Rais Jonathan ambaye ni mkristo na jina lake la kati anaitwa Ebelechukwu likimaanisha “Rehema za Mungu” amesema inawezekana kuna viongozi wa serikali yake ambao wanatumika kupeleka habari katika kundi la Boko Haram ambalo kwa muda sasa limekuwa likidaiwa kufanya mashambulio katika makanisa pamoja na ofisi za serikali. Kwa mujibu wa CNN wananchi kwa hasira wamekuwa wakitembea barabarani wakiwa mamebeba mabango na majeneza ya kebehi yakiwa na maneno yasemayo President Badluck.
Wananchi wamekuwa wakihoji kwa nini mashambulio hayo yanazidi kutokewa pasipo viongozi wa juu wa ulinzi nchini humo wakiwa hawajawajibishwa. Mashambulio hayo yanadaiwa kusababisha kuyumba kwa umoja wa raia wa nchi hiyo.
Mch Ayo Oritsejafor |
Wiki iliyopita bomu moja lililodaiwa kulipuliwa na kundi la Boko haram lilipoteza uhai wa jumla ya raia 150 katika jiji la kano nchini humo. Rais Jonathan ambaye amekuwa akitumia ukurasa wake wa facebook kutoa maoni yake kwa muda sasa amekuwa kimya huku watu wengi wakimuandikia comments za lawama kwa kutochukua hatua kali dhidi ya mashambulio hayo kwa wakristo.
Source: Christian post
No comments:
Post a Comment