Sunday, February 12, 2012

Changers Conference ilivyogusa fahamu za Vijana jijini Mwanza


Mnamo tarehe 12-01-2012  Kanisa la Mwanza International Community Church[MICC] liliandaa kongamano kubwa maalumu la vijana lililopewa jina la “Changer Conference”.Kongamano hilo lililokuwa na lengo la kuamsha morali ndani ya vijana ili kuleta mabadiliko nchini lilifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Crest.Vijana kutoka sehemu mbalimbali na wa dini zote walihudhuria ikiwemo wanachuo kutoka Saint Augustine University(SAUT), Bugando University, CBE-Mwanza Campus pamoja na wanachuo wa chuo cha Uchungaji cha PAG Makongoro .

Wasemaji wakuu katika kongamano hilo walikuwa Mchungaji kiongozi wa kanisa la MICC Pastor Zakayo Nzogere pamoja na Mtumishi Mikenze .Mchungaji Nzogere katika moja ya kauli zake alisema “ili nchi ipate mabadiliko katika nyanja zote ni lazima ufahamu wa watanzania ubadilike, fikra tegemezi zimelididimiza taifa kwa muda mrefu, Haiwezekani pamoja na raslimali tulizonazo kama watanzania bado bajeti ya nchi haiwezi kwenda pasipo kutegemea msaada wa wahisani.

Alisema “ Haiwezekani mtu uwe na familia yako ukae chini upange bajeti ya kula wewe na familia yako kwa mwaka mzima kisha umpelekee mwanaume mwenzio ili akupe fungu la kuifanikisha bajeti yako!!!”. Tatizo hili ni la serikali nyingi za Afrika sasa ni wakati umefika kwa vijana kukua na kuondoa dhana hiyo kwa kuwa walioko juu wamejisahau hivyo inahitajika damu changa zitakazoleta mabadiliko ya dhati kwa manufaa ya Taifa na kanisa kwa ujumla”

Kwa upande wa mtumishi Daniel Mikenze yeye alielezea namna ambavyo kijana anavyoweza kupambana na changamoto za Maisha na kujiongezea kipato ikiwa ana elimu ya kutosha au ameishia darasa la saba kwa kuwa Tanzania fursa bado nyingi. Aidha Mtumishi wa Mungu na mmiliki wa shule za Sekondari za Kassa(Kassa Charity Primary&Secondary Schools) Mr Kassa, yeye aliopewa kusalimia  pamoja na mambo Mengine aliwasisitiza Vijana kufanyia kazi ufahamu uliotolewa katika kongamano hilo.

Mtumishi Kassa alisema anakumbuka aliwahi kuhudhuria kongamano kama hilo miaka ya nyuma nchi Fulani na ilimlazimu kulipia laki sita(600,000) kama ada ya kongamano. Kwa kuwa hakuwa na pesa za kutosha hivyo baada ya kulipia ilimlazimu kuwa analala ukumbi wa kongamano.kiingilio katika Kongamano hilo la Changers Conrerence 2012 kilikuwa ni sh 3000/= tu ambapo pia ilimuwezesha mshiriki kupata chakula cha mchana pamoja na usafiri wa kumtoa chuona na kumrudisha.

Mch Goodluck Kyara wa Kanisa la New Vine Christian Centre lililoko Nyegezi(Tema) aliongoza kongamano hilo kama Mc

Sehemu ya Umati wa Vijana waliohudhuria Kongamano hilo

Mchungaji Msaidizi wa kanisa la MICC Mch David Yared akiongea katika kongamano hilo

Tafes Saut Praise and Worship Team ilihudumu siku hiyo

Wanenaji wa kongamano hilo Mch Zakayo Nzogere kushoto na Mtumishi Daniel Mikenze Kulia,katikati mmoja wa waalikwa Mr Kassa kwa pamoja wakimsikiliza Mc Mchungaji Kyara alipokwa akimkaribisha mnenaji wa kwanza Mch Nzogelle

Mbeba maono wa kongamano hilo na Senior Pastor wa MICC Mch Zakayo Nzogere akihutubu

Mtumishi wa Mungu Daniel Mikenze na mmiliki wa EFFCO(PYT) LTD  akimtambulisha mkewe kabla hajaanza kufundisha.

Vijana wakiwa makini ukumbini hapo

Noel Makongompasi Masebene Mlabwa wa kwanza kulia akisikiliza kwa makini huku Mch Nyachi wa tatu kulia akifuatilia kinachoongelewa,huu ulikuwa mstari wa mwisho  ukumbini hapo.

Kongamano likiendelea

Baadhi ya wazee wa kanisa wa kanisa la MICC pamoja na timu iliyoandaa kongamano hilo wakitoa shukrani kwa wahudhuriaji kwa kuitikia wito

Mmoja ya wachungaji waalikwa akifanya maombezi kwa timu nzima iliyoandaa Kongamano hilo
Kushoto ni Brother Barnabas Shija kutoka Saint Augustine University na nyuma inayoonekana ni Tafes Praise timu ikimalizia kumtumikia Mungu siku hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...