Tuesday, August 23, 2011

Kutana na DOUBLE E Sisters Mabinti wanaofanya Vizuri kwenye Tasnia ya Muziki wa Injili



Evelyn na Esther wanaounda kundi la DOUBLE E Sisters wakiongea mara baada ya kunyakua Tuzo ya KUNDI BORA la Muziki wa injili 2011

Kila kukicha muziki wa kiroho ama wa injili wigo wake umekuwa ukipanuka siku hadi siku, na kupeleka wasanii wa muziki huo kungezeka kila kukicha, kundi la muziki wa injili liitwalo Double E ni moja ya kasi ya zao hilo,Kwa sasa kundi hilo linafanya vyema katika anga za injili nchini Tanzania. Kufanya vyema huko kumepelekea kundi hilo kupata tuzo ya Tanzania Gospel muziki Award kwa kuibuka na tuzo ya kundi Bora la mwaka 2010/2011.


Hosanna Inc imefanikiwa kufanya mahojiano kuhusiana na mambo mbalimbali hususani suala zima la uimbaji wa nyimbo za injili na namna walivyofanikiwa kuinyakua tuzo hiyo na kuacha wengine wakiwa na butwaa.  


Kundi hilo linaundwa na wakina dada wawili ambao ni watoto wa familia moja, Ester na Evelyn Benard, HI  ilianza na Ester ambaye alianza kwa kueleza kuwa yeye Ester Benald Kingo alizaliwa miaka 21 katika hospital ya Mount Meru mkoani Arusha na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya uhuru iliyopo Arusha na sekondari akajiunga Kenton secondary School iliyopo jijini Dar es saalam na baadae akaenda nchini Uganda akajiunga na shule ya `Nai High School;

DOUBLE E SISTERS Wakipokea TUZO pale Diamond Jubelee mapema mwaka huu

Kwa upande wa Eveline Benald Kingo ambaye ni dada yake Ester yeye alizaliwa miaka 24 iliyopita jijini Dar es salaam, na kupata elimu yake jijini Dar es salaam na baadae mjini Arusha na kwenda nchini Uganda.

Akieleza jinsi walivyoanzisha kundi lao la Double E, Ester ansema kuwa kundi hilo limetokana na yeye mwenyewe kwa vile alikuwa anapenda sana kuimba na kujikuta akimuambukiza dada yake, hivyo ikapelekea wao kuamua kuunda kundi  hilo lilijulikana kwa jina la Double E, yaani Ester na Eveline.

‘‘Namshukuru sana Mungu kwa kutufikisha hapa tulipo kwa sababu yeye ndiye aliyekusudia kundi letu liwepo, kiufupi mimi nilikuwa napenda kuimba tangu nilikuwa na miaka saba, wakati huo nilikuwa naimba Sunday school na baadaye nikaendelea na kuanza kutunga tunga nikaona ni vyema nimshirikishe na dada yangu ambaye kweli alikubali na kujikuta tukifanya pamoja,’’anasema Ester.
  
Kwa upande wa Eveline ambaye yeye ni mkubwa, anasema kwanza anammshukuru Mungu kwa namna ambavyo kundi lao limefanikiwa kupokelewa vyema ndani ya jamii na kujikuta likipata mafanikio kila kukicha, Eveline anaongeza kuwa mdogo wake ndiye aliyepelekea yeye aingie kwenye fani ya kuimba, na kweli alibaini kuwa hana namna hivyo aliingia kwenye fani ya uimbaji na kufanya vyema.

Evelyn na Esther wakiwa na Mama yao mzazi ambaye ni mzee wa kanisa katika kanisa la Eagt Mito ya Baraka
Double  E wenye ndoto ya kuwa na studio yao ya kurekodi Video na Audio, pia ni wanafunzi wa kozi ya IT . Evelyn aliiambia Hosanna Inc kuwa moja kati ya changamoto kubwa waliokutana nayo ni kukatishwa Tamaa, alisema wengi waliwaambia kuwa nyie hamuwezi kuimba labda mjaribu kitu kingine lakini kwa kuwa walimjua wanayemtumikia hivyo hawakukata tamaa.


Mpaka sasa kundi hilo la Double E, limefanikiwa kutoa albamu yao ya Kwanza iitwayo NAPAMBANA na inafanya vyema katika soko la mziki wa injili, Album hiyo inajumuisha nyimbo zipatazo 10 ikiwemo `Napambana, it`s over, Yesu yupo, Umeniumba, Natangaza, yatima, pamoja na `Wamtumainio Bwana ambazo zote wameziekodi studio ya Baucha iliyoko maeneo ya stesheni jijini Dar es salaam. Mpaka sasa Double E wamefanikiwa kurekodi video ya wimbo wao uitwao `Napambana` unaofanya vyema katika muziki wa injili.

Kushoto ni Evelyn Benard na kulia kwake ni Esther Benard
 Kwa sasa wanajiandaa kurekodi albamu ya pili ambayo wamekwisha ikamilisha, wanasema kuwa wanatarajia ifikapo mwishoni mwa mwaka huu itakuwa tayari iko sokoni. Mabinti hawa wameshirikishwa katika nyimbo za wanamuziki mbalimbali akiwemo Anaclara pamoja na Flora Okevo, pia wameingiza sauti katika wimbo uitwao Umenichagua uliomo katika album mpya ya Mtumishi Emmanuel Mgaya.

Wanamuziki hao wametoa ujumbe kwa waimbaji wenzao kuwa wasonge mbele kihuduma na wajitahidi  kuwasaidia waimbaji wachanga wanaochipukia ili nao waweze kusonga mbele zaidi, aidha walimalizia kwa kutoa shukrani kwa familia yao ambayo imekuwa ikiwapa sapoti kubwa na pia kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao wamekuwa nao bega kwa bega kuhakikisha wanatimiza ndoto zao katika uimbaji. 



Their Favorite Gospel Group: Marry Marry
Best Hymn: Chakutumaini Sina
Favorite Bible Verse: Methew 18:18-20
Their Favorite Gospel Artist: Ephraim Sekeleti
Favorite Colour: Chocolate


Uskose kufuatilia Hosanna Inc jumanne ijayo tutakuwa na mtumishi wa Mungu Denis Massawe Mtanzania afanyaye huduma nchini  Uingereza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...