Tuesday, October 9, 2012

Kutana na Atosha Kissava Muimbaji Kutoka Mzumbe University Morogoro


Minister Atosha kissava
Atosha kissava si jina geni miongoni mwa waimbaji nchini, ni mmoja kati  ya watumishi wenye upeo mpana kwanza na yule wanayemtumikia pamoja na kile ambacho wameitiwa kufanya katika ufalme wa Mungu.Kwa sasa Atosha ni mwanafunzi katika chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, anatokea mkoani Iringa na alikuwa mmoja wa waimbaji waliofanya vyema kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu katika uwanja wa Taifa.

Akiwa mjini Morogoro Atosha ameiambia Hosanna Inc kuwa album yake ya sasa inaitwa NAINUA MACHO YANGU JUU na inajumla ya nyimbo nane ambazo ni


1.Nainua macho yangu juu

2.Alfa&omega

3.Unaweza

4.Nifanane na wewe

5 Nibariki na mimi

6.Kwake yesu

7.Njoni njoni

8.Yatima

Shughuli nzima  ya kurekodi haikuwa kazi nyepesi sana kwani ilimbidi afanye uwianao wa kati ya Masomo na huduma na hatimaye baada ya kumaliza uandishi wa nyimbo aliingia studio na kurekodi Audio katika studio za LIGHT MEDIA chini ya producer AMBA. Amba ni mmoja kati ya maproducer wakongwe mkoani IRINGA na amekuwa akiproduce kazi nyingi za Rais wa wanamuziki wa injili nchini Mtumishi Addo November.

Atosha akiwa mbele ya camera
Atosha alizidi kuiambia Hosanna Inc kuwa video album yake imefanywa na kampuni iitwayo Complex Corner chini ya editors MECK XAVERY na  HENRY MBILINYI.Kuna tofauti kubwa kati ya video za Atosha na video nyingine za gospel ambazo zimezoeleka, hii yake imeonyesha ubunifu wa hali ya juu na imeondoa kwa kiasi kikubwa ile dhana kwamba wanamuziki wa Injili huongoza kwa kutengeneza video mbovuwakiwa na lengo la kukwepa gharama.

Vocaly yeye husema ni kwa Neema tu, kiukweli GOD has blessed her Mightly,Katika album yake hii ya  NAINUA MACHO YANGU JUU  sauti  ameingiza yeye peke yake.Kwa upande wa video kuna wadada watatu  Angelita Mtae, Glory Mawenya,na Grace Kamete ambao wamemsapot katika kufanya video album hiyo.Hii ni moja kati ya album nzuri nchini na Hosanna Inc inaamini kuwa yule Mungu aliyeianzisha kazi ndani ya ATOSHA, atasimama na kuhakikisha anaitimiza kwa utukufu wake.

GOD is Good  

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...