Saturday, January 28, 2012

Mwakasege akosoa mfumo wa elimu ya juu.


Mwl Christopher Mwakasege
Mwl Christopher Mwakasege, amesema mfumo wa elimu inayotolewa hapa nchini haiwezi kuwajenga Watanzania katika kukabiliana na ushindani kwenye soko la ajira.

Mwakasege ambaye ambaye amemaliza semina yake mkoani Kilimanjaro  kwenye uwanja wa mashujaa, Mwl Mwakasege alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika semina maalumu iliyohusu “UELEWA WA KUSUDI LA MUNGU KATIKA MASOMO”.
Semina hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa mpira wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS) na kuhudhuriwa na na mamia ya watu wakiwemo wanafunzi wa chuo hicho.

Huku mahubiri yake yakionekana kuwagusa wanafunzi wengi, Mwakasege alisema mfumo wa elimu unaotolewa hapa nchini unalenga kuandaa viongozi na si wataalamu.
Alisema Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa na maono kwa kuanzisha Chuo cha Kivukoni ambacho kilikuwa mahsusi kwa ajili ya kuandaa viongozi na haikujalisha kama walikuwa wamesoma sana.

Alisema kutokana na mfumo wa kisiasa kubadilika baada ya Tanzania kuridhia mfumo wa vyama vigi vya siasa, Chuo cha Kivukoni kwa sasa kimebaki kuwa cha kupika makada wa chama.

Aliwataka wasomi hao kujiuliza kwa nini wanasoma na wanafanya hivyo kwa ajili ya nani na kuongeza kuwa elimu ni mfumo uliotengenezwa kuunganisha sekta mbalimbali katika mamlaka za mataifa mbalimbali duniani.

Alisema kila taifa linao mfumo tofauti wa elimu na kutolea mfano elimu ya Marekani ambako alidai ili uwe daktari sharti usome kwa miaka saba na baada ya hapo ufanye kazi miaka mitatu ukiwa chini ya daktari mtaalamu kabla ya kuhalalishwa kuwa daktari kamili.
Mwakasege alidai kuwa tofauti na Marekani nchi nyingine ikiwamo Tanzania madaktari wanasoma miaka mitano na baada ya hapo wanakuwa madaktari kamili.

Naye mwenyekiti wa maandalizi ya semina hiyo, Paul Makonda, alisema katika semina hiyo kuwa taifa haliwezi kuendelea pasipo watu wake kufuata mafundisho ya Mungu.

Paul Makonda
Hosanna Inc ilifanikiwa kuongea na Mtumishi wa Mungu Komredi Paul Makonda ambaye ni mwanafunzi(MUCCoBS),na ni Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Mkoani Kilimanjaro na pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu nchini Tanzania (TAHLISO). Makonda Nini hasa kilichopelekea wanafunzi wa (MUCCoBS)  kuandaa semina hiyo na hiki ndicho alichotuhabarisha.

Paul Makonda: Kuna uhusiano mkubwa kati masomo tunayosoma vyuoni na kusudi la Mungu juu ya Maisha yetu, hivyo kwa kulitambua hivyo ikabidi tumtafute Mwalimu Mwakasege kama mtumishi wa Mungu aweze KU-LINK hilo suala, i mean uhusiano uliopo kati ya Kusudi la Mungu na Masomo tunayosoma.

Kaka skufichi Mwakasege alitisha, alielezea kwa kina akitumia Kitabu cha Daniel pamoja na Habakuki, aligusia mambo mengi ikiwemo kwa nini watu wanasoma digrii nyingi anaanza na hii kisha anabadilisha.

Source: Tanzania Daima, Hosanna Inc

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...