Monday, December 5, 2011

NAFASI YA MWANAMKE KIBIBLIA.


Mwanzo 1:27 ‘Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wa Mungu alimwumba,mwanaume na mwanamke aliwaumba. Sikiliza mahali popote pale mwanamke ni mtu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa katika kufanya mambo kuliko hata mwanaume.Ikiwa ushawishi huu utatumiwa katika mpango wa Mungu basi kusudi la Mungu litatekelezwa.

Mungu hakumwumba mwanamke kwa bahati mbaya au makosa,kila ambacho Mungu alikifanya ,alikifanya kwa kusudi.kwa lugha nyingine kila ambacho Mungu alikifanya maana yake moja kina nafasi mbele zake na mbili kuna wajibu ambao Mungu aliweka ili utekelezwe na hicho kitu.


Lengo la ujumbe huu ni kukueleza nafasi ambayo Mungu amempa mwanamke katika kanisa,jamii,nchi,ndoa na nk na wajibu wa yeye kutekeleza katika nafasi hiyo:-
1.Mungu anamtazama mwanamke kama msaidizi wa mumewe . Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema si vyema huyo mtu awe peke yake,nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”. Tangu kuumbwa kwa Adam,mpaka Mungu kumletea Eva inasemekana miaka mingi ilipita hapa katikati.Sasa tunajua katika ile sura ya kwanza na ya pili ya kitabu cha mwanzo,Mungu alikuwa amempa Adam wajibu wa kutekeleza.

Ikafika wakati Mungu akaona ule wajibu ni mkubwa sana kwa Adam kuutekelekeza ndipo akampa Eva.Kitu Mungu anataka tujue hapa ni hiki,wajibu aliopewa Adam peke yake asingeweza kuutekeleza bila Eva,maana yake nafasi ya Eva kwa Adam ilikuwa ni ya muhimu zaidi.Pasipo Eva,Adam angeshindwa kutekeleza wajibu.

Sasa hata leo katika ndoa,kanisa Mungu ameweka wanawake ili wawe wasaidizi katika majukumu ambayo Mungu amewapa na waume zao au wachungaji wao makanisani.

2. Mwanamke kama mlinzi wa agano na kusudi la Mungu. Mithali 14:1 “ Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake ; bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe” , Mwanzo 3;13 “ Bwana Mungu akamwambia mwanamke ,nini hili ulilolifanya ? Mwanamke akasema nyoka alinidanganya ,nikala”..


Ndoa ni agano la Mungu kwa wanadamu. Mlinzi wa agano kimsingi ni mwanamke. Mara nyingi shetani akitaka kuvuruga ndoa atatafuta mpenyo au nafasi hiyo kwa mwanamke ili asambaratishe ndoa hiyo.Sasa mwanamke yupo ili kulinda kusudi hilo.Asipokaa kwenye nafasi yake ya ulinzi basi ajue kwamba kusudi la Mungu la kuwaunganisha halitatimia.
Nisikilize ndoa yoyote inapovuruguka ujue mwanamke hakusimama vema kwenye nafasi yake ya ulinzi. Ngoja nikuonyeshe kitu hiki. Adam na Eva walipokula tunda ambalo Mungu aliwaambia wasile , kila mmoja wao aliulwiza swali lake. 

Adamu aliulizwa uko wapi? Mwanzo 3:9, na Eva alimwambia Mwanamke ni nini hili ulilolifanya , Mwanzo 3:13.Ipo tofauti kubwa sana katika haya maswali mawili.Swali la Adam lilimaanisha kwa nini haupo kwenye nafasi yako? Na swali la Eva lilivuka hapo na kumaanisha kwa nini hujafanya ulilotakiwa kufanya yaani kulinda agano.Mahali popote mwanamke ulipo ikiwa ni katika ndoa ,kanisa ,jamii,nchi, jifunze kulinda kusudi la Mungu ambalo unajua Mungu amekuagiza . jifunze kupitia mama yake Musa , yeye alilinda agano la wana wa wa Israeli kwa kumficha Musa na kuhakikisha hafi maana alijua Musa hakuzaliwa kwa bahati mbaya. Kutoka 2:1-10. 


Na; Patrick Samson Sanga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...