Wednesday, December 29, 2010

Haki Miliki kwenye Nyimbo za Injili

                                  
Moja ya makusudi ya Haki miliki kwenye nyimbo ni pamoja na kulinda nyimbo hizo zisisambazwe, kuimbwa wala kutumiwa na mtu mwingine hadi kwa makubaliano maalumu na mtungaji au muimbaji wake wa kwanza.  Na makubaliano hayo zaidi hulenga kwenye malipo ya pesa. Mtu akiimba, kusambaza au kutumia nyimbo kwa namna inayokiuka sheria za Haki miliki hatua ambazo huchukuliwa ni pamoja na kushitakiwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Je, ni sahihi kwa nyimbo za Injili, zikiwemo za kumsifu na kumwabudu Mungu, kuwekewa Haki miliki?

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...