Baba wa Mbinguni,Nasimama mbelee zako
Naleta mahitaji yangu,Sijiwezi Baba
Nimekwenda mahali pote,Sijapata Msaada
Nategemea kwako leo Unigusee tena…
" Niguse tena" ni moja ya nyimbo zilizowapatia umaarufu kundi krystaal hapa nchini
Kundi la Krystaal linaundwa na ndugu watatu, Michael Lwamba, Fabian Lwamba na Aliston Lwamba wote wakiwa ni vijana wakiume. Ndugu hao walienda kuishi nchini Canada wakitokea Zaire(DRC) huku wakiwa wamepitia majaribu mengi na ugumu wa maisha. Mwaka 1989 mara baada ya mauaji ya wanafunzi mjini Lubumbashi , ndugu hawa waliachana. Kila mmoja aliishi kivyake kwenye kambi za tofauti za wakimbizi kwa zaidi ya miaka mitano. Walipitia vitisho,magonjwa na njaa kabla ya Michael na Aliston kupata mfadhili aliyewachukua mpaka nchini Canada , akilini mwao walidhani kuwa mwenzao Fabian alikufa kwenye mauaji hayo. Fabian alikuja kukutana na ndugu zake kama muujiza huko Saskatoon Saskatchewan Canada mwaka 1997. Kitabu chao cha Keep on Standing-The story of Krystaal kinaelezea maisha yao walivyoachana mpaka walivyokutana tena Canada kwenye nchi ya ugeni
MAFANIKIO.
MAFANIKIO.
Mwaka 2004 album yao ya Keep on Standing iliwapatia tuzo mbalimbali kama; tuzo nne za MAJA zinazotolewa nchini Canada(MAJA awards) wakiwa ni Waimbaji wa mwaka, Kikundi bora na Album ya mwaka. Wameshinda mara mbili tuzo za Canadian Gospel Music Association na kutunukiwa mara nne tuzo za VIBE za nchini Canada.
January mwaka 2005 Krystaal walialikwa kutumbuiza ili kuchangisha fedha za kuwasaidia wahanga wa Tsunami,kimbunga ambacho kilizikumba pwani za Mwaka 2005, Krystaal waliimba nchini Tanzania kwenye mkutano wa injili wa Mwl Christopher Mwakasege. Walipokuwa Birmingham Uingereza waliimba kwenye Kongamano la Wabaptist mbele ya watu zaidi ya 14000 huku Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter akiwa Mgeni rasmi.
HAITI MISSION
Krystaal kwa kushirikiana na World vision,wanaendeleza mkakati wa kuwasaidia wahanga wa mafuriko yaliyotokea kisiwa cha Haiti, hii ni kwa kuuza nyimbo yao iitwayo In the name of Love kupitia I-TUNES(mtandao) na pato hilo linkwenda kwa wahanga hao..
Tangazo la Krystaal kuhimiza watu wanunue nyimbo yao ili wachangie wahanga Haiti
No comments:
Post a Comment