Saturday, August 13, 2011

Riot Concert kuweka Historia Nchini



Righteous Invasion of Truth { RIOT} ni huduma iliyoko hapa nchini yenye lengo la kuwafikia vijana na Kwa Neno la Mungu. Riot mnamo tarehe 20/08/2011 ambayo itakuwa ni ijumaa ijayo itakuwa ikizinduliwa Rasmi pale Mlimani City ambapo kesho yake Tarehe 21 August 2011 itakuwa ni siku maalumu ya Tamasha lenyewe lililopewa jina la Tshirt & Jeans Gospel Concert litakalofanyika Kiramu Hall Mbezi kuanzia saa Tisa mchana.

Katika siku hiyo ya Jumamosi makundi mengi ya vijana kutoka ndani na nje ya Tanzania yatakuwa yakimtukuza Mungu.Kutoka nchini Tanzania Shekinah Dancers, Door Keepers, Wambura and The 12, Bushando  pamoja na kundi maarufu la Gospel Hip hop linaloundwa na Gee and Seth litapanda jukwaani.

Gee na Seth wakighani hawa Broz  watakuwepo
Shekinah Dancers kutoka Tanzania nao watapanda jukwaani
kutoka Uganda ni GODs Army,Mass Choir pamoja na Soul 5.Kutoka nchini Kenya watakuwepo Wernono Family, Dj Tourch, Bupe, The Saint huku kutoka nchini Zambia atakuwepo Ephraimu Sekeleti na Kundi lake pamoja na  Prince Kennedy.
Kwenye Tantable Kwa habari ya Mixing na kila kitu Dj Touch from Kenya atasimamia show

GODS ARMY Kutoka Uganda
Kwa muda mrefu Gospel Music Industry ya Tanzania imekuwa ikienda kwa mfumo ule ule pasipo mabadiliko, nikimaanisha uimbaji wa nyimbo zinazoaminika kuwa ni za vijana umekuwa mgumu au haupenyi kabisa kwenye akili za wengi. Wapo ambao hawaamini kama Hip hop, Ragga(Danceall), vinaweza kuimbwa madhabahuni.

Ephraimu Sekeleti Kutoka Zambia pamoja na kundi lake wataimba siku hiyo
Hakuna safari isiyokuwa na mwisho, Riot wamekuja wakitumia nyimbo na staili zinazowagusa vijana kama ulimbo wa kuwaleta vijana hao kwa Kristo. Imekuwa ni kawaida kusikia tunafanya Revolution kwenye Muziki wa Injili na wengi wamekiri hivyo lakini kwa ujio huu wa Riot ni Alama Tosha kuwa wameamua kuleta mabadiliko kwenye Muziki wa Injili nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...