|
Manusha Sarawan akielezea mchakato ulivyokuwa hadi kumpata Rose Muhando |
Mtumishi wa Mungu na muimbaji wa nyimbo za injili kutoka Dodoma Tanzania Rose Muhando ametangazwa kuwa msanii wa kwanza Afrika kuchaguliwa kuingia mkataba na kampuni kubwa na maarufu duniani inayojihusisha na biashara ya muziki ya SONY ukiachilia mbali wasanii kutoka nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Sonny Mama Manusha Sarawan, Mchakato huo ulishirikisha zaidi ya wanamuziki 100 kutoka barani Afrika na Rose akaibuka mshindi.Mkutano wa kumtangaza Rose mhando kama mshindi wa shindano hilo ulifanyika leo katika Hoteli ya kilimanjaro.
|
Bahati Bukuku, Diamond pamoja na Ali Kiba wakifuatilia kwa makini mkutano huo hivi leo |
kampuni za Sony na Rockstar 4000 iliyowahi kumpa msanii wa bongo fleva Ally Kiba jukumu la kufanya nyimbo ya pamoja na R.kelly ndio zimetangaza kuhusu jambo hili leo Dar es salaam.Mwakilishi wa Rockstar 4000 upande wa kipaji Afrika Seven Mosha amesema japo kwa sasa hawawezi kutaja kiwango cha pesa atakachopata Rose Muhando baada ya kupata hilo dili, mkataba wake ni wa miaka mitano.
Amesema baada ya movie zake kutengenezwa, vitabu vyake pamoja na vitega uchumi vingine ndio wataanza kutaja mapato yake.Seven amesema katika mchujo walioufanya mpaka kumpata Rose Muhando, ulihusisha wasanii wengine nane wakubwa wa Tanzania, waimbaji wa Gospel na Bongo Fleva na pia walikua na idadi nyingine kubwa ya wasanii wa nchi nyingine za Afrika kama Nigeria ambapo mwishoni mtumishi wa Mungu Rose Muhando akashika nafasi ya kwanza.
|
Wanamuziki wa injili John Shabaani na Bahati Bukuku wakimpongeza Rose Muhando ukumbini hapo. |
Katika mkataba huo, tayari Rose Muhando amerekodi album nzima Afrika kusini kazi ikiwa imesimamiwa na Sony ambapo amepata nafasi ya kushirikiana katika nyimbo na na wanamuziki wengine wakali wa gospel wa nchi hiyo ambao watatajwa hivi karibuni.
Rose Muhando amekuwa akifanya vizuri kwenye Mauzo ya album zake na kwa sasa ndiye Mwanamuziki anayeongoza kwa mauzo ya album zake nchini. Kwa mujibu wa Seven amesema mkataba huo haumfungi Rose Muhando kurekodi nyimbo zake na studio yoyote Tanzania, japo mpango wa Sony sasa hivi ni kumpeleka juu zaidi kwenye mauzo ya kimuziki Afrika ambapo atatumia lugha hiyo hiyo ya kiswahili.
|
Rose Muhando ameingia katika orodha ya wanamuziki mbalimbali wakubwa Duniani wanaofanya kazi na Kampuni ya Sonny. Music |
No comments:
Post a Comment