Nakusalimu
kwa jina la Bwana.
Imenilazimu
katika mwezi huu tuweze kujifunza jambo hili juu ya “kuomba
kwa kuzingatia muda wa kuomba”. Maombi ni somo pana sana, ndani yake kuna
vitu vingi sana ambavyo kila siku Roho matakatifu yuko tayari kutufunza kwa
kila aliye tayari kujifunza.
Hebu
leo tujifunze kwa shuhuda kadhaa;
Ushuhuda
wa kwanza;
Tarehe
18/09/2008, nikiwa mkoa wa Dare s salaam nilikaribishwa nyumba fulani kwa
chakula cha jioni na kupumzika hapo. Kwa kawaida mimi ni mpenzi sana wa
kuangalia kanda za video za vita. Baada ya chakula cha jioni mtoto mmoja wa ile
familia akaniwekea mkanda wa vita niliouchagua. Basi tukaanza kuangalia huku
tunazungumza mambo kadha wa kadha. Kama wewe ni mpenzi pia wa kanda hizo
utagundua nyingi zake huwa zinaanza na kisa fulani halafu mbeleni ndio kunakuwa
na mapambao mazuri kweli kweli, (mniwie radhi msiopenda kanda za vita, maana
najua mpo) nimelazimika kutumia ushuhuda huu ili ujumbe uweze kueleweka.
Sasa
mkanda ulipofika mahali ambapo ni patamu au pazuri kwa maana ya mapigano kuanza
ghafla nikasikia rohoni msukumo wa kuomba uliokuja kwa kasi ya ajabu.
Nikajaribu kujivuta vuta ili mkanda uishe kwanza, msukumo ukazidi kana kwamba
utafikiri kuna mtu anachochea jiko, (ndani niilijua nini natakiwa kufanya
lakini akili ilikuwa kwenye mkanda). Nikamwambia Roho mtakatifu niache nga
nimalizie mkanda ndio nikaombe. Ghafla nikaletewa kwenye ufahamu wangu picha ya
watu katika nchi fulani wanaoteseka na kuuwawa kwa sababu ya kumwamini Yesu. Ndipo
likaja swali huo mkanda na hizi roho za watu walioniamini kipi muhimu?
Nakumambia
licha ya kwamba nilikuwa ugenini nikamwambia yule ndugu niruhusu nikitumie
chumba chako kuomba kwa muda usiojulikana. Niliingia kwenye maombi usiku ule
bila kujali nipo ugenini maana rohoni nashuhudiwa usipoomba kuna roho
zinaangamizwa usiku huu. Niliomba maombi ya kumanaisha mpaka nilipoona shwari
rohoni mwangu. Nilipomaliza nakumbuka ilikuwa kama saa sita hivi, hapo
ndipo nikarudi kwenye kideo sasa, kwa raha zangu niliangali hadi saa nane.
Nasema ka raha zangu kwa sababu ule msukumoulkuwa umekwisha saa hiyo.
Baada ya
hapo tukaenda kulala kulipokaribia kucha ndipo Roho wa Yesu akanionyesha kitu
kilichotokea wakati waombaji wengine nikiwemo na mimi tulipokuwa tukiombea ile
nchi. Maana najua jambo hili Mungu aliweka kwa watu wengi siku ile na ndio
maana nimeandika na tarehe kabisa. Kristo akanishuhudia kwamba kwa kutii kule
tuliubariki sana myo wake. Nikamshukuru na kuendelea na kazi za siku
hiyo.
Ushuhuda
wa pili;
Siku
moja, Ijumaa asubuhi, wakati najiandaa kwenda ofsini ghafla ukaja msukumo ndani
yangu wa kumuombea kijana mmoja ninaye mfahamu, maana alikuwa ana kesi fulani
mahakamani na Jumatatu ya wiki iliyofuata ndiyo ilikuwa hukumu yake. So
nilichokifanya nilitii agizo la Mungu nikaanza kuomba, nikaomba kwa muda kiasi
na kisha nikaendelea na kazi zangu za siku ile. Ilipofika Jumatatu yule ndugu
akaenda mahakamani, kumbe kwa bahati mbaya alichanganya tarehe alitakiwa kwenda
ile Ijumaa na siyo Jumatatu.
Na kwa sababu hiyo mshtaki wake akawa amepewa
kibali tangu Ijumaa cha kumkamata lakini ahsante kwa Yesu hakufanya hivyo, na
baada ya taratibu nyingine za kimahakama kufuatwa wakapangiwa tarehe nyingine ya
kufika mahakamani.
Na Patrick Sanga
No comments:
Post a Comment