Tuesday, November 20, 2012

Historia ya Mwanamuziki Donnie Mcclurckin

Pastor Donnie Mcclurkin
Donnie Mc Clurkin ni Mwanamuziki Mashuhuri wa nyimbo za Injili na Mchungaji wa Kanisa la Perfecting Faith church lililo katika jimbo la Detroit nchini Marekani.

Donnie alizaliwa na Familia ya Bw Donald Sr na Mama Frances Mcclurkin mnamo Jan 25 mwaka 1959 na kukulia katika mji wa Louisville. Akiwa na umri wa miaka nane(8), mdogo wake wa kiume mwenye miaka miwili(2) aligongwa na gari na kufa papo hapo huku Donnie akishuhudia.Wakati Donne akiwa na majonzi mazito usiku huo huo ambao walimzika mdogo wake, mjomba wake alimbaka Donne.


Baada ya kifo hicho familia yake iliingia kwenye mgogoro kubwa ambao ulitokana na utumiaji wa dawa za kulevya. Baada ya kufikisha miaka 13, binamu yake mtoto wa mjomba wake alimbaka Donnie pamoja na dada zake wawili kitendo amabacho kilimuumiza sana na kumuachiia kovu la aina yake. Muda wote alijiona mkosaji, mtu aliyekandamizwa na hakuwa na ujasiri mbele za watu na mwenye wingi wa aibu.

Kwa kipindi hicho chote alipata Faraja toka kwa shangazi yake ambaye alikuwa muimbaji wa nyimbo za Injili. Shangazi yake huyo alimfanya Donnie ajiingize kanisani na kuanza kupiga piano na kuimba kwaya kama sehemu ya kufuta machungu na kuondokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao. Mama yake mzazi naye alikuwa muimbaji kanisani hivyo kanisani kukawa ndio nyumbani kwake na kambi yake pindi nyumbani kukitokea matatizo.

Tarehe 14 Julai 1969 akiwa na miaka takribani kumi(10) ikiwa ni siku ya jumapili akiwa kanisani  huko Amityville Gospel Tabernacle mtumishi wa Mungu aliyekuwa akihubiri aliwaambia watu kuwa “KRISTO ALIKUFA KWA SABABU ANAKUPENDA” wazo hili hilo ndilo lilikuwa kwa Mcclurkin ndipo akaamua kuyakabidhi maisha yake kwa Yesu. Kwenye kitabu alichoandika kuhusu maisha yake alisema “ Kanisa limekuwa ndio ulimwengu wangu mahali ambapo najisikia Amani na najisikia kama ndio Mahali Pangu halisi”Mwaka 1971 wakati anamiaka 11, alikuwa akimpenda sana mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za injili kipindi hicho aliyeitwa Anre Crouch. Siku aliposikia kua Crouch anakuja katika jimbo lao alimuomba mama yake ruhusa waende kwenye tamasha na kumuahidi jumatatu yake ataamka mapema na kwenda shule kama kawaida. Mama yake alikubali na wakaenda Tamashani na Donnie akaenda kukaa mbele kabisa sambamba na mamaye.

Baada ya Crouch kuingia ukumbini saa tano usiku kabla hajaanza kuimba alimuona Donnie na kumfata, Donnie anasema, Crouch akaniuliza kitu gain unafanya hapa, nkamjibu nakusubiri wewe!!, akaniuliza kama nimelipenda Tamasha nkamjibu ndio, akanambia wakati yuko mdogo hakuweza kuimba wala kucheza mpaka baba yake alipomuobea. Nkamjibu baba yangu hajaokoka hivyo hawezi kuniombea. Mwishoni akaniuliza kama nitapenda aniombee nami nkamkubalia. Akaweka mkono wake kichwani kwangu akasema “Mungu mpe kile ambacho umenipa mimi” kisha akaelekea stejini. Huo ulikuwa ndio mwanzo wa hiki nlichonacho leo.

Akiwa kanisani hapo alianzisha kundi llilokuwa linajulikana kama The Mcclurkin Singers na baadaye alianzisha kundi lililokuwa likijulikana kama The New York Restoration Choir. Mwaka 1983 wakati akiendelea kutumika na kwaya alikutana na Pastor Marvin Winans. Mch Winans alivutiwa sana na namna Donnie alivyokuwa akiimba kwenye semina ya injili.

Baadaye Mch Winans alimwalika Mcclurkin katika mji wa Detroit alikokua akiishi ili kumsaidia kuanzisha huduma(kanisa) liitwalo Perfecting Faith Church.Miaka sita baadaye(1989)  Donnie aliamua kuhamia Detroit na kuanza kufanya kazi na Pastor Winans. Katika kipindi hiki ndipo Mcclurkin alipata wasaa wa kuzunguka sehemu mbalimbali na kufanya huduma akiwa chini ya pastor Winans. Donnie anasema Familia ya Winans imekuwa karibu sana nay eye Kuanzia Bebe, Cece, na Pastor Marvin na wakat mwingine anafkiri yeye ni Donnie Mcclurkin Winans.

Donnie Mcclurkin na Cece Winans wakiwa wameshikilia tuzo za Trumpert awards walizopewa mwaka 2007
Mwaka 1991 alikuwa hajiskii vizuri kiafya, hivyo alienda Hospitali, walipompima walimwambia kuwa anaugonjwa wa Leukemia(kansa ya damu), na madaktari wakamwambia unahitaji matibabu ya haraka. Akawambia naombeni mnipe siku 60 ili nkaongee na Baba yangu(Mungu). Nkawasiliana na Pastor Andre Crouch naye akamshirikisha baba yake ambaye kwa muda huo alikuwa Askofu jijini Califonia. Wakaomba nami nkaomba Leukemia ikaondoka, madaktari waliponipima tena hawakuikuta tena kansa mpaka leo Kristo amenipomya anasema Donnie.

Akiwa na Pastor Winans, alisaini mkataba na kurekodi album yake iliyoitwa LP, Album hiyo iliyokuwa na nyimbo kama Stand iliyongoza kwa umaarufu na kuzinduliwa na Oprah Winfrey. Nyimbo hii ilitunukiwa tuzo ya Grammy kwa mwaka huo wa 1996 kwa upande wa nyimbo za Injili. Album z\ake tatu za solo zilikamata nafasi za juu sana kwenye chati za Bilboard.

Akiwa na furaha ya ajabu Mcclurkin kupitia makongamano mbalimbali huwasimulia watu ukweli wa maisha yake huku akipinga kwa nguvu mahusiano ya jinsia moja. Mcclurkin anaamini kwamba suala la Homosexuality ni suala la kiroho haliwezi tibika kisaikolojia na linahitaji msaada wa Mungu pekee. Baada ya watu wengi kuwa wanamuomba aelezee historia ya maisha yake, Mcclurkin aliamua kurudi nyumbani kwao Amityville New York na kumuomba Mama yake ruhusa ili aandike kitabu kuhusu maisha yake.


Frances Mcclurkin (mamaye), alimruhusu Donnie aandike kitabu kinachoyaelezea maisha yake kinaga ubaga, ndipo Mcclurkin akatumia  miezi 18 kuandika kitabu hicho ambacho alikiita ETERNAL VICTIM, EXTERNAL VICTOR. Alisema aliamua kuandika kitabu sio kwa kusudi la kuweka wazi uovu uliokuwa ukifanyika ndani ya Familia yao bali kwa sababu yeye ni Mwalimu, na mwalimu ni vizuri ajitoe yeye kama ujumbe ili watu wengine wajue kuwa hawako peke yao kwenye mambo wanayopitia.

Mwaka 2008 Mcclurkin alichaguliwa kuwa miongoni mwa wanamuziki ambao watakuwa kwenye timu ya Barak Obama katika harakati za uchaguzi wa nchini Marekani. Mcclurkin alikubali na kujumuika na Barak Obama, lakini kutokana na msimamo wake wa kupinga mahusiano ya jinsia moja, Mashoga wengi walipinga kuwepo kwake kwenye timu ya Obama. Hivyo ili kupata kura za mashoga ilibidi Mcclurkin atolewe kwenye orodha hiyo ingawa alifanikiwa kuimba kwenye moja ya kampeni za Rais Obama.

Mcclurkin, Nofle pamoja na Mary Mary wakiwa na Rais G. Bush

Tukutane jumanne ijayo ili uone tumekuandalia nini cha kukujenga kupitia maisha na changamoto za watumishi wa Mungu mbalimbali wanazo kutana nazo katika maisha .

Saturday, November 17, 2012

Hafla ya Kuchangia maandalizi ya Usiku wa Kusifu na Kuabudu yafanyika Peacok Hotel


Paul Mwangosi wa pili akiimba sambamba na marehemu Fanuel Sedekia

Tanzania Praise and Worship Team ni kundi la kusifu na kuabudu linaloongozwa na Mtumishi wa Mungu Paul Mwangosi.Dhumuni kubwa la uwepo wa Kundi hili ni kumwabudu MUNGU katika ROHO na KWELI.Mnamo mwaka 2008 mmbeba maono wa Kundi hili mtumishi Mwangosi ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akihudumu kama kiongozi wa kusifu na kuabudu katika semina za Mwl Christopher Mwakasege alipata maono ya kuanzisha Kundi litakalokuwa likimsifu Mungu kwa namna ya kipekee.

Ilipofika mwaka 2011 Mtumishi Mwangosi aliwaita marafiki na jamaa kisha akawashirikisha maono yake, Maono hayo yalipokelewa vizuri ndipo ikaundwa kamati maalumu ya kuhakikisha maono hayo ya kuwa na BAND na KUWA NA SIKU MAALUMU ambayo nchi nzima itakuwa ikimsifu na kumuabudu Mungu yanatimia nah ii itaanzia jijini Dar es Salaam na kusambaa mikoa yote. Kwa kuanza mwaka jana 2011 ulifanyika Mkesha ule usiku wa kuamkia siku ya kuadhimisha miaka 50 ya Tanzania, mkesha huu ulifanyika katika kanisa la City Christian Centre(CCC) na kuanzia hapo maono hayo yaliendelea

Kwa Mwaka huu wa 2012 tukio hili litafanyika usiku katika kanisa la City Christian Centre(CCC-Upanga) mnamo tarehe 7-11-2012 ambapo waimbaji mbali mbali wa hapa nchini watahudumu kwa lengo moja tu la kumpatia Mungu Ibada.
Kwa kuwa maandalizi ya mkesha huo yanahitaji pesa, kamati nzima inayoratibu mkesha huon iliyo chini ya Mtumishi Emmanuel Kwayu, iliamua kuandaa Chakula Maalumu kilichoambatana na Harambee.Hafla hii nzima ilifanyika usiku wa jana tarehe 16/11/2012 kuanzia saa 2: 00usiku mpaka saa 4: 00 usiku katika hotel ya Peacok jijini Dar es salaam ambapo watu walijumuika pamoja wakiongozwa na Band ya Tanzania Praise and Worship team.

Hapa chini ni sehemu ya matukio ya hafla hiyo na jipange kuhudhuria siku hiyo
 7-11-2012 kwani ni siku ya kihistoria.

Ukumbi ukiwa tayari kwa Hafla

Shangwe

No Coment

Audience ikienda sawana Praise Team

Simon Jengo Mratibu wa Kamati akieleza jambo katika hafla hiyo

Tanzania Praise and Worship Team Ikihudumu

Tumbo ni Kwa Chakula, na  Chakula ni kwa Tumbo, that is Biblical

Bloggers

Angalia Praise Team Ikihudumu Siku ya Jana

Friday, November 16, 2012

R.I.O.T Presents Men's Conference from 19-25/Nov/2012 in Dar es Salaam
Righteous Invasion of Truth (R.I.O.T) gladly brings ‘Men of Valor’, its first men’s conference in Dar es Salaam. M.O.V. is an interactive platform, reaching out to men across different ethnic groups, socio-economic and religious backgrounds to restore, transform, equip and edify the man holistically.

Men have a natural tendency of internalizing issues. When you ask a man what he is thinking when things are up to his neck, without a glance, he’ll instinctively say, “Nothing”. Men do cry, but their tears are only visible from the inside. That’s why God had to say, “It is not good for a man to be alone”. As much as studies show that women are twice as much susceptible to depression, surprisingly the male-to-female ratio for completed suicides is greater than 4:1

When in this state where the internalization of things has reached its limit, men tend to shift the blame for how they feel on the inside to outside things. We exhibit anger or irritability over everything. Men are more prone to using alcohol or drugs as an outlet. As if this isn’t enough, the male infant has a higher mortality rate than the female. Let alone the fact that the woman has a higher life expectancy rate.

To those that have overcome these obstacles, there is still no rest for them. The enemy has strategically planned to emasculate the ‘man’ figure from marriage, family and even the society at large. The ‘man’ as an authority figure is being undermined from his God-given position bestowed upon him from Genesis by God Himself.

How can men prevail this ongoing fierce battle?  If only we could learn the greatest ‘Art of War’ –PRAISE!  You might be the least in your father’s house or perhaps you are coming from the poorest family in your clan, but I clearly hear the Commander-in-Chief of the Army of The Lord saying this to you: “Jehovah is with you, Mighty Man of Valor”!

The Event will be conducted at Makumbusho Hall near Institute of Finance(IFM)
From 19th-25/Nov/2012
Time:5;30Pm - 8:30Pm
We welcome you all Men and Women

Thursday, November 15, 2012

Package From Altar:Namna Mwanamke Anavyoweza Kutumia Nafasi Zake Kubadilisha Maisha Ya Ndoa Yake (1) 
Mithali 14: 1 ‘Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’.

Mchungaji mmoja rafiki yangu aliniambia asilimia hamsini mpaka sabini ya changamoto au matatizo anayoshughulika nayo mara kwa mara katika kanisa lake ni ya wanandoa. Kwa lugha nyepesi asilimia 50 – 70 ni matatizo yatokanayo au yanayohusiana na ndoa. Binafsi pia kwa upande wangu kupitia nafasi yangu katika mwili wa Kristo, email za wasomaji ninazopata na pia baadhi ya semina za ndoa ambazo nimefanya kuhusu eneo hili nimegundua kwa hakika ndoa nyingi za wana wa Mungu zina shida na wao hawajajua kwamba vita hii inatoka kwa Shetani, maana anajua ndoa zikitengamaa ni faida kwa ufalme wa Mungu na ni uharibifu kwenye ufalme wake wa giza. Naam anapigana usiku na mchana ili kuhakikisha ndoa hazitengamai kwa kuleta fujo za kila aina.

Kila siku katika ndoa kuna changamoto zinazaliwa mpaka imefika mahala baadhi ya wanandoa wanawaza kwa nini walikubali kuoa au kuolewa. Kwa hakika laiti Biblia ingetoa mwanya kwa wanandoa kuachana basi kuna baadhi ya wanandoa wangehakikisha wanaitumia hiyo nafasi vizuri kwa kuwa ndoa zimegeuka ndoano. Matarajio ambayo kila mmoja alikuwa nayo kwenye ndoa anaona hayatimii. Kinachosumbua watu wengi ni kwamba kabla hawajaonana hawakujua nini kinakuja kupitia ndoa, hawakuweza kuona uhalisia wa maisha ya ndoa utakuwaje? Bali kila mmoja alikuwa na mtazamo/fikra na matarajio yake binafsi juu ya ndoa yake.Naam zipo sababu nyingi sana zinazopelekea matatizo au changamoto kwa wanandoa. Katika somo hili nitaandika zaidi zile zinazotokana na upinzani kutoka kwa Shetani ili kuathiri kusudi la Mungu. Lengo la ujumbe huu ni kukufundisha wewe mama (Mwanandoa) namna ya kuzitumia ‘nafasi’ ambazo Mungu amekupa Kibiblia ili kuiponya ndoa yako au kubadilisha hali ya sasa ya ndoa yako endapo unaona si ile ambayo Mungu amekusudia.

Kwa nini Mwanamke?
Pengine utaniuliza kwa nini mwanamke ndiye awajibike katika kuponya au kubadilisha maisha ya ndoa yake? Binafsi katika kuisoma Biblia nimegundua kwamba kwa kuzingatia nafasi ambazo mwanamke amepewa kibiblia ni ishara ya kwamba kwa habari ya  ndoa, Mwanamke ana nafasi kubwa ya kuijenga au kuibomoa ndoa yake na hivyo nyumba yake kwa ujumla. Mara kwa mara Mungu ananifundisha masuala ya wanawake, suala la wanawake kuwa kwenye ‘nafasi zao’ husisitizwa sana.

Kwa nini nafasi?
Sijui kama unafahamu maana ya nafasi ambayo Mungu anampa mtu katika ulimwengu wa roho. Hizi ni nafasi ambazo Mungu amekupa wewe mawanamke katika ulimwengu wa roho ili uzitumie kufanikisha kusudi lake kupitia ndoa yako. Nafasi (position) ni eneo ambalo mtu anapaswa kuwepo kwa kuhusianisha na vitu au watu wengine, naam ni wadhifa ambao mtu anakuwa nao kwa kuhusianisha na mtu au watu wengine.

Kwa hiyo hizi ni nafasi ambazo Mungu amempa mwanamke zikihusiana na mwanaume katika kilitumika kusudi la Mungu hapa duniani. Mwanamke anapokuwa amesimama katika nafasi zake ndipo anapoweza kuruhusu mawazo ya Mungu kupitia ndoa yake kutimia naam ndivyo anavyoweza kuzuia mawazo ya Iblisi kupitia ndoa yake yasitimie. Naam nafasi ya mwanamke katika ndoa ndiyo inayoamua uzima au mauti ya ndoa yake, nafasi ndiyo inayopelekea kufanikiwa au kufeli kwa ndoa yake, nafasi ya mwanamke katika ndoa ndio inayoamua nini kingie au kitoke kwenye ndoa.
Katika kusoma kwangu Biblia nimegundua kwamba Mungu amempa nafasi zifuatazo mwanamke;
  • Mwanamke kama ‘msaidizi’ wa mumewe
  • Mwanamke kama ‘mlinzi’ wa mwanaume
  • Mwanamke kama ‘mjenzi’ wa nyumba yake
  • Mwanamke kama ‘mshauri’ wa mumewe
  • Mwanamke kama ‘mleta kibali’ kwa mumewe
Naam kutokana na changamoto zinazoendelea katika ndoa mbalimbali nimelazimika kuanza kuandaa mfululizo huu wa namna mwanamke anavyoweza kusimama kwenye nafasi zake na kuiponya ndoa yake. Jukumu langu kubwa itakuwa ni kufafanua kila nafasi ambayo mwanamke amepewa na namna anavyoweza kuitumia hiyo nafasi kubadilisha ndoa yake ambayo anaona inaangamia.

Somo litaendelea alhamis Ijayo

Mwl Patric Sanga 0715-816800

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...