio hili unaendelea ili
kuwabaini wahalifu hao kwa hatua za kisheria”alisema.
Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste
[MMPT] Emanueli Simoni [49] alisema,”mimi nilipata taarifa kuwa kanisa langu
limeteketea kwa moto, nilikwenda polisi Sentro kutoa taarifa, ndipo tulikwenda
eneo la tukio tukakuta kanisa lote limeteketea kwa moto”alisema.
Eliasi alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya
saa 4 usiku katika eneo la Buronge katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji.Alisema katika kanisa kulikuwa na Mabechi 14,
Mlango 1, Vilago 3, Sanduku za kutozea sadaka na ubao wa kufundishia.Vyote
vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 1,337,000 mali ya kanisa hilo.Alisema ajui watu waliochoma kanisa hilo, wala
hakuna mtu anayeshikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.
Mchungaji huyo anaiomba serikali iangalie sana
matatizo ya uchomaji wa makanisa sasa yanaenea nchi nzima. Pia amelitaka Jeshi
la polisi Mkoani hapo kufanya doria kwenye makanisa wakati wa usiku ili
kukomesha vitendo vya uchomaji wa makanisa.
Alisema kanisa ni taasisi ya jamii hivyo anaomba
serikali ichangie gharama ya ujenzi wa jengo hilo ili wananchi wanaohabudu
katika kanisa hilo wapate sehemu ya kuabudia.
No comments:
Post a Comment