Thursday, November 8, 2012

Purukushani za Grezy G.K na mamaye Mh Naomi Kaihula(Mtumishi)




Kushoto ni Ambwene Yesayah (A.Y), Gwamaka Kaihula(Crezy G.K) Hamisi Mwinjuma(Mwana F.A) wakati WA Mahafali ya Gwamaka wiki iliyopita

Mheshimiwa Naomi Kaihula ni Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).Kabla hajawa Mbunge Mh Kaihula alikuwa Mwalimu wa Sekondari ya Tambaza kisha baadaye alijiendeleza Kimasomo, baadaye alichukua Shahada ya Uzamili(Masters degree) kisha akaajiriwa kama Lecturer wa moja ya vyuo vya elimu ya juu hapa nchini.

Pamoja  na CV hiyo fupi, mama huyu AMEOKOKA, na pia ndiye mama mzazi wa Mwanamuziki wa hip Hop Gwamaka Kaihula(Krezi G.K) kutoka EAST COAST TEAM. Nilibahatika kuwa mmoja wa wanafunzi wa mama huyu, nakumbuka chuoni, moja kati ya vitu alivyokuwa akituambia ni kuwa”Msifuatishe Gwamaka(G.K) nshapiga kelele sana arudi darasani asome yeye anakalia hayo hayo tu, nawaambia nyie someni ipo siku mtamuajiri. Wakati mwingine aliwahi sema NAFANYA MAOMBI SANA ILI GWAMAKA ABADILIKE asome kama nyinyi, haya ni moja kati ya maneno mbayo siwezi yasahau.

Wiki moja iliyopita Gwamaka Kaihula(G.K) alihitimu Shahada yake ya kwanza kutoka chuo kikuu cha Tumaini Dar es Salaam Campus(TUDARCO), na hii ni baada ya miaka sita(6) toka mama huyu atoe zile kauli, kumbuka wakati anasema hivyo darasani alikuwa akidai miaka mingi amekuwa akimuimbia mwanaye arudi shule lakini wapi.Hapa KIBIBLIA tunajifunza kitu kuwa kuna mambo mengine unaweza yaombea na Kuyaombea utashirikisha watu wataomba but yanaonekana kama bado hayaendi, good thing ni kwamba Mungu wetu ni mwaminifu HUFANYA.

Kwa mtu yeyote aliyeokoka na mwenye mtoto atakuwa akielewa vizuri ni namna gani mzazi unaumia pindi unapoona mtoto hajakaa sawa kitabia. Cha msingi hakuna kukata tamaa ni kwenda mbele za Mungu bila kukoma na kwa wakati wake hufanya. Inawezekana labda umekuwa ukiomba Mungu afanye jambo Fulani miaka nenda rudi, elewa MUNGU wetu hajatupungukia  wala hajalala, ni Mwingi wa FADHILA atajibu tu tusipozimia ROHO.


Mh Naomi Mwakyoma Kaihula kushoto, mama mzazi wa G.K akiwa Bungeni Dodoma

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...