Wednesday, January 4, 2012

Viongozi wa Dini Nchini Uganda walalamikia Kitendo cha Mchungaji Kumwagiwa Tindikali


Mchungaji Umar Mulinde kabla hajashambuliwa kwa Tindikali
Viongozi wa Dini nchini Uganda wamelalamikia kitendo kilichofanywa na watu wasiojulikana cha Kumwagia Tindikali(Acid) usoni Mchungaji Umar Mulinde wa kanisa la GOSPEL LIFE CHURCH lililoko jijini kampala nchini humo.Kitendo hicho kilifanyika siku ya mkesha wa Christmas (Christmas Eve)  mara baada ya kumaliza kuongoza Ibada kanisani hapo.

Mch Umulinde alipata shambulio hilo majira ya saa tisa alfajiri baada ya mkesha kumalizika na baadaye aliwahishwa kupelekwa Hospitali na washirika wake katika International Hospital Kampala. Kwa Mujibu wa New Vision  Babaake na Pastor Umar alikuwa ni Imam na Mch Umar Mwenyewe alikuwa Sheikh kabla hajamkabidhi Yesu Maisha kama Bwana na Mwokozi wa Maisha Yake.

Mchungaji Umar Mulinde akiwa Hospitalini
Baada ya Mch Umar kuokoka alipata vipingamizi vingi kutoka katika familia yake yenye msimamo mkali na dini ya Kiislamu. Shambulio hilo limepelekea Mchungaji Umar  kupoteza uwezo wa kuona wa jicho lake la kulia, huku upande wa kulia wa sura yake ukiwa umedhurika.

Akielezea tukio hilo akiwa hospitalini Mch Umar anasema baada ya kutoka kanisani kuna mtu mmoja alinifata akijifanya mkristo na kuniita kwa nguvu Pastor,  Pastor, Pastor, nilipogeuka kuangalia ninani anayeniita  ndipo aliponimwagia Tindikali usoni, nilipogeuka baada ya kumwagiwa mtu mwingine akanimwagia tena tindikali mgongoni kisha akakimbia akisema “Allah Akbar”( Mungu Mkubwa)”

Mch Umar amekuwa akiendesha mikutano ya Injili na kuwaambia watu wote hususani waislam wamgeukie kristo kama alivtofanya yeye. Kwa muda wote ambao yuko Hospitali Mch Amar amekuwa akiuguzwa na mkewe ambapo watumishi wengi nchini humo wamefika na kumuangalia pamoja na kufanya maombi.

Mchungaji Umar Mulinde akiwa na mkewe hospitalini

Mchungaji Umarakionyesha nguo zake alizokuwa amevaa wakati anashambuliwa

Mchungaji Umar Mulinde akiwa Hospitali Baada ya Shambulio

Mchungaji Umar Mulinde akiwa katika moja ya mikutano yake akitangaza Habari njema za Ufalme wa Mungu

Source: Christian Post and Uganda Media

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...