† Awashukia Wanasiasa
Wanaoendekeza Itikadi Zao Hadi Kwenye Makanisa Na Michango Yake
Mh Freeeman mbowe |
MWEYEKITI wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA) Freeeman mbowe amewataka wanasiasa kuachana na tabia ya
kupeleka itikadi zao za kisiasa hadi ndani ya makanisa kwa kuwa itikadi hizo za
kisiasa zinaonekana kushamiri hata kwenye baadhi ya makanisa na hivyo kunyima
maendeleo ingawaje wanasiasa hao wana nafasi kubwa sana ya kuchangia
Mbowe aliyasema hayo wiki iliyopita katika
harambee maalumu ya kuchangia mabweni ya shule ya Ufundi yaOlikii ambayo ipo
chini ya kanisa la KKKT Dayosisi ya kaskazini kati ambapo pia katika harambee
hiyo jumla ya Milioni 10 ziliweza kupatikana
Alisema kuwa inashangaza sana kuona kuwa baadhi
ya wanasisasa wanashindwa kuchangia shuguli mbalimbali za maendeleo ya kanisa
au kushiriki hata kwa pamoja katika kuchangia michango au kuendesha harambee
kwa kuhofia kukutwa na Mwanasiasa mwingine jambo ambalo kama litaendelea hivyo
basi litasababisha kabisa maendeleo ya kanisa kuwa hafifu sana
Aliongeza kuwa wanasisa wanapswa kujua na
kutambua kuwa ni wajibu wao hata kuhakikisha kuwa wanakuwa sehemu ya
kanisa kwa kuweza kuendesha shuguli mbalimbali za maendeleo hasa katika
ujenzi wa makanisa pamoja na mambo ya msingi ambayo yanafanywa na kanisa la leo
ambapo kwa sasa bado hali ya kiitikadi inaendelea kushamiri ndani ya makanisa
Alifafanua kuwa hali hiyo pamoja na kuwa si njema
sana kwa maendeleo ya kanisa kama itaendelea hivyo itasababisha kasi ya
kumjua Mungu hasa katika siasa hizo itapungua sana na badala yake kasi
hiyo itaelekezwa zaidi katika mapabano ambayo hayana maana huku mapambano hayo
huenda hata yakasabisha sana baadhi ya watu kukosa Amani dhidi ya wanasiasa hao
“inashangaza sana leo mimi kama Mbowe nikionekana
mahala hapa ambapo ni patakatifu basi mtu wa CCM haji wala hashiriki kabisa
sasa je tunajenga taifa la Kichadema au Ki CCM hapa na hali hii si hali ya
kuendelea kuingalia kwa macho yetu bali hali hii inatakiwa kuangaliwa hata na
viongozi wa dini wasimame vizuri na hata ikiwezekana waombe si jambo zuri
kwani kama ni Siasa basi zisiingizwe itikadi hadi ndani ya makanisa yetu kwani
pia hali hiyo inasababisha tuyabomoe na wala sio kuyjenga;’aliongeza Mbowe
Katika hatua nyingine alisema kuwa nao wanasiasa
ambao wanangangani itikadi za kivyama wanapaswa kujua na kutambua kuwa kamwe
hawapaswi kufunga ndoa na vyama vya kisasa bali wanatakiwa kuhakikisha kuwa
wanakuwa wazalendo wa vyama vyao na kamwe itikadi kati ya CCM na Chadema
isisababishe wakashindwa kutumikia Taifa hasa kwa Upande wa Makanisa yao.
Awali Meneja wa Shule hiyo ya Sekondari na Ufundi
ya Olikii Mchungaji Izack Kisiri alisema kuwa lengo halisi la kufanya Harambee
hiyo ambayo imefanikiwa kukusanya kiasi cha Zaidi ya Milioni 10 ni kuendeleza
Mabweni kwa wanafunzi wa shule hiyo ili kuimarisha zaidi elimu
Mchungaji Kisiri alisema kuwa pamoja na kuwa
wamefanikiwa kupata zaidi ya Milioni 10 lakini bado shule hiyo ina hiuitaji
mkubwa sana wa mabweni kwani endapo kama kutakuwa na Mabweni ya kutosha
basi itaweza kuongeza sana hata kiwango cha elimu hasa katika eneo hilo la Olokii
ambalo bado lina uhitaji mkubwa sana .
‘tunafikiria kukusanya kiasi cha Shilingi Milioni
250 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili lakini kwa awamu hii ya kwanza
tunashukuru Mungu tumepata hii Milioni 10 lakini tunawatia Moyo wakristo na
wadau wengine wa elimu kuhakikisha kuwa wanatuunga mkono na kuweza kuimarisha
elimu hasa kwa kuwa na mabweni imara”aliongeza Mchungaji Kisiri.
Awali Askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri
mkoani hapa( KKKT)dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt Thomas Laizer alisema kuwa ni
jambo la ajabu sana kwa wanasiasa kuchukiana ovyo kwa kuwa siasa inaenda kama
mchezo wa mpira ambao kamwe hautabiriki na hivyo wanatakiwa kuhakikisha kuwa
wanajijengea tabia ya kupenda na kuthaminiana wao kwa wao hasa kwenye majukumu
ya msingi ya Kimaendeleo.
Dkt Thomas alisema kuwa wapinzani kuwakataa
watawala na watawala kuwakataa wapinzani si jambo jema na halitakiwi
kuendelezwa kwa sasa kwani wote wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa kitu
kimoja na kutatua matatizo mbalimbali ambayo yanaikabili jamii kwa sasa
likiwemo suala zima la uvunjifu wa amani ndani ya Nchi.
Na Bety Alex, MERU
No comments:
Post a Comment