Friday, December 16, 2011

Washindani Wa Tuzo za Grammy Watangazwa



Grammy Awards ni tuzo zinazoheshimika ulimwenguni kote na huenda ndio Tuzo Mashuhuri kuliko tuzo zote katika Tasnia ya Muziki duniani. Tuzo hizi hujumuisha aina mbalimbali ya Muziki ukiwemo muziki wa Injili. Mapema wiki hii majina ya washindani wa categories zote yalitangazwa huku tuzo hizo zikitegemewa kufanyika 12-Feb-2011 Los Angles nchini Marekani. 

Hii itakuwa ni mara ya 54 kwa Grammy Awards kufanyika, Kwa upande wa Muziki wa injili kuna categories mbili (a) Nyimbo Bora ya Injili ya Mwaka (b) Album Bora ya Injili ya Mwaka.Katika katika Tuzo zote mbili Kirk Franklin na Marry Marry ndio wameonekana kidedea kwa Majina yao kutokea kuwania tuzo zote mbili.

"Best Gospel Song"

Marry Marry ("Sitting With Me")

Donald Lawrence ("Spiritual")

Kirk Franklin ("Hello Fear")

Richard Smallwood ("Trust Me")

Canton Jones ("Window").

"Best Gospel Album"

Kim Burrell (The Love Album)

Kirk Franklin (“Hello Fear”)

Andrae Crouch (The Journey)

Marry Marry (“Something Big respectively”)

Trin-i-tee 5:7 (Angel & Chanelle Deluxe Edition)

Chakushangaza hapa ni kwamba wakati watanzania wengi bado wakiwakubali wakongwe kama Doen Moen, Ron Kenorly, Paul Baloche na wengine wengi, ukweli ni kwamba kwa sasa kuna damu nyingi changa zifanyazo vizuri, huku wakongwe hao wakibakiza heshima katika jamii kwa utumishi wao mbele za Mungu.

Kirk Franklin na Marry Marry


2 comments:

  1. Jamani, naomba mnisadie kuelewa nahisi labda
    bado ni mchanga sana; je kupokea tuzo ni
    kibiblia? Binafsi huwa naona kama ingekuwa
    vizuri waimbaji kama watumishi wengine pia
    wangesubiri kupokea tuzo mbinguni. Msikwazike
    wapendwa, nahitaji tu kueleweshwa zaidi.

    ReplyDelete
  2. Mtumishi sio kila kitu kipo kwenye Biblia, ila kikubwa hapa tunaangalia lengo hasa la Tuzo hizo, naamini lengo ni kupeana changamoto ili watumishi wafanye kazi nzuri zaidi kiuimbaji. Lakini Mwisho wa siku mwenye kupima Mungu na ni kwa Vigezo vyake

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...