Saturday, August 20, 2011

Mch Zachery Tim akutwa amekufa Hotelini jijini New York


Mch Zachery Tim
Mchungaji na mwanzilishi wa huduma ya New Destiny Christian Center (NDCC) iliyoko katika jimbo la Orlando jijini Florida nchini MarekaniZachery Tim(42) amekutwa amekufa ijumaa iliyopita chumbani kwake katika Hotel aliyofikia jijini New York iitwayo W Hotel, mfanyakazi mmoja wa Usafi katika hotel hiyo ndiye aliyeukuta Mwili wa Mch Tim ukiwa sakafuni katika chumba chake.

Mpaka sasa haijajulikana wazi ni sababu gani zilizopelekea kifo chake japokuwa polisi  wanadai hakuna dalili zozote za kiharifu kuwa Mch Tim aliuwawa ingawa bado wanaendelea na  uchunguzi. Mchungaji Zachery Tim ameacha mke ambaye alikuwa ametalikiana nae pamoja na watoto wane.

Kabla hajaokoka Mch Tim alipitia katika misukosuko mingi ya maisha ambapo alikuwa mtumiaji wa Madawa ya Kulevya  na alijiingiza katika magenge mbalimbali ya uharifu. Baada ya kuokoa na kuitwa kwenye huduma Mch Tim alijenga centre  kubwa ya Vijana kwa ajili ya kuwatibu walioathirika na madawa ya kulevya pamoja na kutoa ushauri mbalimbali, centre hiyo ina ukubwa wa kilometa za mraba zipatazo 34000.
Mch Zachery Tim na Mkewe
Hakuishia hapo alifanikiwa kuchukua Masters mbili moja ikiwamo ya masomo ya uhasibu  kutoka katika Towson State University, na nyingine ya Theolojia kutoka Maranatha Bible College na alipewa digrii mbili za uzamivu(Udaktari wa Heshima PHD) Kutoka  Vision International University, na nyingine kutoka  St Thomas Christian University kwa kazi kubwa aliyofanya katika utumishi wake mbele za  Mungu.

Mch Tim alianza huduma mnamo mwaka 1996 akiwa na watu sita tu ambapo hadi sasa kanisa lake lina zaidi ya washirika elfu nane(8000) huku  ibada zake za jumapili zikionyeshwa zaidi ya nchi mia moja duniani kupitia Television na Radio mbalimbali huku mara kadhaa aliitwa nakufundisha katika kituo cha television cha TRINITY BROADCASTING NETWORK (TBN).

Watumishi mbalimbali kupitia Twitter na Facebook wameonyesha kusikitishwa na kifo cha mchungaji huyo mashuhuri.Fuatana nasi usome comments za watumishi mbalimbali kutoka katika Page zao za Twitter na Facebook.

Dr Jamaal Harrison Bryant
JAMAL BRYANT:pastor of Empowerment Temple in Baltimore, Md., wrote on Twitter: “Dear Lord today bless the children, congregation & colleagues of Dr Zachery Tims. Cast off sorrow & help us celebrate!”

BISHOP T.D. JAKES Through Twitter wrote: "DEEPLY saddened to hear of the passing of Pastor Tims @ztims ...praying for his family and church."

Cece Winans
GOSPEL SINGER CECE WINANS : called on her Twitter followers to "send up prayers" for the family and congregation of Pastor Tims, writing: "My heart is saddened by the passing away of my brother, Pastor Zachery Tims! May the God comfort, strengthen, heal and bless his family and congregation. Let's all send up prayers..." 


EV PAULA WHITE: also expressed remorse on losing Tims on her Facebook page:
Ev Paula White
Today my heart is grieved over the loss of my spiritual son and long time friend and associate, Pastor Zachery Tims. While words are difficult for me to find during this time of loss, I honor the great work he has done for the kingdom of God and pray for every family member, friend, associate and the incredible congregation of New Destiny. 

The Bible says that we mourn with those that mourn and rejoice with those that rejoice. As the family of God we walk through this together...


1 comment:

  1. Kama kawaida ya "Walokole" hawa wa kujifanya. Huyu aliachana na mkewe mwaka 1999 baada ya kukiri kuwa alikuwa ana uhusiano wa kimapenzi na "stripper" kwa mwaka mzima.

    Halafu inasemekana alikuwa na madawa ya kulevya alipofariki hotelini. Just sad kwa watu hawa wanaojifanya watakatifu kumbe ni kudanganya watu ili watajirike.

    http://blogs.wsj.com/metropolis/2011/08/15/no-answers-in-death-of-florida-pastor-in-times-square-hotel/

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...