KUHUSU
MATUKIO
YA
UCHOMAJI WA MAKANISA MBAGALA DAR ES SALAAM.
Oktoba
12 mwaka huu, matukio mabaya na yenye kutia doa sifa ya amani umoja na
Utengemano wa Taifa la Tanzania, yalijitokeza huko Mbagala Jijini Dar es
Salaam, wakati watu wenye jazba wanaoaminika kuwa ni Waislamu wenye msimamo
mkali walipovamia makanisa saba na kuyachoma moto eti kwa kulipiza kisasi cha
mtoto aliyekojolea kuran katika utani wa kitoto.
Askofu Mkuu wa TAG nchini Askofu Barnabas Mtokambali |
Katika
mkasa huo ambao ni kama muendelezo wa ghasia zingine zilizotokea kule Zanzibar
miezi michache iliyopita na kuteketeza makanisa mbalimbali mbali na kuharibu
mali za kanisa na zile za watu binafsi.Tukio
la Mbagala limesababisha makanisa saba kuharibiwa vibaya, mali kuibiwa na hata
kuhatarisha maisha ya watanzania na kuwafanya waishi kwa hofu na kupoteza
matumaini.
CHANZO
CHA TUKIO
Kwa
mujibu wa walioshuhudia, Polisi na wahusika (Waislamu) chanzo cha ghasia hizo
na mabishano ya kitoto baina ya watoto wa dini ya Kiislamu na kikristo,
waliobishana kuwa ikiwa mtu atakojolea kuran na kuitemea mate atageuka mbuzi au
nyoka.
Lakini
baada ya tukio hilo la kitoto watu walilikuza na kulipeleka kwenye misikiti na
hivyo kuchocheza ghasia. Kimsingi tukio lenyewe ni jepesi sana ukilinganisha na
matokeo yake. Ukweli kwamba waliofanya utani huo ni watoto na chanzo chake ni
mabishano ya kitoto, unatia shaka kuwa huenda kuna hoja nyuma ya pazia ambayo
isipotazamwa kwa makini inaweza kulete matokeo mabaya sana.
Jambo
linalonitia shaka ni kufanana kwa matukio ya kuchomwa moto kwa makanisa ya
Zanziabar na ya Mbagala ambapo hakukuwa na uhusiano wa vyanzo vya ghasia na
makanisa husika.
Mfano;
Ghasia za Zanzibar zilizopelekea kuangamizwa kwa makanisa zinaelezwa kuwa
zilitokana na kikundi cha Kiislamu cha Uamsho wa Mihadhara, kilichokuwa
kikiandamana kudai mjadala wa Muungano, lakini zikaishia kwenye uchomaji wa makanisa,
hapa hauonekani uhusiano wa kanisa na Muungano; nalazimika kujiuliza kulikoni?
Vivyo
hivyo tukio la Mbagala halina uhusiano wa moja kwa moja na kanisa kwa kuwa
hakuna ushahidi wala hata tetesi kuwa mtoto huyo alitumwa na kanisa lolote.
Wahusika wa dini ya Kiislamu akiwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
analielezea tukio la kitoto kama lisilostahili hata mtu kufunguliwa mashtaka
bali kuelekezwa tu. Ni vipi lisababishe uchomaji wa makanisa?
MAKANISA
YALIYOCHOMWA MOTO
Katika
ghasia hizo za aina yake, makanisa saba yamethibitishwa kuharibiwa kwa kuchomwa
moto, kupasuliwa vioo, viti na kuibiwa vyombo vya muziki na jenereta. Makanisa
hayo ni TAG Kizuiani, Agape, Kibonde maji, SDA Sabato, Mbagala Kizuiani,
Katoliki Kristo Mfalme Mbagala Rangi Tatu, Anglican Mbagala Kizuiani, KKKT,
Mbagala Zakhem na TAG, Shimo la Mchanga.
Pamoja
na majengo hayo kubomolewa kwa viwango tofauti mengine yakichomwa moto, pia
wahusika waliiba Genereta, na vyombo vya muziki vya makanisa hayo na kuvunja
magari na baadhi yao kuchomwa moto.
Choko
choko zilizinazoweza kuwa cahanzo cha matukio hayo ni:
Januari
sita mwaka huu, kikundi kimoja kinachoitwa JUAKITA, kiliitisha kongamano la
kujadili katiba mpya Tanzania, kwa upande wa Waislamu. Katika kongamano hilo
lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kulitolewas kauli
za kichozi kama:
1.
Lazima Rais ajaye atoke Zanzibar
2.
Kukabiliana na ukuaji wa kasi wa dini ya Kikristo
3.
Kupinga Muungano ili kuupa nguvu Uislamu
4.
Kupigana kufa na kupona kutetea maslahi yao wakati huu wa kuandaa katiba mpya.
Kauli
hizo zilitolewa na Sheikh Nasoro Mohamed, kutoka Zanzibar, ambaye alikuwa mgeni
rasmi. Baadaye zikaandaliwa kanda za CD zilizosambaza ujumbe huo.
Uchunguzi
unaonesha kuwa uchochezi huu umekuwa ukiwaandaa watu kusubiri vijitukio vidogo
tu ili kulipua ghasi. Tuliona jinsi makanisa yalivyochomwa kule Zanzibar. kwa
kuwakumbusha tu makanisan yaliyoangamizwa katika tukio hilo ni: EAGT, Elimu
Pentecost na TAG, Anglikana, Katoliki na FPCT.
Ni
jambo la kusikitisha kuwa matukio haya yanatokea siku mbili tu kabla ya
maadhimisho ya miaka 13, ya kifo cha Rais wa Kwanza, Mwl. Julius kambarege
Nyerere. Leo hotuba na midahalo inarindima kila mahali kumuenzi Nyerere, lakini
wengi wetu tukiwa tumejaa majozi baada ya nyumba zetu za ibada kuharibiwa
katika matukio yanayoashiri hatari kubwa.
Hofu
yangu ni kuwa, roho hii ya ubaguzi wa kidini ambayo Baba wa Taifa hayati Mwl.
Julius Kambarage Nyerere aliifananisha na dhambi ya kula nyama ya mtu, imekuwa
ikiyatafuna mataifa ya Afrika kama ifuatavyo:
1.
Mwaka 2000, vuguvugu la kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu (Sharia), lilianza
kwenye majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria, miaka michache baadaye majimbo kadhaa
yakajitangazia sheria hizo na tangu wakati huo kumekuwa na mapambano
yasiyoisha. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka ya karibuni zaidi ya Wakristo
500 wameuawa kikatili na makanisa kuchomwa moto.
2.
Roho hii imekuwa ikienea kwa kasi katika maeneo mbali mbali ya Afrika ambapo
imelikumba taifa la Mali, majimbo ya kaskazini tayari yametangaza kujitenga na
kuna vuguvugu lenye kuhusisha mapigano ya silaha.
3.
Itakumbukwa kuwa miezi michache tu ilizopita vuguvugu hili la kudai utawala wa
kidini liliibuka nchini Kenya ambapo watu wanaojiita wanaharakati walianzisha
madai ya kutaka eneo la Pwani kujitenga na Jamhuri ya Kenya na kujitangazia
taifa la Kiislamu.
4.
Katika tukio hilo inasemekana mtoto huyo alitengenezewa mabishano ya kitoto
kuwa akichoma kurani atakuwa chizi naye akabisha
kisha
akapewa kiberiti na kurani akachoma tena walioandaa
mzaha
huo wakamkamata na kumpeleka mahakamani.
Tukio
linalofanana na hilo lilitokea tena Bagamoyo mkoani Pwani
ambapo
mtoto wa kike alishtakiwa na hata kuhukumiwa kifungo
kwa
madai ya kuchoma kuran lakini tukio lilikuwa katika mabishano
ya
midhaha ya kitoto
WITO
WANGU
Natoa
wito kwa Wakristo wote nchini kujiepusha na mizaha
inayoweza
kutengeneza sababu za kulipuka kwa ghasi na kutengeneza
mwanya
wa watu wenye nia mbaya kutekeleza agenda zao zaria Ili
kulinda
amani umoja na utengemano wetu, nawasihi viongozi wa makanisa
kuonya
na kukemea waumini na watoto wetu wasishiriki kwa namna yoyote ile mizaha
inayopelekea kuchoma au kuharibu vitabu au nyaraka
za
kidini.
Nawasihi
watanzania wote kwa ujula kujiepusha na mizaha ya kidini inayoweza kuchafua
amani yetu, na pale jambo lolote lenye kukera linapotokea tujiepushe kuwa
mawakala wa shetani wa kueneza chuki badala ya amani na upendo.
USHAURI
WANGU KWA SERIKALI NA VIONGOZI
Nawashauri
viongozi wa Serikali ambao leo wanatoa matamko na kushiriki midahalo ya
kumuenzi Mwl. Nyerere kukumbuka kuwa huyo alikuwa na mapenzi makubwa na amani
na umoja wa taifa. Kwa hiyo kumuenzi kwa vitendo ni kudumisha utawala bora,
unaofuata sheria usio na chembe ya ubaguzi wa aina yoyote.
Kulipuka
majukwaani kumuenzi Nyerere bila kuilinda na kuitetea amani ya nchi ni
kujidanganya.
Ni
wajibu wa kila Mtanzania kutii sheria na mamlaka kwa kuwa zimewekwa/kuruhusiwa
na Mungu, hivyo kuziasi ni Kumuasi Mungu, yaani ni dhambi. Hivyo kila Mtanzania
anastahili kukumbuka wajibu wake wa kutii mamlaka.
Viongozi
wenzangu wa dini wakumbuke kuwa wana wajibu mkubwa katika jamii, na jamii
inawasikiliza hivyo ni vyema wakawa makini katika matamshi na maelekezo yao ili
wasiwe chanzo cha kuchochea vurugu za kidini na uvunjaji wa amani.
Pia
ningependa kuwashauri viongozi wa serikali kusimama imara katika kusimamia
sheria na haki, na kuepuka kauli au vitendo vitakavyofanya baadhi ya watanzania
kudhani kuwa hawatendewi haki.
Ni
vema ieleweke kuwa matukio kama haya ya uvunjaji wa amani yasipodhibitiwa na
kukomeshwa haraka yanaweza kuumba chuki ambayo inaweza kuibua mlipuko mkubwa na
machungu kwa wananchi na matokeo yake yakawa mabaya kwa Taifa zima. Hekima na
busara inatufundisha kuwa tusipoziba ufa tutajenga ukuta.
Ni
vyema wenye dhamana ya kuongoza wakakumbuka kuwa wanawajibu mbele ya Mungu
aliyewaweka au kuwaruhusu kuingia madarakani na siku moja watatoa hesabu mbele
zake.
Ni
vyema viongozi wa Serikali wakajizuia kufanya maamuzi yanayoashiria upendeleo
kwa baadhi ya makundi ya kidini na kukiuka utawala wa sheria, mfano; kutii
waandamanaji na kuwaachia bila mashrti watu waliokamatwa kwa mujibu wa sheria
kuna jenga kiburi kwa makundi yenye kiu ya matumizi ya nguvu na kujenga hofu
kwa pande zingine.
Ni
vyema mamlaka zikasiamama katika sheria na kufanya hukumu kulingana sheria
badala ya kuamua mambo ya kisheria kisiasa.
WITO
MAALUMU KWA VIONGOZI WA DINI
Nitumie
nafasi hii kuwasihi vingozi wenzangu wa dini, kusimama imara katika kuombea
taifa na kuhubiri kwa nguvu ili kukabiliana na giza la kiroho ambalo linatishia
kuifunika nchi.
Takwimu
za karibuni kabisa za utafiti uliofanywa na taasisi ya Washnton DC iitwayo, Pew
Research Centre, na kurushwa na Televisheni ya CNN, Katika kipindi chake cha
Inside Africa, zilionesha kuwa watanzania asilimia 93, wanaamini mambo ya
ushirikina na uchawi wakati Uganda ni asilimia 29 na Kenya ni asilimia 27. Tu.
Mahali ambapo giza la kiroho limezingira kiasi hiki ni lazima matukio ya
kishetani yashamiri tuchukue hatua.
Mwisho,
natoa wito kwa watanzania wenzangu tuulinde umoja, amani na utengamano wa taifa
letu, tuikimbie dhambi ya ubaguzi kwa kuwa tukiiruhusu itatuangamiza sote.
Tuliombee taifa letu na kukiwa na mbegu ya chuki tuimalize kwa njia ya
majadiliano na vikao vya pamoja vinavyohusisha viongozi wa dini zote na
serikali pia.
Imetolewa
leo 14/10/2012
Na
Dk. Barnabas Mtokambali
Askofu
Mkuu wa TAG
Amina,powerfull message,God bless Tanzania God bless Africa.
ReplyDeletewe declare peace over you Tanzania and we proclaim Jesus is Lord over you in JESUS' name,no weapon formed against you shall prosper in the name of Lord Jesus.
Diana & Bubele(Tanzanians in Birmigham)
Kwakweli inasikitisha sana, hali ni mbaya sana.Hata hivyo tunamuomba Baba wa Mbinguni, aingilie kati, maana yeye anajua yote.
ReplyDeleteEnny
Jesus is Love and his love for Tanzania will preserve us and our nation but when and only when we shall turn and repent and pray....2Chronicles 7:14.
ReplyDeleteplay your part and God bless you.
Hakika yatupasa kuwa waangalifu sana hasa pale ambapo pana utata uliokinzika, hekima na busara ni kitu cha msingi sana lakini zaidi ya yote ni neema tujaliwayo katika kuyaona kwa namna yake mambo yenye utata.Ee Mungu tujalie namna nyepesi ya kuenenda na haya.
ReplyDeleteZablon