Monday, August 1, 2011

JIFUNZE KULINDA NA KULISIMAMIA WAZO LA MUNGU (Part 1)



Maandiko ya msingi: Yeremia 29:11, Isaya 55:8, Ufunuo 17:17

UTANGULIZI:
Maisha (future) ya mtu ni matokeo ya mawazo jumlisha maamuzi anayotekeleza kwenye maisha yake. Matokeo ni kitu kinachozaliwa/kinachofunuliwa. e.g Mpira, mitihani. Kwa hiyo matokeo ni ufunuo. Na kwa hiyo maisha ya mtu ni ufunuo wa mawazo yake na maamuzi yake i.e Maisha ya mtu yanatengenezwa kwa mawazo na maamuzi yake. Mawazo na maamuzi yako yataamua kile utakachozaa/kitakachofunuliwa – Utakachozaa kitaamua future yako na future yako itaamua destiny yako. Maamuzi unayotekeleza yanaweka alama ambayo siyo rahisi kuyafuta.


Ufahamu juu ya nafsi ya mtu
Neno ufunuo (kiroho) – ni udhihirisho wa nafsi ya mtu/shetani/Mungu. Kufunua ni tendo la kudhihirisha nafsi ya mtu/shetani/Mungu. Ndani ya nafsi ya mtu kuna hisia, nia/matakwa na akili. Hivyo kufunua ni kudhihirisha/kuweka wazi hisia (emotions), nia (will), mind (akili/kumbukumbu/uwezo wa kuamua/maamuzi) za mtu husika. Nafsi ya mtu ni kiti cha hisia, nia/matakwa na kumbukumbu zake. 

Kwa lugha nyingine maisha ya nje ya  mtu yanafunua nafsi yake ilikuwa inawaza nini na ikaamua nini.Siku zote maamuzi mabaya yanaleta ugonjwa wa nafsi (soul sickness). Watu wengi ni wagonjwa/wanateseka kwenye maishani/nafsi zao  kwa sababu hawako makini kulinda na kusimamia mawazo/wazo la Mungu juu yao. Kukosa kwao umakini kumewapelekea kuwa na maamuzi mabaya/kujiletea laana kwenye maisha yao na hivyo kuleta ugonjwa kwenye nafsi zao.

Wazo ni mfano wa mimba ndani ya mtu iliyobeba ujumbe maalumu.
Kabla Mungu hajaliachilia wazo ndani ya mtu anakuwa ameshatembea/ameshalitazama hili wazo hadi mwisho wake i.e kiutekelezaji na matokeo yake (Isaya 55:11). Mawazo ambayo Mungu anaachilia ndani ya mtu anayo tayari (Yeremia 29:11). Hata sasa Mungu anaweka wazo kama mimba i.e (Mimba=Wazo) na hiyo mimba imebeba ujumbe maalumu ambao unatakiwa kufanyiwa kazi (Mat 1:18-25). Ndani ya hilo wazo kuna uwepo/nguvu za Mungu (hekima,ufahamu,maarifa,upako) kwa lengo la kukupa majibu ya maombi/maswali yako mbele za Mungu i.e baraka, uponyaji, ulinzi,utajiri, kazi,watoto, mke/mume nk. Majibu ya maombi/maswali ya mtu yapo kwenye mawazo/wazo ambalo Mungu anaachilia kwa mtu huyo.

Reference:

Isaya 55:8-11, v11 says “Ndivyo litakavyokuwa neno langu litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma”. Tafsiri nyingine zimeutafsiri ifuatavyo mstari huo.

NAB – So shall my word be that goes forth from my mouth; It shall not return to me void, but shall do my will, achieving the end for which I sent it.

NLT – It is the same with my word. I send it out, and it always produces fruit. It will accomplish all I want it to, and it will prosper everywhere I send it.

NRSV – so shall my word be that goes out from my mouth; it shall not return to me empty, but it shall accomplish that which I purpose, and succeed in the thing for which I sent it.
Sasa ukiitafakari hiyo mistari kimapana utagundua mwisho wake inatupa picha kwamba neno la Mungu ni wazo la Mungu na wazo la Mungu ndiyo mapenzi yake.

Ufunuo 17:17 ‘Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake
NLT – For God has put a plan into their minds, a plan that will carry out his purposes. They will mutually agree to give their authority to the scarlet beast, and so the words of God will be fulfilled. Tafsiri hii inatuambia Mungu ameweka mpango/wazo ndani yao, wazo/mpango utakaofanikisha/kamilisha kusudi lake.

Hii ina maana hata sasa Mungu anatia/anapanda/anaweka kwenye mioyo/nafsi za watu mipango/mawazo yake ambayo anataka wayatekeleze kwa kuyalinda na kuyasimamia.

Mawazo huingia moyoni na mawazo hutoka moyoni. Reference: Ezekiel 30:10 & Mathayo 15:18.

Ezekieli 30:10 ‘Bwana Mungu asema hivi; Itakuwa katika siku hiyo mawazo yataingia moyoni mwako , nawe utakusudia kusudi baya’. Kusudi lake baya ni matokeo ya namna alivyowaza, yaani kile alichokusudia wakati anawza na sio wazo lililoingia. Reference Zaburi 36:4, 2Samweli 11:1, Mwanzo 6:5-6. Je, wewe unakusudia nini wazo lolote linapoingia ndani yako?
Mithali 20:24Mwenendo wa mtu watoka kwa Bwana’ 


Tafsiri nyingine zinasema;

NLT- How can we understand the road we travel? It is the Lord who directs our steps.
RSV – A man’s steps are ordered by the Lord; how then can man understand his way?
Hii ina maana Mungu ndiye mwenye njia/mwenendo wako kwa hiyo anapokuletea mawazo/wazo ni kwa ajili ya wewe kutembea kwenye njia yako. Zaburi

Kila wazo ambalo Mungu analiweka kwa mtu analiatazama kama mimba. Mimba ni mfano wa nafsi ambayo imebeba kitu ambacho kinatakiwa kudhihirishwa . i.e ndani ya wazo kuna kitu kinatakiwa siku moja kizaliwe.

Siku zote Yesu alilinda na kusimamia  mawazo/mapenzi ya babaye, (John 5:30; 6:38). Yesu aliposema kwenye Yn 4:34 kwamba ‘ Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake” alimaanisha ndani yangu kuna mawazo ya baba nimebebeshwa ambayo ni lazima yatimie. Kwa hiyo neno lake ndio wazo lake na wazo lake ndio mapenzi yake. i.e {neno = wazo = mapenzi ya Mungu}. His word represent his thought, his thought represent his will. Thus his word, his thought, his will.

Mungu alifanya hivyo kipindi cha utumwa wa wana wa Israel, akamweka Musa kuwa wazo la ukombozi, Kipindi cha mateso ya Waisrael akamweka Samson kama wazo la ushindi na maovu yalipozidi akamleta Yesu kama wazo la Wokovu. Hata sasa Mungu anataka kukusaidia kukuondoa kwenye hali uliyo nayo kiroho, kiuchumi, kibiashara, kwenye ndoa, watoto nk. 

Njia kubwa anayotumia ni kukuletea wazo ambalo unawajibika kulilinda na kulisimamia hadi litimie. Je, unakumbuka habari za Mjane wa kipindi cha nabii Elisha – 2 Wafalme 4:1-7. Mungu anayo mawazo mengi positive kwa ajili yako katika kila nyanja ya maisha yako.  Kila aliyebeba wazo/ mimba hiyo ana wajibu mkubwa sana wa kuhakikisha mimba  hiyo inalelewa vizuri hadi itakapozaliwa.

Mambo ya kufanya ili wazo la Mungu ndani yako litimie;
1.Kuwa makini namna unavyolitafsiri/waza/tazama hilo wazo (Ulinzi). 
  • Unalipokeaje wazo, unaliwazaje, unalitafsirije,unalitoaje kama amuzi.
  • Hili ni eneo ambalo unapaswa kuwa makini sana, maana maamuzi yanategemea mawazo yako.    
  • Watu wengi hujutia maamuzi waliyofanya baada ya mabaya kuwakuta tokana na maamuzi waliyoyafanya.
  • Jifunze kulitazama wazo kama mimba/mbegu.
  • Unahitaji uongozi wa Mungu wa kukusaidia katika kufanya maamuzi.
  • Imeandikwa mtiini Mungu, mpingeni Shetani naye atawakimbia. Unatii wazo ndipo unapokuwa na nguvu ya kupinga wazo, maana mfumo wa utendaji ni mawazo.
2. Kuwa makini juu ya maamuzi unayoyatekeleza ( Usimamizi).
  • Kila uamuzi unaoufanya leo unaumba kesho/future yako.
  • Na kila uamuzi unaoufanya unazaa/unafunua kitu fulani (results).
  • Na kila kinachozaliwa (matokeo) kina gharama zake.
  • Mtoto anapozaliwa ndio ufunuo wenyewe, tunajua mwenzetu alibeba nini?
  • Kila wazo ambalo Mungu analiweka kwa mtu, ndani yake kuna uzima na mauti. Reference: Mwanzo 2:16-25(Adam),15:4-7(Abraham), 2Sam 11:1(Daudi), Kumb 30:19, 1Sam15 (Saul), Kumbu 8:11-18, Yn 3:16, Hesabu 20:12(Musa), Wito – Paul anasema nisije nikawahubiri wengine nikawa…, Kumkana Roho Mtakatifu.
  • Sasa ni jukumu lako kuchagua uzima/baraka.
  • Unapochagua uzima maana yake unalinda na kusimamia wazo/kusudi la Mungu litimie. The vice versa is also true.
  • Unapomuasi Mungu na kuamua unavyotaka, ujue unachagua njia ya uharibifu/mauti/laana (a dead end).
  • Mungu anapoliweka wazo ndani ya mtu, matokeo ya lile wazo yapo katika uweza wa mtu na anazitaka mbingu na nchi kuweka record (Deut. 30:19)
  • KJV – “I call heaven and earth to record this day against you, that I have set before you life and death, blessing and cursing: therefore choose life, which both thou and thy seed may live”
  • NLT - Today I have given you the choice between life and death, between blessings and curses. I call on heaven and earth to witness the choice you make. Oh, that you would choose life, that you and your descendants might live
  • Biblia inaposema kum 30:19 ‘uwe hai wewe na uzao wako’, maana yake Mungu anataka unapofanya maamuzi connect future ndani yake.
  • When only God is watching, what kind of choices/decision do we make? He is looking for people He can trust, as He desires to use us in His work.
 NB: Kuwaza ni KULINDA NA Kuamua ni KUSIMAMIA.

Tamati;
Zaburi 50:18-22 inasema ‘Ndivyo ulivyofanya nami nikanyamaza…’ Mungu alinyamaza kwa kuwa moja yeye hana uwezo wa kuamua kwa niaba ya mtu mwingine, kwani suala la kuchagua uzima au mauti ni la mtu binafsi. Natumia fursa kukusihi uwe makini na maamuzi unayofanya kwenye maisha yako kwani mawazo na maamuzi yako yanaumba future yako. Uzima na baraka vipo kwa wale wanaonitii tu.

Unapokuwa kwenye laana ambayo imesababishwa na maamuzi yako, unafanyaje/unatokaje humo ndani?
 Tutaendelea na sehemu ya pili juu ya namna ya kutoka kwenye tatizo kupitia maamuzi uliyoyafanya na yakakufukisha mahali pabaya.


Na: Patrick & Flora Sanga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...