Saturday, November 10, 2012

Baada ya kuokoka DOTNATA aachia nyimbo yake ya Injili


Husna Posh "Dotnata"
Mwigizaji mkongwe wa kike katika tasnia ya filamu za kibongo, ambaye pia ni mjasiriamali Husna Posh 'Dotnata', baada ya wiki kadhaa kuutangazia umma kuwa ameokoka na ana mpango wa kufungua kanisa, kwa sasa amekuja na nyimbo mbili za muziki wa injili. Kati ya hizo ameanza kwanza kuiacha nyimbo yake inayokwenda kwa jina la  Baraka.

Ndani ya nyimbo hiyo alisema kuwa ameamua kuwashirikisha wasanii chipukizi wawili wa kike ili kukuza vipaji vya wasanii katika upande wa nyimbo za injili
"Kwa sababu nyimbo inaitwa baraka nimeamua kuwashirikisha wasanii wa kike ili baraka zianze kwa wakina mama kwanza, na pia ni katika hali ya kukuza vipaji vya wasanii kwenye upande wa nyimbo za injili" alisema Dotnata

Alisema kuwa uwezo aliouonyesha kwenye nyimbo hiyo ni mkubwa sana ,huku akisisitiza kuwa nyimbo hiyo imebeba maudhuhi ya hali ya juu yanayoendana na jina lenyewe la baraka hivyo aliwaomba watanzania waipokee nyimbo hiyo na waifanye ya kwao ili wapokee baraka hizo

Aliongezea kuwa nyimbo hiyo ambayo tayari ameshatoa video yake, na tayari imeanza kupigwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari aliwataka mashabiki wake wakae tayari kuzipokea nyimbo nyingine ambazo hivi karibuni ataziachia.Hosanna Inc jumamosi ya leo imefanikiwa kuisikiliza moja ya nyimbo hizo kupitia WAPO REDIO.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...