Tuesday, November 6, 2012

Waziri wa Zamani wa Mashauri ya Kigeni wa Israel asema niliwahi fanya Mapenzi na Mashakhsia Muhimu wa Kiarabu ili kupata taarifa Muhimu kwa maslahi ya IsraelMh Tzipi Livni

Tzipi Livni aliyewahi kuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kwamba, aliwahi kuwa na mahusiano ya kingono na baadhi ya shakhsia na wanasiasa wa Kiarabu. Livni amesema, alipokuwa anafanya kazi katika Shirika la Kijasusi la Israel MOSAD wakati mwingine alikuwa akifanya mapenzi na shakhsia muhimu wa kiasiasa wa Kiarabu ili aweze kupata taarifa muhimu. 

Aidha waziri huyo wa zamani wa Mashauri ya Kigeni wa Israel anasema kwamba, alifanya hivyo ili kuwaharibia majina wanasiasa na shakhsia hao, kuwatengenezea faili la kashfa au wakati mwingine alikuwa akifanya hivyo ili kuwalainisha wakubaliane na msimamo fulani wa Israel. Tzipi Livni aidha sambamba na kukiri utovu huo wa kimaadili hadharani amesema bayana kwamba, haoni vibaya kuwa na mahusiano ya kingono kwa ajili ya kupata taarifa muhimu kwa maslahi ya Israel, anajivuni kwa hilo na kwamba, ikilazimu yuko tayari kurudia tena kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...