Friday, July 29, 2011

Makala Maalumu: kumbukumbu ya safari ya kundi la Christ ambassadors kutoka Rwanda kuja Tanzania na kuwapoteza wenzao watatu katika ajali ya Gari.

Kundi la Ambasadors of christ choir Rwanda kabla ya ajali
Ambassadors of Christ Choir ni kwaya ambayo kwa sasa inafanya Vizuri sana na nyimbo zake zimekuwa Gumzo hapa nchini. Kundi hili lenye maskani yake nchini Rwanda katika jiji la Kigali hivi sasa limetimiza miezi takribani miwili tangu baadhi ya wanakikundi hicho kufariki dunia tarehe 9/05/2011  walipokuja nchini kwa mualiko wa kwaya ya Acasia Mwenge SDA ya jijini Da es salaam.

Baada ya kupata Mualiko huo, tarehe 5/05/2011 Kundi hilo lilianza safari ya kuja jijini Dar es salaam kwa ajili ya Uzinduzi wa DVD ya kwaya ya Acasia ambao ulipangwa kufanyika katika ukumbi wa PTA ulio katika viwanja vya Sabasaba jijini Dr es salaam.

Ambassadors of Christ walifanikiwa kufika Dar es salaam tarehe 6/05/2011. Kundi hili liliweza kushiriki ibada ya sabato siku ya jumamsi ya tarehe 7/5/2011 na lilialikwa katika Interview katika kituo cha Redio cha Morning Star Adventist Radio of Tanzania kilichoko jijini Dar-es salaam  kwenye kipindi kiitwacho “LULU ZA INJILI”  ambacho hungozwa na Bro Emmanuel Maduhu.

Wakiwa Redioni hapo, kundi hili lilivutia wasikilizaji wengi hasa kwa uwezo wao wa kuimba Live. Tarehe 8/05/2011 ndio siku iliyokuwa ikisubiriwa kwani ilikuwa siku Maalumu kwa kwaya ya Acasia Mwenge SDA Kufanya uzinduzi wa dvd yao ya Pili iitwayo “MNAZARAYO” katika ukumbi wa PTA.

Kundi hilo likiimba wakati wa uzinduzi wa dvd ya acasia choir katika ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam
Watu kutoka kona tofauti tofauti za jijini Dar walifurika kutaka kuwaona vijana hawa Live wakiwa jukwaani wakimtukuza Mungu. Muda uliwadia na ndipo vikundi mbalimbali vya injili vilitangulia kuimba wakiwemo Voice of Victory wakifuatiwa na Triumph Generation pamoja na Harvesters vyote vya jijini Dar es salaam.

Muda uliwadia ambapo ukumbi mzima ulizizima kwa furaha na vifijo pindi Ambassadors of Christ walipotajwa kuwa ndio wanafuata kupanda jukwaani. Taratibu huku ala ya nyimbo yao maarufu iitwayo Twapaona vijana hawa walipanda jukwani na ukumbi mzima ulizidi kupiga kelele za furaha.

Miongoni mwa nyimbo ambazo Ambassadors of Christ walizimba Live siku hiyo ni pamoja na Kazi Tufanye, Yesu Ndiye Njia, Twapaona, Kuna Siku, Huyo ni Yesu, pamoja na nyimbo yao maarufu iitwayo Kwetu Pazuri. Watu wote waliofika ukumbini hapo walibarikiwa na kazi za kundi hili kwa utukufu wa Mungu.

Kuhusu Ajali

Baada ya kumaliza huduma tarehe 8/05/2011, kundi zima la Ambassadors of Christ lilianza safari ya kurudi Kigali asubuhi ya tarehe 9/05/2011 kwa njia ya basi. Walipofika Wilaya ya Kahama mkoani shinyanga mnamo saa tatu usiku walikutana na Lorry likiwa limepaki barabarani likiwa halina reflector yeyote. Dreva wa gari la kundi hilo hakuweza kulina lorry hilo na pindi alipoliona na  kutaka kuliovatake  ndipo lorry lingine lilikuwa likija kwa kasi hivyo wakakutana uso kwa uso na ajali ikatokea.

Hali ya Gari la kundi hilo baada ya ajali
Baada ya ajali hiyo iliyotokea  kilometa kadhaa kabla ya kufika Rwanda, wanakwaya watatu wa kundi hil Filbert Manzi, Gatare Ephraim pamoja na mtanzania Amos Fares  ambaye nayee ni muimbaji wakundi hilo aliyekuwa mbele akielekeza njia walifariki papo hapo.

Muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea serikali ya Rwanda ilituma Helkopta ya Jeshi la ulinzi la nchi hiyo [RDF] pamoja na Ambulance mbili kwa ajili ya kusafirishia wagonjwa kutoka Kahama kwenda Hospitali ya Mkoa wa shinyanga. Baada ya kufika Hospitali ya shinyanga wahanga hao waliweza kupata huduma ya kwanza na hatimaye walikimbizwa nchini Rwanda katika Hospitali iitwayo King Faisal kwa matibanu zaidi.

Helkopta ya Jeshi la ulinzi la Rwanda iliyofika kwenye eneo la ajali
Kwa msaada wa Mungu majeruhi wane wa ajali hiyo walipata nafuu na hatimaye kurutuhusiwa kutoka Hospitali. Taratibu za mazishi zilifanywa ambapo Marehemu Filbert Manzi aliyekuwa mmoja wa vingozi wa kwaya hiy na pia mtangazaji wa kitu kimoja cha Redio nchini Rwanda, pamoja na Gatare Efraimu ambaye alikuwa ni muanzilishi na kiongozi wa kwaya hiyo wa walizikiwa nchini Rwanda, wakati Mtanzania Amos Fares yeye alizikiwa nyumbani kwao  mkoani Kigoma.

Zifuatazo ni baadhi ya matukio ya kundi hilo wakati wakiimba jijini Dar na baada ya ajali hiyo.

Majeruhi
Pichani ni kijana Marc Ndizaye kabla na baada ya ajali ila yeye aliruhusiwa baada ya matibabu
Baadhi ya Majeruhi kabla na baada ya ajali
Waliotangulia
Hawa ndio watumishi waliopoteza maisha kufuatia ajali hiyo

Hili ndio kava la Album yao ambapo kushoto mstari wa juu vijana hao watatu Ephraim, Filbert, na Mtanzania Amos hawako nasi tena


Miili ya marehemu Ephraimu na Filbert ikiwa nchini Rwanda

Miili yao ikiwa kanisani

Ephraim ambaye alikuwa kiongozi na muanzilishi wa kwaya hiyo
Philbert Manzi katika siku za utumishi wake chini ya jua
Safari ya Mwisho ya Philbert Manzi

Hatimaye muda huu uliwadia na kuacha simanzi zito

 Mungu anabaki kuwa Mungu kwa lolote afanyalo juu yetu kwa ajili ya Utukufu wake

Hii ni kazi yao iitwayo NI VEMA ambayo inafanya Vizuri sana hapa nchini

 


11 comments:

  1. I AM ALWAYS BLESSED WITH THE SONGS OF THIS GROUP, ESPECIALLY KAZI TUFANYE (hapa ephraim huwa anasollo "Tufaanye"...)

    ReplyDelete
  2. May their soul rest in Peace. I'm so much blessed via this blog pia. UBARIKIWE SANA

    ReplyDelete
  3. its heart,bwana ametoa and bwana ametwaa,may they are soul rest in peace,kwa wanakwaya waliobaki wasikate tamaa cz the lord has something great for them,

    ReplyDelete
  4. jamani roho inaniuma!!!!!!!! wa2mishi hawa waliofariki,Mungu awalaze mahala pema peponi.

    ReplyDelete
  5. its very sad,we loved them but our ALMIGHTY GOD LOVE them more....

    that is the work of his hands his name be GLORYIFIED.....

    ReplyDelete
  6. Katika yote hayo, utukufu na heshima tunamrejeshea Bwana Yesu!

    ReplyDelete
  7. Really painful but it's according to God's will that they died,

    ReplyDelete
  8. Nitumie fursa hii pia kuendelea kuwapa pole sana waimbaji wenzetu katika Kristo KNY Zabron Singers

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...