Pastor Donnie Mcclurkin |
Donnie
Mc Clurkin ni Mwanamuziki Mashuhuri wa nyimbo za Injili na Mchungaji wa
Kanisa la Perfecting Faith church lililo katika jimbo la Detroit nchini
Marekani.
Donnie
alizaliwa na Familia ya Bw Donald Sr na Mama Frances Mcclurkin mnamo
Jan 25 mwaka 1959 na kukulia katika mji wa Louisville. Akiwa na umri wa
miaka nane(8), mdogo wake wa kiume mwenye miaka miwili(2) aligongwa na
gari na kufa papo hapo huku Donnie akishuhudia.Wakati Donne akiwa na
majonzi mazito usiku huo huo ambao walimzika mdogo wake, mjomba wake
alimbaka Donne.
Baada
ya kifo hicho familia yake iliingia kwenye mgogoro kubwa ambao
ulitokana na utumiaji wa dawa za kulevya. Baada ya kufikisha miaka 13,
binamu yake mtoto wa mjomba wake alimbaka Donnie pamoja na dada zake
wawili kitendo amabacho kilimuumiza sana na kumuachiia kovu la aina
yake. Muda wote alijiona mkosaji, mtu aliyekandamizwa na hakuwa na
ujasiri mbele za watu na mwenye wingi wa aibu.
Kwa
kipindi hicho chote alipata Faraja toka kwa shangazi yake ambaye
alikuwa muimbaji wa nyimbo za Injili. Shangazi yake huyo alimfanya
Donnie ajiingize kanisani na kuanza kupiga piano na kuimba kwaya kama
sehemu ya kufuta machungu na kuondokana na msongo wa mawazo aliokuwa
nao. Mama yake mzazi naye alikuwa muimbaji kanisani hivyo kanisani
kukawa ndio nyumbani kwake na kambi yake pindi nyumbani kukitokea
matatizo.
Tarehe
14 Julai 1969 akiwa na miaka takribani kumi(10) ikiwa ni siku ya
jumapili akiwa kanisani huko Amityville Gospel Tabernacle mtumishi wa
Mungu aliyekuwa akihubiri aliwaambia watu kuwa “KRISTO ALIKUFA KWA
SABABU ANAKUPENDA” wazo hili hilo ndilo lilikuwa kwa Mcclurkin ndipo
akaamua kuyakabidhi maisha yake kwa Yesu. Kwenye kitabu alichoandika
kuhusu maisha yake alisema “ Kanisa limekuwa ndio ulimwengu wangu mahali
ambapo najisikia Amani na najisikia kama ndio Mahali Pangu halisi”
Mwaka
1971 wakati anamiaka 11, alikuwa akimpenda sana mwanamuziki mashuhuri
wa nyimbo za injili kipindi hicho aliyeitwa Anre Crouch. Siku aliposikia
kua Crouch anakuja katika jimbo lao alimuomba mama yake ruhusa waende
kwenye tamasha na kumuahidi jumatatu yake ataamka mapema na kwenda shule
kama kawaida. Mama yake alikubali na wakaenda Tamashani na Donnie
akaenda kukaa mbele kabisa sambamba na mamaye.
Baada
ya Crouch kuingia ukumbini saa tano usiku kabla hajaanza kuimba
alimuona Donnie na kumfata, Donnie anasema, Crouch akaniuliza kitu gain
unafanya hapa, nkamjibu nakusubiri wewe!!, akaniuliza kama nimelipenda
Tamasha nkamjibu ndio, akanambia wakati yuko mdogo hakuweza kuimba wala
kucheza mpaka baba yake alipomuobea. Nkamjibu baba yangu hajaokoka hivyo
hawezi kuniombea. Mwishoni akaniuliza kama nitapenda aniombee nami
nkamkubalia. Akaweka mkono wake kichwani kwangu akasema “Mungu mpe kile ambacho umenipa mimi” kisha akaelekea stejini. Huo ulikuwa ndio mwanzo wa hiki nlichonacho leo.
Akiwa
kanisani hapo alianzisha kundi llilokuwa linajulikana kama The
Mcclurkin Singers na baadaye alianzisha kundi lililokuwa likijulikana
kama The New York Restoration Choir. Mwaka 1983 wakati akiendelea
kutumika na kwaya alikutana na Pastor Marvin Winans. Mch Winans alivutiwa sana na namna Donnie alivyokuwa akiimba kwenye semina ya injili.
Baadaye
Mch Winans alimwalika Mcclurkin katika mji wa Detroit alikokua akiishi
ili kumsaidia kuanzisha huduma(kanisa) liitwalo Perfecting Faith
Church.Miaka sita baadaye(1989) Donnie aliamua kuhamia Detroit na
kuanza kufanya kazi na Pastor Winans. Katika kipindi hiki ndipo
Mcclurkin alipata wasaa wa kuzunguka sehemu mbalimbali na kufanya huduma
akiwa chini ya pastor Winans. Donnie anasema Familia ya Winans imekuwa
karibu sana nay eye Kuanzia Bebe, Cece, na Pastor Marvin na wakat
mwingine anafkiri yeye ni Donnie Mcclurkin Winans.
Donnie Mcclurkin na Cece Winans wakiwa wameshikilia tuzo za Trumpert awards walizopewa mwaka 2007 |
Mwaka
1991 alikuwa hajiskii vizuri kiafya, hivyo alienda Hospitali,
walipompima walimwambia kuwa anaugonjwa wa Leukemia(kansa ya damu), na
madaktari wakamwambia unahitaji matibabu ya haraka. Akawambia naombeni
mnipe siku 60 ili nkaongee na Baba yangu(Mungu). Nkawasiliana na Pastor
Andre Crouch naye akamshirikisha baba yake ambaye kwa muda huo alikuwa
Askofu jijini Califonia. Wakaomba nami nkaomba Leukemia ikaondoka,
madaktari waliponipima tena hawakuikuta tena kansa mpaka leo Kristo
amenipomya anasema Donnie.
Akiwa
na Pastor Winans, alisaini mkataba na kurekodi album yake iliyoitwa LP,
Album hiyo iliyokuwa na nyimbo kama Stand iliyongoza kwa umaarufu na
kuzinduliwa na Oprah Winfrey. Nyimbo hii ilitunukiwa tuzo ya Grammy kwa
mwaka huo wa 1996 kwa upande wa nyimbo za Injili. Album z\ake tatu za
solo zilikamata nafasi za juu sana kwenye chati za Bilboard.
Akiwa
na furaha ya ajabu Mcclurkin kupitia makongamano mbalimbali huwasimulia
watu ukweli wa maisha yake huku akipinga kwa nguvu mahusiano ya jinsia
moja. Mcclurkin anaamini kwamba suala la Homosexuality ni suala la
kiroho haliwezi tibika kisaikolojia na linahitaji msaada wa Mungu pekee.
Baada ya watu wengi kuwa wanamuomba aelezee historia ya maisha yake,
Mcclurkin aliamua kurudi nyumbani kwao Amityville New York na kumuomba
Mama yake ruhusa ili aandike kitabu kuhusu maisha yake.
Frances
Mcclurkin (mamaye), alimruhusu Donnie aandike kitabu kinachoyaelezea
maisha yake kinaga ubaga, ndipo Mcclurkin akatumia miezi 18 kuandika
kitabu hicho ambacho alikiita ETERNAL VICTIM, EXTERNAL VICTOR. Alisema
aliamua kuandika kitabu sio kwa kusudi la kuweka wazi uovu uliokuwa
ukifanyika ndani ya Familia yao bali kwa sababu yeye ni Mwalimu, na
mwalimu ni vizuri ajitoe yeye kama ujumbe ili watu wengine wajue kuwa
hawako peke yao kwenye mambo wanayopitia.
Mwaka
2008 Mcclurkin alichaguliwa kuwa miongoni mwa wanamuziki ambao watakuwa
kwenye timu ya Barak Obama katika harakati za uchaguzi wa nchini
Marekani. Mcclurkin alikubali na kujumuika na Barak Obama, lakini
kutokana na msimamo wake wa kupinga mahusiano ya jinsia moja, Mashoga
wengi walipinga kuwepo kwake kwenye timu ya Obama. Hivyo ili kupata kura
za mashoga ilibidi Mcclurkin atolewe kwenye orodha hiyo ingawa
alifanikiwa kuimba kwenye moja ya kampeni za Rais Obama.
Mcclurkin, Nofle pamoja na Mary Mary wakiwa na Rais G. Bush |
Tukutane
jumanne ijayo ili uone tumekuandalia nini cha kukujenga kupitia maisha
na changamoto za watumishi wa Mungu mbalimbali wanazo kutana nazo katika
maisha .