Glorious Celebration |
Kundi hili limeanza januari mwaka huu na linaundwa vijana wapatao kama 15 pamoja na wapigaji baadhi yao ni Emmaanuel Mabisa, Daniel kibambe,Alex Kisoga Nice Marandu,Angel Bernard, Marry Igoti, Jesca Honore, Mercy Denis, Ima Griper, Aaron Botto na wengine wengi
Kabla ya kuundwa kikundi cha Glorious Celebration, kulikuwa na kikundi kinaitwa Glory to God Praise and Worship Team kilichoanzishwa 2009. Kikundi hiki kilikuwa kikiongozwa na viongozi wafuatatao: Rulea Sanga kama (Meneja Masoko), Alex Kisonga (Mwenyekiti), Emmanuel Mabisa Katibu, Merry (Muweka hazina).
Wazo la kuunda kikundi hiki lilitoka kwa Alex Kisonga ambapo aliona ni vizuri kuwashirikisha rafiki zake, Rulea Sanga na Emmanuel Mabisa, ndipo wakapanga siku ya kwanza ya kikao cha kutafuta jina la kikundi, kikao hicho kilifanyika januari 2009.katika hotel ya Tarakea iliyoko Mwenge, Dar es Salaam, Tanzania, ambapo walijadili katiba ya kikundi hicho.
Glorious Cerebration wakiwa stejini tayari kuanza kuimba |
Katika tamasha hilo Umeme ulikatika mida ya saa tano usiku, na baada ya kutafuta njia nyingine ya kufanikisha kupata umeme, jenereta nalo likagoma kuwaka kutokana na kukosa uwezo wa kusukuma vyombo vya muziki Kama wanadamu, mambo yalikuwa magumu kwa waandaji wa tamasha hilo (Rulea Sanga, Alex Kisonga na Emmanuel Mabisa),
Iliwalazimu waandaaji hao kuwatangazia wapendwa waliohudhuria kuwa tamasha limeshindika, kwahiyo watu warudi majumbani na baadae itatangazwa kulipia usumbufu huo waliopata mashabiki wao.Watu wakaanza kudai fedha zao na mneno makali ambayo kwa mtu wa kawaida ni ngumu kuyavumilia
Haikuishia hapo, baadhi ya wadai walimfuta Emmanuel Mabisa nyumbani kwake wakidai atoe pesa Kuna mpendwa mmoja alifikia kuchukua TV ya Mabisa lakini Mungu aliingilia kati na kufanikiwa kumrudishia pesa zake
Baada ya kimya kirefu cha Glory to GOD Praise and Worship Team Emma Mabisa aliamua kwenda Arusha na kujiunga na New Life Band ya jijini humo. Baadaye Mabisa aliamua kuachana na Band hiyo na kurudi Dar es Salaam, akiwa chini ya Mchungaji Getrude Pangalile Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B. Akiwa hapo aliendelea na huduma yake ya uimbaji na upigaji wa vyombo vya muziki.
Ndugu msomaji, ukiwa na wazo au maono usiache kufuatilia...Hii ndiyo iliyomtokea Mabisa baada ya kumtembelea Mchungaji Mwakang'ata na kumueleza karama aliyonayo ya uimbaji na maono aliyonayo. Mungu alimgusa Mchungaji Mwakang'ata na kuweza kumkubalia kuanzisha bendi mpya ambayo inatwa Glorious Celebration
Glorious Celebration katika Tuzo za Muziki wa Injili nchini Tanzania na hapa walishirikiana na baadhi ya waimbaji wa THT akiweno Linah Sanga kushoto |
Glorious Celebration imeundwa mwaka 2011 chini ya mchungaji Mwakang'ata amabye amekuwa msaada mkubwa sana kwa kuchangia mambo mengi kama kununua vyombo vya muziki, kutoa gari la kikundi, kuwaandalia makazi baadhi ya Wana-Glorious Celebration. Huu ni moyo wa agape.
Kikundi hiki kinawaimbaji kutoka makanisa tofauti tofauti ya hapa Tazannia, hii ni kutokana na kuwa na vionjo mbalimbali vya uimbaji na vipaji vingine ambavyo Mungu amewajalia.
Glorious Celebration ilizinduliwa April 2011 katika kanisa la Full Victory Gospel Church lililoko Chang'ombe. Dar es Salaam, Tanzania, chini ya Mchungaji Mwakang'ta. Ilikuwa ni siku ya furaha kwa watu waliohudhuria mahali pale, watu walibarikiwa sana.
Baada ya kuzinduliwa Glorious Celebration imefanikiwa kufanya huduma katika makanisa mbalimbali likiwemo kanisa la Mito ya Baraka lililo chini ya Mch Mwakiborwa pia wamewahi kufanya huduma katika kanisa la Word Alive Sinza ambalo liko chini ya Mchungaji Thadeo Lubala. Katika kanisa hilo ndipo Bw Eric Shigongo ambaye ni mmiliki Global Publishers co ltd pamoja na Atriums Hotels huabudu.
Glorious Celebtarion wakiwa jukwaani Diamond Jubelee |
Kikundi hiki pia kilialikwa katika tamasha kubwa lilofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jiji Dar es Salaam la utoaji tuzo za Muziki wa Injili Tazania. Ambapo waimbaji hawa walikonga mioyo ya watu pale walipokuwa wanapiga LIVE
No comments:
Post a Comment