Thursday, July 21, 2011

Mwl Christopher Mwakasege atoa shuhuda juu ya kifo Fanuel Sedekia


Mwalimu Christopher Mwakasege
Mwalimu Christopher Mwakasege ametoa ushuhuda huo katika semina inayoendelea sasa katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza Semina hiyo yenye somo linaloitwa namna ambavyo Roho Mtakatifu awezavyo kukusaidia ili upokee kile unachokiomba imeanza tar 19-07-2011 na inatazamiwa kuisha tar 23-07-2011.


Alisema Roho mtakatifu akwambiavyo omba hiyo haina MJADALA ni kuingia kwenye maombi mpaka upate unachokiomba kwa kuwa gharama ya kuingia kwenye maombi ili kupata ulichotakiwa kukipata ni ndogo kuliko gharama ya kukosa kile ulichoambiwa ukipate katika Maombi hayo.

Roho mtakatifu anapokupa mzigo wa kuombea jambo anakupa na muda ukizembea  muda huo ukipita kinakuwa ni kiporo, na kiporo kinaweza kikalika na kipo ambacho hakiliki.  .

“Tulipoenda Israel na Fanuel Sedekia kisha akaanza kuumwa madaktari waliniambia ubongo wake kwa asilimia tisini haufanyi kazi. Lakini walishangaa kwa nini kila mara niko pale Hospitali wakasema kwa nini usikae tu Hotelini kisha ukawa unapiga simu kuulizia hali ya Mgonjwa? Wao hawakujua kwa nini naenda pale kwa kuwa suala la kupiga simu tu sio tatizo ningeweza kurudi Arusha kisha nikawa napiga simu.

Suala hapa ni kuwa nilikuwa naenda kila mara kwa ajili ya kumfanyia maombi, nilikuwa nakaa kandokando ya Bahari ya Galilaya nafanya maombi juu ya Sedikia kwa masaa sita nikitoka hapo nasikia upako wa ajabu sana kIsha napanda Taxi kuelekea Hospitali. Nikifika Hospitali madactari na watu wa ICU walikuwa washanifahamu hivyo naenda moja kwa moja kwenye chumba cha nguo nabadili nguo kIsha naingia ICU alikolazwa.

Nikifika nambana Mungu kwa maswali Mengi namuuliza Sedekia, hivi unaongea nini na Yesu muda wote huo si urudi? na kisha namuuliza Yesu, hivi Yesu si unafahamu kuwa Sedekia anamke ukimchukua mkewe atamuachia nani? Kisha baada ya maneno hayo naweka mkono juu yake. Nilipokuwa nikiweka mkono juu yake ghafla upako wote unakuwa kama umenyonywa.

Baada ya hapo narudi hotelini naanza tena kumuuliza Mungu hivi Mungu kama basi husikii maombi yangu sikia maombi ya watanzania kwa kuwa saa hiyo nilijua watanzania wengi wanamuombea Sedekia.

Inafikia wakati nakata tamaa lakini ndani yangu najisemea Mwakasege haiwezekani jitie moyo kisha nabadili aina ya maombi, kwa kuwa nilikuwa na nguo zake pamoja na passport yake nikawa naviweka kati kisha nikawa naanza maombi ya Yeriko, nikawa niko hotelini usiku nazunguka nguo zake na paspot yake huku nikifanya maombi.

Taratibu Mungu akaanza kuniambia kuwa sedekia harudi, Kipidi hicho mimi na familia yangu tulikuwa tumepanga kwenda kupumzika nchini Uingereza wakati wa skukuu ya Chrismass,  na booking mpaka ya Hotel tulikuwa tumeshafanya, na watoto wote wako nyumbani wakijiuliza tunaendaje kupumzika wakati Sedekia anaumwa? Chrismass ikapita na mwaka mpya pia kisha Sedekia akafariki.

Baada ya kifo hicho sikuchoka nkarudi tena kwa Mungu nikamuuliza kwa nini Mungu umeamua kumchukua Sedekia mikononi mwangu? Mungu alinijibu vitu ambavyo siwezi kuvisema hapa.

Kila siku mimi ni mgeni katika maombi namhitaji ROHO anifundishe kwa upya kwa kuwa sijui vita gani ninakwenda kupambana nayo, Mungu anabaki kuwa Mungu kwa kuwa hufanya atakavyo”


21 comments:

  1. ni kweli bila roho mtakatifu uwezi kujiita mkiristo kabisaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huwa sichoki kkufuatilia mwlm Mungu wako niwaajabu sana

      Delete
  2. Asante sana Mwalimu Mwakasege kwa somo lenye nguvu na upako mwingi, kusema kweli nimebarikiwa sana tena sana na nilipo nazidi kumwomba Mungu anipe hiyo neema ya kuomba na zaidi kuongozwa na Roho Mtakatifu mana ndo nguvu ktk maombi,,,mbarikiwe sana wapendwa,,,

    ReplyDelete
  3. seminar ya mwl. mwakasege itafanyika tena lini dar?

    ReplyDelete
  4. Bwana Yesu Asifiwe sana.
    Mwalimu Mwakasege,umekuwa msaada sana katika maisha yetu,Sisi tunaishi Dar,na tumekuwa wahudhuriaji wa semina zako zote unazokuja kufundisha hapa Dar,japo si kwa siku zote za semina bali siku chache kwa kila semina,huwa tunapata angalau siku mbili,tatu.
    Tumebarikiwa sana na vitabu vyako vya mafundisho mbalimbali.
    Tunamshuhudia Mungu mwaka 2008,kwa kupitia mafundisho ya kitabu cha kumiliki na kutawala kwa njia ya maombi ambacho kinafundisha mbinu za kufaya maombi ya muda mrefu,hakika tulifanya kazi mafundisho hayo na hatimaye Roho Mtakatifu alitufundisha na kutuwezesha kufanya maombi ya muda mrefu ambayo hatujawahi kuanya katika maisha yetu yote.Tulikuwa na hitaji letu tulilokuwa tunamweleza Mungu na hatimaye,Mungu alitujibu na kutupa mzaliwa wa kwanza(lango la familia).
    Katika maombi haya ,tulijifunza sana mambo mengi na kugundua kwamba ,maombi ya muda mrefu yana siri kubwa sana ya mafanikio ambapo Mungu hujidhihirisha dhahiri kwa yote umwombayo.Jina la Bwana liinuliwe juu.
    Tumejifunza kwamba kitu kizuri huwa na vita sana,ili ukate tamaa ya kuomba(kuachilia nguvu za Mungu kwa kiwango kikubwa)sawa sawa na uzito wa jambo husika.
    Kwa hiyo, uvivu na uzito wa kusoma vitabu vya mafundisho,biblia,kuomba na kushindwa kuomba kwa muda mrefu ni mbinu atumiazo adui akijua dhahiri kuwa katka maombi hayo,kuna mafanikio makubwa,ya kudumu na ya muda mrefu .
    Ni maombi yetu ,watumishi wa Mungu muwe na afya njema na mafanikio zaidi ya kiroho na kimwili pia ili mwendelee kulisha kondoo wa Bwana.MR & MRS.Wilson Shoo.

    ReplyDelete
  5. ubarikiwe mtumishi kwa ushuhuda wakutuia moyo.

    ReplyDelete
  6. NAMSHUKURU MUNGU KWA AJILI YA KILE ALICHOKIWEKA NDANI YAKO KWANI TAIFA NA WATU WENGI WANABARIKIWA.TUNAOMBA MUNGU AKUBARIKI ILI UTIMIZE KAZI YAKE HAPA DUNIANI.

    ReplyDelete
  7. Asante kwa kuhabarisha habari za injili .Pendekezo langu ni kuhusu rangi ya block .Rangi iliyopo na haya maandishi yanaumiza macho .Jaribu kuweka rangia ambayo itafanya macho ya wasomaji yasipate tabu.

    Barikiwa

    ReplyDelete
  8. Mungu anabaki kuwa Mungu hata kama hakujibu kama ulivyoomba. It's a good message for us servant of GOD.

    ReplyDelete
  9. ``Mungu atabaki kuwa Mungu hata kama hakujibu jinsi unavyotaka'' ni ujumbe muhimu utakaosalia nadani yetu milelel namilele Amina..Barikiwa mtumishi
    Geofrey Mukozi

    ReplyDelete
  10. Langu ni kwamba, Mungu ana kusudi na kila jambo analolitenda.
    Fanuel Sedekia amekuwa wa kunivuta katika uepo wa Mungu na atazidi. Kila kuchao nahisi kwamba huduma yake, Mungu kanipa niiendeleze. Ndugu Sedekia hakuwa wa kawaida!

    ReplyDelete
  11. MUNGU NI MUNGU LEO NA HATA MILELE. HUFANYA APENDACHO KWA MUDA APENDAO YEYE NA SIO S AMEN.

    ReplyDelete
  12. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  13. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  14. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  15. Je? Unafahamu kuwa Mungu alishamtuma Eliya katika kizazi chetu, kama alivyoahidi katika Malaki 4:4-5, Naye ameshaleta ujumbe aliotumwa na kuondoka. Mungu alimtuma William Branham kama Eliya kutangaza ujio wa pili wa Kristo, ishara na miujiza iliyopita kiasi ambayo haikuwahi kutendeka hata sasa iliambatana na huduma yake, Fahamu sasa ujue ni wakati gani tunaishi na ni jinsi gani KRISTO yupo mlangoni kurudi.
    http://wingulamashahidiwakristo.blogspot.com/2016/09/mahojiana-ya-ndugu-william-branham_78.html#links

    ReplyDelete
  16. Am really touched by this story, huwa napenda kusikiza nyimbo za marehemu nikiwa hapa kenya.lile nitasema tu ni kuwa tudumu katika yesu.

    ReplyDelete
  17. Mungu akubariki mtumishi mwakasege.

    ReplyDelete
  18. Yani vile huyu mtumishi ninavyobarikiwa na mafundisho yake basi tu nibaraka tosha kwa mungu. Mungu aendelee kukutia nguvu katika utumishi wako hasa katika hizi nyakati za mwisho.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...