Tuesday, February 8, 2011

HISTORIA YA MWANAMUZIKI DONNIE MOEN

Don  Moen Worshiping GOD
Don moen ni muimbaji na mtunzi wa mashairi ya injili aliezaliwa tarehe 29 june 1950 huko Minneapolis Minnesota nchini Marekani. Don alifahamika baada ya kutoa album aliyoipa jina lake la Worship with Don Moen mwaka 1992. Album hiyo iliuza zaidi ya nakala milioni tano na kumfanya Don  kuwa kwenye orodha ya waimbaji waliouza zaidi nchini Marekani.

Alifanya kazi na Integrity records kwa miaka 20 akiwa kama mbunifu mkuu wa integrity music na rais wa integrity lebel. Aliachana na integrity records mwaka jana(2008) na kuanzisha kampuni yake ya The Don Moen Company. Kampuni hiyo imempatia Don tuzo ya Dove mwaka huu huku akiwa na tuzo zingine tisa alizozipata kwa kazi ya muziki. Akiwa kama mtunzi wa mashairi amewatungia waimbaji wengi kama; Claire Cloninger, Paul Overstreet, Martin J. Nystrom, Randy Rothwell, Ron Kenoly, Bob Fitts, Debbye Graafsma, Paul Baloche na Tom Brooks.
Arise is the One among of his album
Album ya Hossana give thanks ilikuwa album bora ya label ya intergrity, album hiyo ilifuatiwa na album nyingine mbili  zilizozofanya vizuri, En tu Presencia and Trono de Gracia ambazo alizitua kwa lugha ya kispaniola. Akiwa kwenye ziara barani Asia mwaka 1999 alirekodi singo ya The Mercy seat kwenye uwanja wa michezo wa Singapore nchini Malaysia na Heal our land akiwa Yodo park nchini Korea Kusini mwaka 2000.

God will give way(the best of don moen) ilitolewa mwaka 2003, wimbo uliobeba album hiyo wa God will give Way aliutoa maalum kwa ajili ya dada yake na mumewe ambao walimpoteza mtoto wao wa kwanza kwenye ajali mbaya ya gari huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya. Don anatarijiwa kutoa album ya I belive there is Way ambayo itakuwa ya mwisho kufanywa na Integrity records. Don ametoa Album zaidi ya album 20 baadhi ya album hizo ni;

.Give Thanks
.Steadfast Love
.Bless the Lord
.Christmas
.Eternal God
.Worship with Don Moen
.God with Us
.Trust in the Lord – Live Worship with Don Moen
.Rivers of Joy
.Emmanuel Has Come
.Praise with Don Moen

TUZO

Baadhi ya tuzo alizoshinda nipamoja na hizi zifuatazo
Ameshinda tuzo za Dove mara tisa
1994-Album bora ya mwaka “God with Us”
Dove Awards
1992-Wimbo bora wa mwaka “God Will Make A Way”
1993-Album bora ya mwaka “Worship with Don Moen”
1995-Wimbo bora wa mwaka “Mighty Cross”
1998-Wimbo bora wa mwaka “Emmanuel Has Come”
1999 -Album bora ya mwaka “God for Us“
2001-Album bora ya kispaniola ya mwaka “En Tú Presencia”
2003-Record bora ya country ya mwaka “God Is Good All The Time”
2004-Album bora ya kispaniola ya mwaka “Trono de Gracia” 
 
Don kwa sasa anaishi Alabama nchini Maekani pamoja na mkewe Laura na watoto wao watano.

1 comment:

  1. Ninnampenda sana nyimbo za kuabudu za huyu mwimbaji Don Moen,ambazo kiukweli anaimba kwa upako sana.Mungu ambariki na huduma iguse maisha na roho za watu,yamkini ifanye mabadiliko.AMEN.
    Natamani kupatra parckage yake yote ya nyimbo zake ila ,sijui ni jinsi gani ya kupata kwa pamoja.
    Wilson Shoo.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...