|
Paul Mwangosi wa pili akiimba sambamba na
marehemu Fanuel Sedekia |
Tanzania
Praise and Worship Team ni kundi la kusifu na kuabudu linaloongozwa na Mtumishi
wa Mungu Paul Mwangosi.Dhumuni kubwa la uwepo wa Kundi hili ni kumwabudu MUNGU
katika ROHO na KWELI.Mnamo mwaka 2008 mmbeba maono wa Kundi hili mtumishi
Mwangosi ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akihudumu kama kiongozi wa kusifu
na kuabudu katika semina za Mwl Christopher Mwakasege alipata maono ya
kuanzisha Kundi litakalokuwa likimsifu Mungu kwa namna ya kipekee.
Ilipofika
mwaka 2011 Mtumishi Mwangosi aliwaita marafiki na jamaa kisha akawashirikisha
maono yake, Maono hayo yalipokelewa vizuri ndipo ikaundwa kamati maalumu ya
kuhakikisha maono hayo ya kuwa na BAND na KUWA NA SIKU MAALUMU ambayo nchi
nzima itakuwa ikimsifu na kumuabudu Mungu yanatimia nah ii itaanzia jijini Dar
es Salaam na kusambaa mikoa yote. Kwa kuanza mwaka jana 2011 ulifanyika Mkesha ule
usiku wa kuamkia siku ya kuadhimisha miaka 50 ya Tanzania, mkesha huu
ulifanyika katika kanisa la City Christian Centre(CCC) na kuanzia hapo maono
hayo yaliendelea
Kwa
Mwaka huu wa 2012 tukio hili litafanyika usiku katika kanisa la City Christian
Centre(CCC-Upanga) mnamo tarehe 7-11-2012
ambapo waimbaji mbali mbali wa hapa nchini watahudumu kwa lengo moja tu la
kumpatia Mungu Ibada.
Kwa
kuwa maandalizi ya mkesha huo yanahitaji pesa, kamati nzima inayoratibu mkesha
huon iliyo chini ya Mtumishi Emmanuel Kwayu, iliamua kuandaa Chakula Maalumu
kilichoambatana na Harambee.Hafla hii nzima ilifanyika usiku wa jana tarehe
16/11/2012 kuanzia saa 2: 00usiku mpaka saa 4: 00 usiku katika hotel ya Peacok jijini
Dar es salaam ambapo watu walijumuika pamoja wakiongozwa na Band ya Tanzania Praise
and Worship team.
Hapa
chini ni sehemu ya matukio ya hafla hiyo na jipange kuhudhuria siku hiyo
7-11-2012 kwani
ni siku ya kihistoria.
|
Ukumbi ukiwa tayari kwa Hafla |
|
Shangwe |
|
No Coment |
|
Audience ikienda sawana Praise Team |
|
Simon Jengo Mratibu wa Kamati akieleza jambo katika hafla hiyo |
|
Tanzania Praise and Worship Team Ikihudumu |
|
Tumbo ni Kwa Chakula, na Chakula ni kwa Tumbo, that is Biblical |
|
Bloggers | | |
Angalia Praise Team Ikihudumu Siku ya Jana
No comments:
Post a Comment