|
Askofu Ben Bahati toka kenya mmoja kati ya wahubiri wa mkutano |
Umoja wa makanisa jijini mwanza jana jioni umefungua rasmi mkutano mkubwa wa injiri ujulikanao kama D-Change Festival katika viwanja vya Furahisha. kusanyioko hilo lililoanza jana linatarajia kumalizika tar 30mwezi huu na limehusisha wanamuziki wa injiri toka Kenya akiwemo Solomoni Mukubwa,Anastazia Mukabwa, kundi la The Fielder-Marshals pamoja na Mhubiri na Muimbaji mkongwe Askofu Ben Bahati .Umati wa watu ulijitokeza viwanjani hapo na wengi walimpokea kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao.
Zifuatazo ni Picha za matukio ya Mkutano huo.
|
Waimbaji toka kenya Solomon Mukubwa na Anastazia Mukabwa wakisikiliza mahubiri ya Askofu Ben Bahati |
|
Mchungaji Irene Nzwalla kushoto na A. Mukabwa kulia wakimsifu MUNGU |
|
Umati wa watu ulijitokeza kusikiliza habari njema za Kristo YESU |
|
Kundi la The Field-marshals toka Kenya likimsifu MUNGU siku hiyo |
|
Anastazia Mukabwa Akiwasalimia wakazi wa Mwanza kabla ya kuimba |
|
Anastazia Mukabwa akiimba wimbo wa KIATU KIVUE mbele ya umati wa wakazi wa Mwanza,na kisha akaimba wimbo wake wa "Anayekudharau siku moja atakusalimia kwa Heshima" uliionekana kuwasisimua wengi uwanjani hapo. |
|
Solomon Mukubwa kabla ya kuimba alisema Anaheshimu kila MADHABAHU ya MUNGU iliyo katika jiji la Mwanza |
|
Solomon Mukubwa akiimba wimbo wake wa MUNGU Mwenye Enzi |
|
Sehemu ya Umati uliojitokeza siku ya Ufunguzi wa Mkutano |
|
Askofu Ben Bahati akiwaongoza watu sala ya toba kama ishara ya kumpokea YESU kama Bwana na mwokozi wa maisha yao |
No comments:
Post a Comment