Friday, August 26, 2011

Baba yake Mwl Christopher Mwakasege Afariki Dunia


Mwl Christopher Mwakasege
Zikiwa zimebaki siku tisa kabla  Mwl Mwakasege aanze Semina katika Viwanja Vya Biafra jijini Da es salaam,  Mwl C. Mwakasege amempoteza Baba yake Mzazi Siku Ya leo.

Taarifa ambazo Blog Imezipata na kuthibitishwa na Mmoja wa Karibu na Familia ya Mwl Mwakasege ameihakikishia Bloga kuwa Mzee Mwakasege amefariki siku ya leo tarehe 25/08/2011 katika Hospital Ya Hindu Mandal baada ya kulazwa hospitalini hapo kwa muda wa wiki mbili baada ya kupata matatizo yaliyopelekea mzee huyo kupata ugonjwa kama Stroke.

 Chanzo hicho kimeeleza kuwa taratibu za Msiba kwa Dar-es-Salaama zitafanyika Mbezi na Kisha safari ya Kuelekea Mbeya itafuata.
 Taarifa zaidi zitatumwa hapa Mbezi ipi, Mbezi sehemu gani saa ngapi na mpango mzima wa kufika huko.

Bwana alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake na Libarikiwe. Blog itakujuza mengi.

Source: Sampapaa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...