Sunday, August 28, 2011

Ushuhuda: Namna lilivyopatikana Eneo yalipo Makao Makuu ya Huduma ya Winners Chapel Duniani



Askofu David Oyedepo ni Askofu Mkuu wa kanisa la Living Faith Church ambalo wengi wamezoea kuliita Winners Chapel, katika moja ya mafundisho yake kuhusu Uelekeo wa Kiungu Askofu Oyedepo alitoa ushuhuda wa namna ambavyo eneo yalipo makao makuu ya huduma hiyo lilivyo patikana.

Bishop David Oyedepo
Askofu Oyedepo alisema Mwaka 1991, mtu mmoja  alitupeleka kwenye Motel kubwa yenye apartments zipatazo ishirini na nne, bwawa la kuogelea(swimming pool) pamoja na vitu vingine vingi. Baada ya kuliangalia eneo  hilo nlisimama getini na kumuuliza Mungu “Unasema nini juu ya hili eneo ?” Mungu akanijibu kwa kusema “hili ndilo eneo niliokupa”, baada ya kunijibu hivyo nikafungua macho na kuwaambia watu niliokuwa nimeongozana nao  “Hili ndilo eneo Mungu alilotupa”
Hadi muda huo hatukuwahi kuonana na mmiliki wa eneo hilo wala kuwasiliana nae lakini nilikuwa nimeonana na kuwasiliana na amri jeshi mkuu Mungu mwenye Enzi, na yeye akatupa ishara ya kuendelea mbele kwa kuwa tayari alikwisha tumilikisha.
Baada ya miezi takribani kumi na tatu kwa njia za pekee lile jambo ambalo Mungu alituambia likawa HALISI, mmiliki wa Eneo hilo alitupatia eneo hilo bure pasipo kumpa pesa yeyote, huyo jamaa hakuwa Mshirika wa Kanisa letu, hata hakuwa ameokoka, hatukufanya maombi yeyote ili Mungu atupe eneo hilo, kifupi tulifuata maelekezo ya kauli ya Mungu  kuwa ametupa hilo eneo. Leo hilo Eneo ndio tumeweka makao makuu ya Huduma yetu(Living Faith Church) ambayo imesambaa sehemu nyingi Duniani.
Duniani kote, Sehemu kubwa ya watu waliopoteza uelekeo maishani ni wale wanaofanya mambo ambayo Mungu hajawaambia wafanye, kwa kuwa katika kufanya hilo kunakuwa hakuna msaada wa Mungu na mwisho wa siku unaishia kuwa muhitaji kwa  kuwa utele toka kwa Mungu haupo.
Yesu mwenyewe alifanya mambo Mengi Duniani kwa kuwa Mungu alikuwa upande wake, na hakufanya jambo lolote pasipo kwanza kupata maelekezo toka kwa Mungu {Yohana 5:19-20, 30}.


Faith Tabernacle Church
Eneo yalipojengwa makao makuu ya Huduma hiyo wanapaita Canaan Land na lina ukubwa wa Ekari zipatazo 560 ambazo ni sawa na Kilomita 2.3. Ndani ya Eneo hilo ndipo lilipojengwa kanisa kuu la Huduma hiyo duniani lililopewa jina la Faith Tabernacle church ambalo lina ukubwa wa Ekari zipatazo sabini(70) na hii ni kwa mujibu wa Tovuti ya huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...