Saturday, January 15, 2011

HISTORIA YA ASKOFU THOMAS DEXTER JAKES (TD JAKES)

                                     Bishop Thomas Dexter Jakes                                             
Mafundisho ya Askofu Td jakes ndio chachu kubwa iliopelekea kujulikana kwake kote duniani,naamini kama waamini wa kristo tutajifunza mengikupitia historia yake.   

Thomas Dexter Jakes alizaliwa June 9, 1957 huko South Charleston, West Virginia nchini Marekani. Baba yake Ernest Jakes alikuwa mjasiriamali na muelimishaji wa mambo mbalimbali ya kijamii. Katika ujana wake Jakes alikuwa maarufu kama kijana wa biblia(bible boy) kwenye mitaa yote ya West Virginia. Jakes hutamka ‘th’ badala ya‘s’ (lisp problem) hivyo watu wengi walimwambia hataweza kuhubiri. Baba yake alifariki kwa matatizo ya figo, muda mfupi baada ya baba yake kufariki Jakes alianza kuhubiri. Mwaka 1979 akiwa na fedha kidogo sana za kwake pamoja  na watu kumi waliomuunga mkono, walianzisha kanisa lililojulikana kamaThe Greater Emmanuel Temple of faith, huko Montgomery, West Virginia.

 Jakes alikuwa akifanya kazi ya usafi wa mitaro ya maji taka ili apate fedha za kuendeshea kanisa lake, mpaka hapo kanisa lilipoweza kusisimama lenyewe. Ndani ya miaka kumi tangu kuanzishwa, kanisa la Jakes lilikuwa na waumini wapatao1000. Mwaka 1982 Jakes aliacha kazi za usafi na kuanza kuhudumu siku nzima kwenye kanisa lake. Mpaka kufikia mwaka 1990 Jakes alikuwa ameshalihamisha kanisa lake mara mbili. Kwanza alihama kutoka Montgomery mpaka Smothers, akahama tena kutoka smothers mpaka South Charleston.

Mwaka 1993 Jakes alihamisha tena kanisa lake kwenda Cross lanes.  Mwaka 1995 akiwa na umri wa miaka 38, mahubiri yake yalianza kurushwa na vituo mbalimbali vya television nchini marekani. Mwaka mmoja baadae Jakes alianzisha Kanisa jipya lililojulikana kama Potter’s House, huko Dallas Texas, likiwa na familia zaidi ya 50 ambazo Jakes alihama nazo kutoka kanisa lake la zamani lililokuwa Cross lanes. Ndani ya miaka 12 tangu kuanzishwa, Potter’s House ilikuwa na waumini zaidi ya 30,000. 

                                                        

Familia
Mwaka 1981 Jakes alifunga ndoa na Serita Ann Jamison. Wamebarikiwa kuwa na watoto watano, Jamar, Jermaine, Cora, Sara na Thomas. Kwenye Program ya mwaka 2006 inayojulikana kama The 2006 PBS Program Africa American lives, Jakes alifanyiwa vipimo vya DNA na kuonesha Chromosomes [chembechembe za vipimo vya DNA] zake ziliashiria kuwa anatokea kwenye jamii ya watu wa Igbo ambayo kwa sasa inajulikana kama Nigeria. Uhusiano wake na Nigeria unatokea kwa bibi yake mzaa baba ambaye alikuwa raia wa Nigeria.

Marriage of his  Daughter Sarah

Bishop Noel Jones kushoto, Td Jakes na mkewe Serita siku ya ndoa ya binti yao Sarah

HUDUMA.

Jakes ni muongeaji, mshawishi na muhubiri mzuri. Mahubiri yake hurushwa Marekani na Dunia nzima kupitia television na satellite. Jakes pia ni mwandishi wa vitabu na ameandika vitabu zaidi ya 30 na kumfanya aingie katika orodha ya  waandishi bora wa vitabu nchini Marekani maarufu kamaNew York times Best Writers List. Baadhi ya vitabu vilivyompatia umaarufu mkubwa ni; Can you stand to be blessed? , Naked and not Shamed, Loose that man and let him go na Positioning yourself to Prosper Jakes pia ni muandishi mzuri wa nyimbo, Muimbaji na pia Muigizaji. Anamiliki Lebo ya kurekodia muziki maarufu kama Dexterity Sounds. Pia ana kampuni ya kutungenezea filamu ambayo imejizolea umaarufu mkubwa baada ya kutengeneza filamu kama Woman Thou Art Loosed na Not Easley Broken.

Woman Thou at loosed moja ya filamu maarufu zilizotengenezwa na kampuni ya jakes na yeye Mwenyewe kushiriki katika kuigiza, hiyo ni part ambapo Jakes anakwenda kumtembelea Michell 
                                                                                 
Jakes huandaa makongamano mbalimbali kama vile, Woman Thou Art Loosed, Manpower na God’s Leading Ladies. Kwa sasa Jakes ameyajumuisha yote na kuyapa jina moja la Megafest. Makongamano haya huudhuriwa na Maelfu ya watu kutoka sehemu mbalimbali nchini Marekani.
jarida la Time maarufu kama Time Magazine limemtaja Jakes kuwa ni miongoni mwa viongozi kumi bora wa dini nchini Marekani. Jakes ana Shahada 13 za nidhamu na Doctor of Philosophy (PhD).

Potters House kanisa analoliongoza Akofu Thomas Jakes
                                                                  

2 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...