Albert G Sengo |
Albert G Sengo ni mtangazaji wa Kituo cha Clouds Fm jijini Mwanza na mdau mkubwa wa Hosanna Inc, hivi karibuni amemshukuru Mungu kwa kumuokoa mwanaye aliyemeza coin ya shilingi Hamsini. Sengo alisema
Ilikuwa ni asubuhi ya Jumatatu ya tarehe 27juni2011 nikiwa na plani za kuamka saa 3 mara baada ya uchovu wa pilika pilika za siku iliyopita yaani Fiesta Mwanza stimu za usingizi zilikatika ghafla mara baada ya mke wangu kunipa taarifa kuwa my second kid Cuthbert aka Obama(3) kameza sarafu ya shilingi 50.
Huduma ya kwanza ilikuwa nikumuuliza yu hali gani na anajisikiaje:

Jibu: "nimemeza hela kama wali"
Swali: iko wapi?
Jibu: "nimetupa humu.." akielekeza kidole mdomoni
Swali: sasaaa.. huumiii?
Jibu: "mmh-mmh" akimaanisha kukataa
Ndipo pilika zikaanza kutafuta daktari ambaye alishauri kumpeleka hospitali kufanyiwa uchunguzi. Tulipita hospitali kadhaa bila mafanikio nyingi zikiwa hazitoi huduma ya X-ray kutokana na tatizo la mgao wa umeme linaloendelea nchini.
Huku na huko hatimaye tuakapata huduma ya X-ray katika hospitali binafsi inayoitwa 'Mwananchi' iliyoko wilaya ya Nyamagana mitaa ya Makoroboi nayo ikaonyesha sehemu sarafu hiyo ilipofika, madaktari wakasema kuwa ipo katika eneo lisilo la mashaka sana (kwenye utumbo kifuani) hivyo tumrudishe siku ya pili kama hatakuwa ameitoa kwa njia ya haja kubwa.
Siku ya pili X-ray ikafanyika na kuonyesha kama inavyoonekana pichani juu. Nao madaktari wakasema kuwa ipo kwenye utumbo imeshuka kidogo chini ya mbavu hivyo akatupa siku mbili kurejea kama haitakuwa imetoka. Kweli baada ya siku mbili .... Ikatoka.
Ashukuriwe MUNGU muumba wa mbingu na nchi.

X- Ray ikionyesha Shilingi Hamsini ilivyokaa mwilini mwa mtoto Cathbert |
No comments:
Post a Comment