Monday, August 29, 2011

Album Preview : Amejibu Ahadi By Beatrice Muhone


Amejibu ahadi ni Album ya pili ya Mwanamama Beatrice Muhone kutoka jijini Arusha. Video album hiyo imefanywa na Sowers Group na editing ilifanyika  katika jiji la Kampala nchini Uganda chini ya Tondas Studio.

Hakuna Rafiki Kama Yesu

Hapana Rafiki kama Yesu ni nyimbo ambayo Beatrice amesisitiza kuwa hakuna Rafiki kama Yesu kwa kuwa Yu Pekee. Hii ni Nyimbo ya Tenzi na kiukweli Beatrice ameiimba kwa umahiri mkubwa. Mwanamama Christeline Mke wa Mike Matumaini ndiye aliyemfanyia make up Beatrice, na hivyo amependeza sana humo ndani.

Beatrice akiwa nje na mizigo yake baada ya kuambiwa hakuna Nafasi
Nyimbo alianza na kijistori kuwa Beatrice akiwa bize akipanga nguo kwenye begi kisha  akampigia simu Rafiki yake na kumfahamisha kuwa ataenda kumsalimia kesho yake kwa kuwa yuko likizo, Rafiki yake huyo  alimkubalia kuwa hakuna Tazizo na ntakuja kukupokea lakini Mwisho wa siku alivyofika hakupokelewa, na hata  alipofika na kugonga mlango kijana wa Rafiki yake alimfungulia na kumwambia mama amesema hakuna nafasi Ondoka. Kisha Beat ikaanza tartibu na Beatrice akaingiza sauti. Ni nyimbo nzuri.

Sioshwi Dhambi zangu

Hii ni Nyimbo ya Tenzi inayoelezea NGUVU YA DAMU YA YESU. Ndani ya Video hii inaanza Beatrice akiwa anaingia kanisani huku akiwa amevaa koti la Jeans  kisha akaanza kufanya maombi. Hii nyimbo ina beat flani hivi simple na Jamaa aliyekuwa akishoot hii video alipiga close up za ukweli. Locations za video hii ni kanisani pamoja na ufukweni ambako Beatrice alikuwa amevaa gauni jeupe. Katika video hii nzima Beatrice anaonekana peke yake pasipo watu kumback.

Beatrice akiwa kanisani
Si  njia Rahisi
Katika Nyimbo hii Beatrice anaelezea sio kazi nyepesi kutembea na Yesu, lakini anasema Yesu huyarahisisha mambo mazito yaliyo katikati yetu kwa kuwa yeye huiongoza safari. Pamoja na kwamba hii ni Nyimbo ya Tenzi ila Beatrice aliibadilisha kidogo kwa kuweka maneno mengine ambayo hayamo kwenye tenzi hiyo.

Si njia Rahisi
Katika Video hii inayoonekana Beatrice akitembea barabarani Bro aliyeshoot video hii alipiga Long shoots nyingi nzuri na  kuna watu wanamback up huku sauti flani ya kiume ikiongea. Dressing calour ya Nyimbo hii ni Black.


Uruwera
Kama wewe ni worshiper itafute hii nyimbo inaitwa Uruwera ambalo ni neno la Kinyarwanda lenye maana MTAKATIFU. Ni Nyimbo inayotaja Sifa na UKUU wa MUNGU wetu.  Video inaanza Beatrice yuko bize akimsogelea Ndege Tausi kisha wanyama mbalimbali wanaonyeshwa.
Location za wimbo huu ni kama porini au mbuga flani hivi,na kuna sehemu kadhaa zinaonekana nyumba za asili. Nyimbo hii ni ya taratibu mno na kuna sehemu kadhaa Beatrice ameiimba kwa Lugha ya Kinyarwanda. 

Beatrice akiimba katika wimbo wake wa Uruwera

 Amejibu Ahadi
Nyimbo hii iliyobeba jina la Album,  ni nyimbo ya Furaha,  msingi wake ni Kumshukuru Mungu mara baada ya MUNGU kujibu maombi ya Mwanadamu yaliyodumu kwa Muda Mrefu.  Ndani ya Nyimbo hii Beatrice anasisitiza Kuwa ’’ UU MUNGU KWA KUWA WEWE NDIO NGAO YA WOKOVU WANGU’’, Wema wako na uaminifu  wako ni wa ajabu, umenipaka mafuta ya shangwe nakuinua juu. Hii ni moja kati ya nyimbo ambazo Beatrice ameandika zenye kumfanya kila mtu aisikilizaye kumshukuru Mungu kwa MENGI aliyofanya kati yetu.

Video ilianza Beatrice akiwa na furaha  mno

Bite akiimba ndani ya Amejibu ahadi

I luv you Jesus

Nyimbo hii iliyoibwa kwa lugha ya kiingereza Beatrice anasisita I luv You Jesus because you Loved me Before , Your Holly. Your Might. Kuna Crew kubwa ya kumback up na nyimbo nzima location ni Studio na sehemu kidogo nje ya studio. Shoots zimechukuliwa usiku. 

Bite akiingiza Saut katika I LUV YOU JESUS

Bite akiwa na watu wakimback up 
 
Huniongoza:
 
Katika  Nyimbo hii Beatrice ameuonyesha ukuu wa MUNGU kwa kusema ‘Huniongoza hunishika kwa mkono wa hakika , nitaandamana naye kristo aniongozaye”. Kwa kifupi ni nyimbo inayotaja na kuelezea uweza wa Mungu katika maisha yetu ya kila siku.

Video ya huniongoza inaanza Beatrice akiwa ndani ya kiatu hiki, kaaaazi kweli kweli
Ndani ya Video ya nyimbo hii ambayo kwa sehemu kubwa imekaa kisasa zaidi kuanzia beat, uvaaji na hata uchezaji, pia  kuna mtu alishirikishwa kisha akarap ingawa kwenye video haonekani bali sauti tu ndio inasikika. Video hii inamahadhi ya kuwavutia vijana zaidi kwa kuwa uvaaji wa Beatrice na Wale Dancers wanavyoshake ni kivutio kwa kizazi kipya kilichopo kanisani.

Beatrice akienda sawa na Madancers katika Huniongoza 

Yesu unipendaye

Ni Nyimbo ya Tenzi inayoonyesha upendo wa Yesu kwetu kwa kuwa ngome nyingine hatuna  zaidi ya Yesu. Nyimbo hii mwanzo mpaka Mwisho anaonekana akiwa mbele ya kanisa kubwa na kuna baadhi ya Sean anaonekana yuko msituni. Sehemu kubwa ya album hii ya video ya Amejibu Ahadi Beatrice anaonekana akiwa na Nywele Fupi.

Bite akiwa mbele ya kanisa kubwa akiimba Yesu Unipendaye

Beatrice Muhone

  


Studio  : Tondas Studio
Directed By:  Mike Matumaini
Sound: Kosto Zahinda
Script:  Mike Matumaini
Light : Oswald Basoka
Camera: Sam M M Kikere
Executive Producer: Godfrey Muhone

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...